Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.

Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu.
 
Kipato 150,000 kwa mwezi

Idadi ya watoto ni 5

Kuna tofauti kubwa sana kwa huduma atakazopata mtoto mmoja kwa 150,000 kuliko watoto 5 kwa pesa hiyo hiyo.

Nani hajui hili?

Tunajua sana,

Tunajua vyema kabisa maisha ni magumu, kila mtu ameshatamka hili, lakini atabebeshana mimba na kuzaliana kwa wingi.

Elimu inatakiwa iwafikie watu kwa wingi, uzazi usio wa mpango ni janga na kichocheo kikubwa cha umaskini.
 
Mkuu kama huto jali naomba unichekie location kama hiyo aisee
 
Mimi sisemi vibaya wanaojiriwa na wala siwashushi heshima. Dunia ina watu wengi walioajiriwa. Hata mimi nimewahi kuajiriwa sehemu tofauti na industry tofauti.
Hoja yangu na yako ziko tofauti.
Kuhusu kuchafuka hii ni hoja nyepesi. Hata hapo panapochomwa chipsi ukienda mimi hunikuti.
Kama hoja ni kuwa mwenye mshahara wa laki 7 anaweza kumiliki vibanda 10 vya chipsi.....mimi nafeli wapi? Yeye ana vimiliki vipi na anafanya kazi from 8-5?
Ana free time ya kufanya ukaguzi?
Mind you, uhakika wa ajira na kipato ni serikalini tu. Private nyingi sana hazina uhakika wa kazi. Mikataba ya mwaka hadi mwakana hakuna fringe benefit ya maana. Una mkataba wa mwaka, unakopa wapi mil 20?
Kuna bank moja hapa Tanzania mfanyakazi hawezi kukopa pesa zaidi ya mkopo wa gari, salary advance ambayo maximum ni 4 times your salary au mortgage.
Sasa niambie mil 20 unakopaje hapo kwa mshahara wa laki 7?
Ngoja nikupe kidogo kuhusu mimi:-
1. Nina duka la furniture nimeshare na bro tumeweka partnership kisheria kabisa
2. Mimi binafsi nina stationery
3. Nina banda la chipsi
4. Nna share 50% kwenye kikampuni kidogo cha microfinance.
3. Hapa nafikiria kuanzisha PRINTING SERVICES business nifanye printing ya nguo, embroidery, vikombe, bahasha, vitabu, large format printing etc. Ntaisajili kama kampuni.
Lakini msingi wa vyote hivi ni ajira zangu zilizopita.
Kama unamwandaa mtoto mwandae aje apambane katika sekta zote. Unaonaje ukawa na biashara na ukamwajiri mwanao humo?
Tusifikirie tu status, kupendeza, assurance ya kipato, kazi soft soft.....n.k
Uncertainty zipo kila mahali.

Profits are sweeter than salaries.
 
Umenena baba mzazi baba
 
Wacha nicopy na kupaste hiki ulicho andika. Tafadhali naomba ruhusa yako ? Umeandika jambo la muhimu na la kweli kuhusu misingi ya maisha ya jamii zetu
 
Heshima yako mkuu Sean Paul

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Karibu mkuu, utawasaidia wengine.

Ni muda sasa sisi ngozi nyeusi tuachane na ubinafsi, umaskini wetu mkubwa unatokana na tabia ya ubinafsi.
Kweli kabisa kiwango cha ubinafsi tulicho nacho ni kikubwa sana. Si ajabu kama usemavyo mzazi kuificha familia idadi ya mali na biashara alizonazo

Tuna akili za kijinga sana mzazi anaona heri mtoto asome bila kuwa na future kuliko kumsaidia kuendesha biashara, shughuli au kilimo anacho fanya tuna mentality ya kipumbavu kua mtoto hatosoma atawaza tu mali za urithi na kuuana.

Bado tupo kwenye giza nene sana. Wenzetu hawa weupe hawaamini kuanza katika zero bali kuendeleza kile kidogo kiwe kikubwa Ila sisi tuna amini kila mtu anapaswa kuanza katika zero na kuacha hata kile kidogo kilichopo kisiendelezwe.

Mzazi anaona ni heri afe na mali zake pasipo familia kutambua kuliko kuacha mgawanyo wa majukumu akiwa hai.

Wewe mwenyewe shahidi tazama familia ya dewji Mohammed kapokea uongozi lini tazama na familia ya Mengi kafa mgogoro wa mali huo hapa ndio unaonesha sisi tuna shida kubwa na hatuandai mazingira bora kwa tunaowaacha hai duniani
 
Mkuu, aya yako ya mwisho umemaliza kila kitu. Ngozi nyeusi ipo tayari kutapanya mali zake nje ya ukoo bila kujali uendelezaji wa utajiri wake na akawaacha watoto wake wakihangaika. Hii inaendelea kupigilia msumari ubinafsi wa jamii ya watu wetu.

Na huu ujinga wa kuanzia zero tumeendelea kuuona kama sifa kumbe ni kutokujipanga toka zamani na tunaona kama ni sifa hivi.

Bila kubadilika na kuwaza kuwa na utajiri wa familia nzima na sio mtu mmoja mmoja, vijana wetu wataendelea kuhaha na bahasha mitaani tena wakiwa na ufaulu mzuri sana huku vijana wenzao walioenda kusoma kimkakati na wakianza kufurahia maisha mapema baada ya kumaliza shule.
 
Mwanangu upo sahihi et mwachie mungu mara sijui mungu anajua na apo huelew kitu yan Kwakwel I hate hope for real
 
UUjo
Ujinga mzigo kampuni ya kimataifa ya Steers Iko Hadi hapa Tanzania imeajiri Graduates wa vyuo vikuu kazi yake kubwa kuuza chips kuku na ins matawi kote duniani anauza chips kuku ni mmojawapo wa mabilionra duniani Kwa kuuza chips kuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…