Hii iliwahi kunikuta mie, wakati nipo Advance, wazazi walikua wananipigia kelele sana kisa kutoenda kanisani, na kuacha kabisa kufuata misingi ya dini,
Mwanzoni nilikua nawasikiliza ila kanisani siendi, ikafika hatua wazazi wakawaita watu wazima wanikalishe chini huenda nna tatizo, wale watu walio tumwa niliwapa vipande vyao hadi wakasandaa, wakaenda kutoa majibu kwa wazazi, nashangaa wazazi wakaanza kuninunia na kunisusa fulaan hivi, sikuwa najari hata.
Baadae wakanipeleka kwa katekista azungumze na mie, yulee katekistaa alianzaa kunisema na kuhubiri anayoyajua, nkawa namsikiliza tyuuh, mara akaanza oooh sijui motoni mara jehanamu. Nlichoka kusikiliza uongo wake, nkampa swali
"hayo mambo ya motoni na jehanamu sijui akhera na mbinguni wee uthibitisho unao? Uliwahi kwenda kushuhudia? Ni marehemu gani aliyekufa na kuzikwa akarudi tena duniani kusema kuwa huko kuna mbingu na jehanamu? Sasa km yupo nikutanishe nizungumze nae, km hayupoo naomba uniache sina mda wa kusikiliza hizo ngonjera zako hapa, na ukawaambie wale waliokutuma kuwa kanisani siendi kamweee na sitaki nikiwepo wazungumzie masuala ya dini iwe mwanzo na mwisho"
Yule katekistaaa akapekeka ujumbe kwa wazazi, siku ya pili baba ananambia kuna kikao cha familia, nkasema sawa. Jion yake tukakaa sebulen, mara mama anaanza kulia "mwanangu umekumbwa na nn shetan gan kakushika hvyo, pepo chafu hilo likutoke" nkaona huyu ananiletea uchuro, nkawachana ukweli na nlisema msimamo wangu ni huu na haubadiliki.
"Kuanzia leo nitakapokaa au kuwepo mie naomba masuala ya dini yasiwepo na yakiwepo nisihusishwee, sikuzaliwa ili nije kuridhisha watu, nilizaliwa ili kufurahia na kuishi maisha ya hap duniani. Huko kanisani siendi na sitakwenda kwa matakwa ya mtu yeyote ila maamuzi yangu binafsi, sina pepo chafu, shetani wala ndugu zake, ila mie mwenyewe sitaki na sipendi kwenda kanisani. Siwezi kuishi kwa kuwaridhisha nyie, kingine ambacho hamkijui wazazi mie mwanenu niko real sana, huwa sina sababu ya kufake kitu, siwezi kuinyima haki nafsi yangu kisa nyie hapanaa siweziiii.ntafanya yale ambayo natakiwa kufanya kwenu km wazazi ila masuala yangu binafsi uzazi na utoto nauweka pembeni nasimama mie km mie. Nimemalizaaaaa.
Tangu siku ile had leo sisikii habari zao za dini wala nn, na tunaishi vizuri tyuuh, nakusihi hebu simamia msimamo wako acha kupelekeshwa, mzazi hawezi kukuingilia ktk masuala yako ya imani. Be you!!!
.............