Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante🙏🏼Pole sana.
Ila mimi nimefikia stage natamani sana watoto, hususan wadogo kabisa wale ambao mtu anaweza kuwalea vizuri yeye mwenyewe.
Ila tatizo siku hizi hata ukiwalea vizuri utotoni wakifika kwenye u teenager wanakubadilikia 😂😂😂
Why don't you find your own twins if you sometimes miss them? Have your own twinsIla nahisi naanza kuzoea sarakasi zao😀😀
Nawamiss ule muda wako shule na mimi niko kwa mishe.
Pamoja na yote wakiondoka naamini ndo nitakonda😀😀
Sasa hivi akiharibika wanakusaidia kumharibu zaidi.Hawajui wakimuokoa watasaidia asiharibu na wa kwaoZamani ndio mtoto alikua wa jamii, Kwa Sasa ulezi umekua mgumu sana.
Wangu nawapenda sana, na wao wanalijua hilo, lakini pia wanazingatia kwamba wakikosea kipigo chake utafikiri wamevunja chungu chenye mboga ya familia.
Pole sana Kwa heka heka. Lakini huyo wako pia ukipata nafasi, mfanye achanganyike na wengine kidogo, itamsaidia sana.
Unatakiwa kuwa na TV mpaka ya akiba stoo ikiharibika moja hata hununui nyingine unachukua tu stoo 🤣🤣🤣Ila maisha haya jamani, mie katv kamoja tu ni kamgogoro. Ila kuna watu wananunulia kila mtoto na tv yake😭😭😭
Mweh mweeeh mweeeh! Ngoja kwanza nijipige pige ninunue hata hako kamoja kwanza.Unatakiwa kuwa na TV mpaka ya akiba stoo ikiharibika moja hata hununui nyingine unachukua tu stoo 🤣🤣🤣
Hahaaaa.
Unawaambia tu "shukuruni nyie si watoto wa baba yangu, mngekuwa watoto wake hilo suala hata msingelifikiria".
Tatizo wakimtafuta babu kumuuliza (kama yupo bado) naye wanamkuta kalainiiiika uzeeni siyo yule wa kipindi kile😂😂😂
Sasa hivi akiharibika wanakusaidia kumharibu zaidi.Hawajui wakimuokoa watasaidia asiharibu na wa kwao
Asante mkuu.
Nitajitahidi kijana achangamane zaidi japo huwa anapatana akiwa na wa umri wake
Wala usijali sana yawezekana nina ma tv mengi ila na wewe una kitu hata nikiuza hizo tv zote siwezi kukipata.Ila maisha haya jamani, mie katv kamoja tu ni kamgogoro. Ila kuna watu wananunulia kila mtoto na tv yake😭😭😭
Do it while you still can, time is irreversible.Nikipata twins sijui nitafurahi kiasi gani.
Tena wawe wa kike.
Ningevigeuza mdoli😀
Watoto wa hichi kizazi wana ujasiri na hawaigopi kusema.Teenager mbali sana kaka, kwanza vina tambua haki zao na ipeo mkubwa sana wa mambo.
Mfano vijamaa vyangu vinapenda sana vipikiwe chips, Sasa tukakubaliana kwamba, wakila chips mchana, usiku wale chakula kingine.
Siku hiyo taarifa inatolewa, vinasema but that is not fair, how can you make a decision for us? You should have called a meeting...wakati huo vitoto hata miaka 10 havijafikisha.
Mh borea ujawa mama angu 🥲Walete kwangu nikusaidie kuwachapa. Mie wangu napiga mpaka nauma na meno ...
Ujue unaweza kumchukulia poa huyo dogo alivyoumia kuona matunda mengi yanatupwa hadi kukushauri usome hicho kitabu ila ameonesha kuwa na kitu kikubwa ambacho hata watu wazima wengi hawana.Babu Yao alishatuacha kitambo. Ila hua nafurahia sana kuwa nao...
Jusi kakiume kamekuja kananianbia nisome kitabu kimeandikwa how to use your money wisely? Kamekomaa Daddy you must read that book, you real need it. Nikashangaa...nikamuuliza why? Sasa Kuna siku niliinunua machungwa mwrngi safarini kumbe nimepigwa hatakua mazuri, wakaishia kuyatupa.
Kingine Ile kununua vitu Kwa bulk anaona kama tunanunua vitu tusivyovitumia. Anasema tununue kidogo kidogo kikiisha, tunanunua kingine. Ikabidi Mama yake aingilie kati kwamba hivyo ni vitu vya mwezi mzima, sue tunajua Kila kitu kinahitajika kiasi Gani.
Siku hizi nikipata muda tunaoenda kutembelea watoto yatima, Mara Moja Moja tunaenda kusabahi Bibi, waone maisha mengine yalivyo.
Hapa nilisafiri navyo mkoani vikasema havili chakula Cha hotelini, ikabidi kufungaisha mazagazaga kutoka nyumbani.
View attachment 3108343