Mzazi kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu?

Asante kwa kuwasilisha mawazo ya wengi
 

Inategemea mtoto anataka nini, kama anataka vitu ambavyo ni halali kwa umri wake na viko ndani ya uwezo wako si mbaya kumpatia. Mfano mtoto wako wa miaka minne akililia chips, soda,juice, daftari, kitabu nk na ukaona vipo ndani ya uwezo wenu mpe tu haina shida, ila akililia kondomu kwa ajili ya kufanya pulizo mnyime au akililia K-Vant usimpe hata kama ipo ndani ya uwezo wako.
 
Kama unafaulu vizuri kila muhula sare mpya, begi mpya na pocket money ya kutosha. Sera ya mzee wangu hyo ilinifanya nipige shule nikiwa wa kwanza kila nilikopita. Hakuna chochote niliomba kilichokuwa ndani ya uwezo wa wazazi nikanyimwa. Naapply kwa wanangu pia.
 

Duuuu
 
Binafsi naangalia na mtoto.mwenyewe alivyo, kama anajitambua Hana shida unampa chochote anachotaka, wangu nilimpatia tena bila kuomba maana alikuwa anajitambua, akiwa form 3 mwaka huo huo wako aliambiwa na wenzie watoroke waende sehemu kule watapewa simu za Twanga pepeta (kuhongwa) alichowajibu ana simu nzuri kuliko hiyo pia kuliko hata walimu wake hivyo hakwenda, aliagiza atayekwenda mtembea mwisho wa mwezi aende na simu yake Ila itarudi siku hiyo hiyo ilikwenda akawaonyesha hakuna aliyemshawishi tena maana aliwaambia natimiziwa na mzazi wangu. Kwa kumnyima kutamharibu zaidi, mawazo yangu ni hayo
 
Ndio ni kumuharibu. Ni vema mtoto akajua kuna kupata na kukosa pia kupo.
 
nyie wazazi mnaodekeza watoto kupitiliza ..please tunaomba msiwe mnakufa mapema au kupata matatizo ..maanake huwa tunateseka mno na watoto wenu wasioambilika...
 
Kwa Dunia ya saivi ni heri kumpa kila akitakacho, maana usipompa wee atapewa na wenginee, lol

sasa mtoto wa miaka minne watafanya nini...nyie ndo huwa mnaspoil watoto..mwishowe mnakuja kuwapa shida hao hao watoto mambo yakiwaendea kombo...au unataka kuniambia kijana wa 16-18 kwako bado ni mtoto
 

acha ukuda na wewe..mshua alikuwa anakufundisha maisha..unadhani hiyo hela ambayo mather alikuwa anakupa alikuwa anapata wapi kama siyo kwa mshua wako
 
mimi nimeishi maisha ya msoto mno..lakini nashukuru wazazi kwa kila kitu..maanake wangenilea kizwazwa ningekuwa teja sasa hivi pengine
 
wanangu nitawapa malezi ya standard ...kamwe sito waspoil...maanake kesho yangu siijui...lazima wajifunze kuishi kwenye all weather.....please nadeclare mapema sitaki kufokewa na mtu yoyote...!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…