My week end is super crazy

naona upo blessed nenda nao tu taratibu

utayamiss hayo makelele 🥰🥰
 
Asante🙏🏼

Wadogo wanafurahisha sana.
Hasa ile kuona jinsi wanabadilika kidogo kidogo tokea wako wachanga ni burudani na faraja sana na ndio inafanya mtu utamani kuwapa malezi bora sbb hutamani kuona wakiharibikiwa.

Hapo kwenye u teenager panaogopesha😀 ila naamini teenager mwenye malezi bora anaweza kuvuka hiyo hatua salama kuliko asiye na malezi mazuri
 
Ila nahisi naanza kuzoea sarakasi zao😀😀
Nawamiss ule muda wako shule na mimi niko kwa mishe.

Pamoja na yote wakiondoka naamini ndo nitakonda😀😀
Why don't you find your own twins if you sometimes miss them? Have your own twins
 
Sasa hivi akiharibika wanakusaidia kumharibu zaidi.Hawajui wakimuokoa watasaidia asiharibu na wa kwao

Asante mkuu.
Nitajitahidi kijana achangamane zaidi japo huwa anapatana akiwa na wa umri wake
 
Ila maisha haya jamani, mie katv kamoja tu ni kamgogoro. Ila kuna watu wananunulia kila mtoto na tv yake😭😭😭
 
Ila maisha haya jamani, mie katv kamoja tu ni kamgogoro. Ila kuna watu wananunulia kila mtoto na tv yake😭😭😭
Unatakiwa kuwa na TV mpaka ya akiba stoo ikiharibika moja hata hununui nyingine unachukua tu stoo 🤣🤣🤣
 
Unatakiwa kuwa na TV mpaka ya akiba stoo ikiharibika moja hata hununui nyingine unachukua tu stoo 🤣🤣🤣
Mweh mweeeh mweeeh! Ngoja kwanza nijipige pige ninunue hata hako kamoja kwanza.
 

Babu Yao alishatuacha kitambo. Ila hua nafurahia sana kuwa nao...
Juzi kakiume kamekuja kananiambia nisome kitabu kimeandikwa how to use your money wisely! Kamekomaa Daddy you must read that book, you real need it. Nikashangaa...nikamuuliza why? Sasa Kuna siku niliinunua machungwa mengi safarini kumbe nimepigwa hayakua mazuri, wakaishia kuyatupa.

Kingine Ile kununua vitu Kwa bulk anaona kama tunanunua vitu tusivyovitumia. Anasema tununue kidogo kidogo kikiisha, tunanunua kingine. Ikabidi Mama yake aingilie kati kwamba hivyo ni vitu vya mwezi mzima, sie tunajua Kila kitu kinahitajika kiasi Gani kwa mwezi.

Siku hizi nikipata muda tunaenda kutembelea watoto yatima, Mara Moja Moja tunaenda kusabahi Bibi, waone maisha mengine yalivyo.

Hapa nilisafiri navyo mkoani vikasema havili chakula Cha hotelini, ikabidi kufungaisha mazagazaga kutoka nyumbani.

 
Sasa hivi akiharibika wanakusaidia kumharibu zaidi.Hawajui wakimuokoa watasaidia asiharibu na wa kwao

Asante mkuu.
Nitajitahidi kijana achangamane zaidi japo huwa anapatana akiwa na wa umri wake

Afadhali imekupa uzoefu mpya na kujifunza mambo mapya hasa namna bora ya kumlea kijana awe tayari kuishi mazingira tofauti tofauti.
 
naona upo blessed nenda nao tu taratibu

utayamiss hayo makelele 🥰🥰
Naenda nae polepole dear.

Kuna saa natamani nivitupe nje ila siku wakiondoka nitahuzunika
 
Ila maisha haya jamani, mie katv kamoja tu ni kamgogoro. Ila kuna watu wananunulia kila mtoto na tv yake😭😭😭
Wala usijali sana yawezekana nina ma tv mengi ila na wewe una kitu hata nikiuza hizo tv zote siwezi kukipata.

Pia maisha ni furaha.
Kuwa na ma tv mengi haimaanishi mtu ana furaha.
Kama una furaha ushayapatia maisha.
 
Watoto wa hichi kizazi wana ujasiri na hawaigopi kusema.
Sio kama sisi tumekuzwa na hofu na kuwekewa kutojiamini.

Hayo maneno angeambiwa baba wa enzi za utoto wangu sipati picha😀

Naamini hawa watoto wetu ndo watakaoleta mabadiliko ambayo sisi wazazi wao tunayatamani lakini tunaogopa kuyapambania.
 
Ujue unaweza kumchukulia poa huyo dogo alivyoumia kuona matunda mengi yanatupwa hadi kukushauri usome hicho kitabu ila ameonesha kuwa na kitu kikubwa ambacho hata watu wazima wengi hawana.

Sio kawaida kwa mtoto wa umri huo kuonea huruma pesa.Kuna watu wazima wanatupa chakula,wanatumia vitu vibaya hasa vikiwa vingi ndani hata hawajali sbb vikiishwa vinaletwa vingine .
Hao madogo hao nimewapenda.
Hongea kwa baba na mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…