Ulweso
JF-Expert Member
- May 24, 2016
- 23,111
- 28,020
OKGod forbid
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
OKGod forbid
Okay tufanye hivi mimi sina degree, ni wewe tu ndio una degree na una akili nyingi sana mkuu.Serikali haina Dini.
Ndio maana hiyo degree yako inatia Shaka Sana.
Unashindwa kufanya uhusisho wa hoja zako.
Secular state haiwezi kukupangia mambo ya Dini kwani yenyewe haina Dini.
Lakini Non-secular state kama Iran au Saudia Arabia au Qatar wao watakuambia na kukulazimisha ufuate sheria za Dini yao
Ushetani tuHapana mkuu, ukiona mwanamke ana uwezo wa ku reason maswala ya kiimani huyo ni level nyingine. Nadhani jf nzima hawazidi 10.
Sawa mkuu. So hata wazazi wakiamua nikafanyiwe FGM ni sawa tu kwakuwa ninaishi kwao.Unaishi chini ya paa la mzazi wako, kama hutaki si unahama tu mkuu. Ukiwa chini ya mzazi utafuata kanuni zake ukiona waweza jitegemea basi hama.
Mimi nlikuwa naenda kansani nikiwa kwa wazazi now nina miaka sijui mingapi sijakanyaga
Kadegree kamoja ashamkana MunguWewe ndiye huna Uelewa.
Mama yako anauelewa ndio maana alikusomesha, sasa anashangaa mwanaye kasomea ujinga.
Ribbon allianceMambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.
Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.
Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.
Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.
Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"
Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"
Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"
Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"
Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"
Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.
Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.
Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"
Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.
Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.
Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana
Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"
Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.
Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?
Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
I see that now.Acha kubishana na akili fupi , huwezi bishana na wapumbavu waliokuwa brainwashed ,ni ngumu .Utamaliza nguvu zako bure . Let them believe the garbage that they want to .
Nyota zimejiumba kwa hiyo?Ndo nakuambia tenga dakika 5 tu, toka nje angalia nyota, fikiria kwa makini ukiwa umefungua ubongo. Naamini utarudi kuwa atheist. Karibu sana.
Hiyo ni imani yako. Sikulazimishi uamini nachokiamini mimi...Lakini mbona wewe unataka kunilazimisha niamini unachoamini wewe kuhusu kwenda ibadani?Kama ulicho andika unamaanisha nakwambia iko siku utayakumbuka maneno ya Mama yako nakutamani ungeanza mapema kwenda ibadani
Subiri uzae wa kwako Mama wasijue mlango wa kanisa ama msikitiTunaishi chini ya paa la serikali inayotuongoza...Je ni haki serikali kutulazimisa wananchi wote kuwa waislam?
Tunaishi kwenye dunia ya Mungu, Je Mungu anatulazimisha kumuamini na kwenda kanisani?