lukesam
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 12,661
- 26,457
Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.
Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.
Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.
Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.
Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.
Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.
Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu.