Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Tunaishi chini ya paa la serikali inayotuongoza...Je ni haki serikali kutulazimisa wananchi wote kuwa waislam?

Tunaishi kwenye dunia ya Mungu, Je Mungu anatulazimisha kumhauamini na kwenda kanisani?

Serikali haina Dini.
Ndio maana hiyo degree yako inatia Shaka Sana.
Unashindwa kufanya uhusisho wa hoja zako.

Secular state haiwezi kukupangia mambo ya Dini kwani yenyewe haina Dini.
Lakini Non-secular state kama Iran au Saudia Arabia au Qatar wao watakuambia na kukulazimisha ufuate sheria za Dini yao
 
Tunaishi chini ya paa la serikali inayotuongoza...Je ni haki serikali kutulazimisa wananchi wote kuwa waislam?

Tunaishi kwenye dunia ya Mungu, Je Mungu anatulazimisha kumuamini na kwenda kanisani?
Unaishi chini ya paa la mzazi wako, kama hutaki si unahama tu mkuu. Ukiwa chini ya mzazi utafuata kanuni zake ukiona waweza jitegemea basi hama.
Mimi nlikuwa naenda kansani nikiwa kwa wazazi now nina miaka sijui mingapi sijakanyaga
 
Acha kubishana na akili fupi , huwezi bishana na wapumbavu waliokuwa brainwashed ,ni ngumu .Utamaliza nguvu zako bure . Let them believe the garbage that they want to .
 
Kadigrii kako ndio kanakufanya ujione exceptional,special,much know.
Sasa mama yako unamuona yuko brainwashed.
Enyi watoto watiini wazazi wenu, mpate kuishi siku nyingi.
Fuata mafundisho mema ya wazazi wako na yatakusaidia kwa vizazi vyako.
Au labda wewe watoto wako utawafundisha nini?!
 
Kwani umekariri ndoa ni kanisa ni na msikitini tu ? , Au hujawai sikia ndoa za kiserikali ? .
Na kwani ni lazima wafunge ndoa ? ,By the way hakuna hata ndoa sikuhizi viini macho tu .Sikuhizi kuna ndoa au disco vumbi tu .na vituko tu .
Ni napenda watu wenye free mind ,watu wenye uwezo wa kukaa chini na kutafakari mambo na kuquestion paradigms ,sio majitu yanaishi kama misukule ,tabia ya kukariri mambo .
By the way mimi mwenyewe ni nonconformist ,I'm against so many pre established society norms which to me seems to be garbage ,non logical and tyrannical .I'm a pro free mind a hardcore nonconformist
Unategemea kufunga ndoa ya aina gani? usije ukaanza kumsumbua mama akakuombee kwa viongozi wa kanisa
 
Huyo brainwashed ndiye kamzaa na kumpa hiyo degree , sasa huyu malezi ya mwanaye yatakuwaje, kama hayatakuwa ma'mpotompoto.
 
Mbona umeni- quote Mimi?
 
Wazazi zaeni watoto mpunguze chango tumboni. Hizi ni fibroids kabisa. Hutaki kapange kwako eboooo
 
Hiyo ni 'imani' yako.
Yani ulivyosema hivyo ni kama vile wanaoenda kanisani hawatendi dhambi vile.

Let me tell you, mimi siendi kanisani lakini kwa maisha ninayoishi naweza kuwa wa kwanza kwenda mbinguni...(Kama ipo)
Wewe binti ni Msagaji na hiyo dhambi inakusumbua na imekuathiri Samahani kusema hivyo ila wewe ni Msagaji
 
Hongera sana mdogo wangu kama umesoma vitabu vya dini tofauti japo, nilikushauri tu
Labda nikuulize;
1. una amini kuwa Mungu yupo?
2. una amini kuwa ipo siku ya mwisho/siku ya hukumu?

Kama una amini, ni hatua nzuri na kama huamini, ni kwa nini?
Mimi nilikaa miaka saba bila kusali huku nikimtafuta Mungu kwenye vitabu (Biblia, Quran nk) na pia nikihudhuria Makongamano mbali mbali ya dini zote hivyo I can feel your concern.
Mwishowe nilijiridhisha niikae upande gani (kwa matakwa yangu mwenyewe)

Kwangu ilikuwa rahisi kwa kuwa nilikuwa najitegemea
 
Umesoma vitabu gani? Vitaje nataka nisome.

