Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Naomba nikuulize kwa nia njema kabisa!! JE UNAAMINI KUWA MUNGU YUPO???
 
Kwahyo mama/Baba akiamua sasa nikafanyiwe tohara ni sawa kwakuwa ni mamlaka na sina uhuru wa kuchagua???

Wala sishangai wengi unaowaita 'wasomi' na wasio wasomi wakinishangaa....sijaandika kwaajili yao. sijaandika hii kwaajili ya average minds Nimeandika kwaajili ya wale wachache watakaonielewa. (Above average)
Zingatia hii graph
 
Kua na Age 18+ au 18- Sio kigezo cha kua na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.. Kuna wengine wana30+ lakini bado ni wa hovyo tu... Kua uyaone!!

NB: Kua makini sana na Unayosikia, Unayotizama na Unayosoma..
Kwahyo kigezo cha kumpa mtu uhuru wa maamuzi kwakuwa amekua ni kipi? (Kama sio umri)
 
Umesoma vitabu gani? Vitaje nataka nisome.

Unaishi na mama pekee au huko nyumbani yupo na baba? Naomba nifaham ili nitoe ushauri.
 
Kabisa na ukitaka kujua upumbavu na udumavu wa akili wa mtu mweusi ,we soma hizi comments humu .
Kuna quote nimesahau nani alisema "Religion can make even a proffesor act foolish"
Yani kabisa bado karne hii unakuta professor anaamini akifumba macho akasali kuna invisible force in heaven itamsikia na kumletea majibu. Na isipomjibu ni "mapenzi yake yatimizwe"
 
Ukitaka uhuru basi jitegemer uwe na kwako, mimi hapa nina miaka karibia 10 silijui kanisa na hakuna mtu ananiuliza.

Ukikaa kwa watu fuata masharti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Masharti mengine yote sawa. ila hili naona linahusiana na imani. Sasa mtu umlazimishe kuamini kitu fulani ni haki?
Yesu alishikisha watu mapanga akawalazimisha kuamini dini yake?
 

Husianisha mada yako ni hiki ulichoeleza hapa kwenye maoni haya.
Ndio maana nikakuambia itakuwa maajabu Kama kweli Una Degree.

Nitajie Kanisa au dini yoyote inayotaka FGM,
Unajua unapotoa hoja unatakiwa utumie AKILI ili kuepuka kudharauliwa!

Unaeleza hiki unarukia hiki, unashindwa kufanya Reflection Kama msomi?

Kukaa nyumbani Kwa mtu lazima ufuate sheria zake,
Elewa sheria za watu na kwenye familia zinagaidiwa/zinaongozwa na sheria za nchi pamoja na Dini wanazoziamini.
Kwa hiyo hawawezi kukuagiza mambo yaliyonje ya sheria za Dini au za Nchi.

Kumbuka mpaka iitwe Dini ndani ya nchi yetu lazima iwe imesajiliwa kisheria.
Sasa nafikiri umeelewa ni Kwa nini hawatakuambia mambo ya uhalifu.

Ninachokiona kwako ni unajifunza kujenga hoja. Na upo hatua za awali kabisa.
Hivyo jitahidi utumie akili na Logic katika kujenga hoja zako
 
Swala sio shurti ila kwa kuwa upo kwenye mamlaka yake lazima utii ila ukiwa nje ya kwakwe uko free kufanya unavyojisikiw yeye anaweza kukushauri tu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Unasema sio shurti halafu unasema tema Lazima nitii...hiyo si ndo maana ya shurti?

Wewe kwa imani yako unaamini katika kulazimishana dini?
 
Masharti mengine yote sawa. ila hili naona linahusiana na imani. Sasa mtu umlazimishe kuamini kitu fulani ni haki?
Yesu alishikisha watu mapanga akawalazimisha kuamini dini yake?

Yesu alikuwa na nyumba?
Au je Yesu alikuwa ana familia au watoto kama wewe hapo kwenu?
Tumia Logic unapotoa hoja zako.

Sheria inasema; Waheshimu Baba na Mama yako.
Hiyo ni SHERIA na amri.
Ukishakuwa upo nyumbani lazima amri hiyo uitekeleze iwe Kwa hiyari yako au Kwa nguvu.
 

Kwa ushauri, take it slow. Wengi wa wazazi wetu wamekua wakiamini dini kwa asilimia mia. Kumtoa mia (kuamini dini bila kuhoji) mpaka sifuri (atheism) ni kumuonea. Ni ngumu mno. So we cheza naye tu 50/50 hapo afu mpe muda wa kuadjust. Itafika kipindi atakuewa tu.
Mimi nimeamua play low maana bibi yangu akijua siendi church kwa sababu nimeona hizo fiction zimenichosha, nahisi atafariki kwa kihoro ndani ya mwaka tu na nisingependa kumpoteza kizembe hivyo so I play around tu. Fortunately nipo kwangu, yupo kwake.
Cheers!
 
Unaishi chini ya paa lake, ama fuata mwongozo wake au kajitegemee hatokusumbua.
Yeye ukiishi chini yake anaona ni wajibu wake kukuongoza
Tunaishi chini ya paa la serikali inayotuongoza...Je ni haki serikali kutulazimisa wananchi wote kuwa waislam?

Tunaishi kwenye dunia ya Mungu, Je Mungu anatulazimisha kumuamini na kwenda kanisani?
 
Unasema sio shurti halafu unasema tema Lazima nitii...hiyo si ndo maana ya shurti?

Wewe kwa imani yako unaamini katika kulazimishana dini?

Tofautisha mamlaka au tawala na Imani.

Mzazi anachokifanya ni kutumia utawala na mamlaka yake kuhakikisha sheria alizoziweka hapo nyumbani ikiwa ni pamoja na members wote wa familia kwenda kanisani wanafuata amri hiyo.
Suala la kuwa unaamini au hauamini hiyo sio juu yake. Hiyo ni juu yako.
Yeye anachotaka ni kutii matakwa yake. Wala mambo ya Imani yako hayamhusu.
 
Kuna kuzaa na kutoa maradhi mwilini (alisikika mlevi mmoja akisema)
Yani mpaka umefikia hatua ya kusema kuwa mwanao akiacha dini sio mwanao bali ni maradhi.

Hii inadhihirisha jinsi dini yako ilivyokula nafasi kubwa kwenye ubongo wako.

Tena hiyo ilikuwa nafasi ya muhimu kabisa ambayo ungeitumia kufikiria mambo ya maana, ila wewe umeijaza dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…