Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Acha ujuaji ndugu swala la kuamini au kutokuamini ni lako na ufanye maamuzi unayotaka kujiskia wewe ukiwa kwenye himaya yako sio kwenye himaya ya mtu
Kama mzazi anaona ni sawa kukuelekeza kwenye njia anayoona kwake inafaa hata kama wewe unaona anakupotezea Muda wako
Ile hali ya kua unaishi kwake fuata maelekezo unayopewa tofauti na hapo tafuta kwako upangiane hizo ratiba na mumeo
 
Duh, okay mkuu uko sahihi.

Inashangaza mtu unafikisha miaka 20 bado hujui mambo madogo Kama hayo?

Hata Rais Samia akifika NYUMBANI kwako lazima afuate sheria zako bila kujali Urais wake.

Ndio maana Hata Magufuli alipokuwa akiingia msikitini alikuwa anavua viatu licha ya kuwa yeye ni Mkristo na haamini katika kivua viatu ukiingia Nyumba za Ibada.

Elewa kuwa kila Jambo linamipaka yake.
Hata Wewe ukiwa na familia yako ukaweka sheria, mama au Baba yako akija kwako atafuata sheria za Nyumba yako.
Bila kujali anaamini au haamini.

Hataki aondoke.
Sijui wapi unakwama
 
Wa kike huyu mkuu
 
Huwezi kumuamulia mtu anaekufanya ulale, ule, unye na uwe na nguvu ya kupost mitandaoni. Mtoto Kwa mama hakui ndiomaana hata ukioa Kuna mazingira utamhitaji tu kwahiyo usije ukaharibu uhusiano na mzazi kisa ujeuri wako.
Sawa nmekupata
 
Watu wengi walio magerazani ni watu wenye dini zao, watu wengi wanoharibu nchi ni watu wenye dini, watu wengi makatili na wadhulumaji ni wana dini.
Huyo brainwashed ndiye kamzaa na kumpa hiyo degree , sasa huyu malezi ya mwanaye yatakuwaje, kama hayatakuwa ma'mpotompoto.
 
Mtu anaweza kudhani kabisa nawewe ni critical thinker
 
uzi hauhutaji ushauri kiivo,as long as unaishi kwangu utafata matakwa yangu,unataka kujitawala tafuta mji wako,ondoka hapo kwenu kajitawale
binafsi ningeshakufukuza kwangu,
 
Hayo mengine utajua wewe na Mungu wako ila as long as upo kwa wazazi tii kile unachoambiwa hata kama utafanya kumridhisha tu ila mtii mzazi ndo Mungu wa duniani.
 
Ni kweli
 
Watu wengi walio magerazani ni watu wenye dini zao, watu wengi wanoharibu nchi ni watu wenye dini, watu wengi makatili na wadhulumaji ni wana dini.

Ndio maana nikamuambia mwenzako kuwa kama anaupeo mdogo WA MAMBO aache kujadili mambo makubwa.

Na Wewe upo kundi Hilo Hilo.

Kama hujui tofauti ya mambo haya jua unaakili mgando.
1. Dini Vs Imani
2. Elimu Vs Akili
3. Urembo Vs Uzuri
4. Mapenzi Vs Upendo

Mfano yeye amesoma mpaka Degree hivyo anaelimulakini Hana Akili

Yeye kuambiwa aende Kanisani haimaanishi awe na Imani na Dini au Kanisa Hilo.
Hapo ni suala la mamlaka na taratibu za familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…