Unaishi na mama pekee au huko nyumbani yupo na baba? Naomba nifaham ili nitoe ushauri.
Niko na mzee, ila mzee hana time na haya mambo,...mama ndio anashupalia.

Vitabu ni vingi sana, kwasababu nilipokuwa form 2 nilikuwa na passion sana na dini. Yani ile tunaenda prepo wenzangu wanasoma physics mimi nilikuwa nasoma dini kila siku, so asilimia 80+ ya prepo zangu from form 2 to form 5 nilikuwa nasoma dini tu.
Vichache ni kama
Old & New testament
Heaven is for real-Todd turpo
The case for christ-Lee strobel
The attributes of God-Arthur Pink
Systematic theology-Wayne Grudem
The desire of Ages, The great controversy-Elen G. white
Catechism of the catholic church-
Roman catholic Encyclopedia karibia zote nilizisoma maana zilikuwa library shuleni
Here I stand-Maisha ya Martin Luther
Faragha ya kiroho, ukuaji wa kiroho-somebody Meinard Mtitu
Za wachungaji wa kibongo ndio usiseme
Vya kina mwakasege, Deo Njeni, na wengine wengi ambao hata sasa sivikumbuki majina

Vile vya ushuhuda kama nililala nikaamka usiku Yesu akanichukua akanipeleka kuzimu na mbinguni, nilishasoma vingi mno.
 
Post za jamii forums za wale Wasioamini uwepo wa Mungu zinakupotosha.
Nyie ndio mapaster na masheikh ushuzi mnaopotosha watu kwenda kuwaibia sadaka tu na kuwafanya misukule yenu kuendelea kuneemesha matumbo yenu huko kwenye makanisa na misukule , unafiki tu .Dini ni unafiki na takataka .
We angalia mtu mweusi alivyodumazwa na dini uchwara , na akili imekuwa kama makamasi ,dini ni minyororo ya kiakili ,na ni bora minyororo ya mkoloni iliyokuwa inafunga miguu na mikono kuliko hii minyororo ya kuabudu mapicha ya machoko kama Cesar Borgia ,masanamu ,mavitabu ya uongo , matakataka ,Total rubbish .
Dini ni certified superstition ,Hamna tofauti ya mtu anayependa kwa waganga wa kienyeji au mkishirikina na mtu anayeamini ma upuuz ya dini hayo, dini hizi ni michongo ya watu kuendelea kuwatawala watu wengine na kujinufaisha kiuchumi
 
Hahaha let me laugh. Im sorry lakini nilishindwa kujizuia.

Tulikuwa tunaongelea sheria (in general) za kufuata ukiwa chini ya wazazi.Ukasema ni lazima ufate sheria zote za wazazi ukiwa chini yao hata wakikuambia ukasali kwa mashetani, na ndio nikatoa mfano hapo wa sheria, wazazi wakilazimisha mtoto ukafanyiwe FGM na wao wanaamini kabisa kiutamaduni wao inapaswa ufanyiwe.
je ni haki?? Hauna haki ya kukataa??ni haki kusema huamini katika FGM kama wao??
Again hapa swala ni imani.
Iwe imani ya kidini au kiutamaduni, usichengeshe magoli.
 
Kula chakula cha mama yako huoni kama unalazimishwa, au kuingilia uhuru wako...

Kupelekwa shule na kulipiwa ada hukuona kama unalazimishwa na kuingiliwa uhuru wako...

Kununuliwa nguo za kusitiri uchi wako hukuona kama unalazimishwa kuvaa nguo na kuingiliwa uhuru wako...

Kulala kwenye kitanda na godoro usilochangia chochote huoni kama unalazimishwa na kuingiliwa uhuru wako...

Lakini suala la kiroho pekee yake ndio limekuwa nongwa kwako...
 
Huna imani ila imani ya kula chakula Cha bure unayo 😁 Lana sumaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…