Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Nipo kazini kama mtumishi kwa miaka mingi ila ukweli ni kuwa wajasiriamali na wafanyabiashara waliotuliza akili wanapiga hela na ni hao wanaotuweka mjini sisi maana nikikwama wananibeba ila nisitie aibu ndugu yao .

Ila natamani kusema biashara sio ya kila mtu aisee tukianza kuandika yaliyotukuta basi hata hizi ndoto zangu za kuacha pombe zitapotea tu .

Ila hongera sana kaka , Mungu akuzidishe zaidi na zaidi , ipo siku na mimi nitajipata huko nitoke huku tumwani .


Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
We jamaa una akili. Aisee una akili kubwa sana mwamba. Mwamba umeweza kutuonyesha ulimwengu wa pili sio kila siku watu wanatulisha matango pori ya kuajiriwa ni utumwa.... Wabongo wanapenda kukariri sana...
 
Mimi mwenyewe naumia sana Mkuu yan mpka unahisi kuna watu sijui wanamuomba Mungu yupi sababu na ww unasali tena unafunga unaomnba miujiza hyo hyo lakn wanapata wengine wanaojiweza na walio vizuri kiuchumi😔😔
 
Iwapo wauza chipsi na bodaboda wote wataamua leo hii kuacha hizo kazi, trust me tutatamani warejee. Kila mmoja ana umuhimu wake
Sawa na akina mpwayungu wanawaponda walimu, kila cku wanashawishiwa waachane na ualimu. Hebu imagine walimu wote wakiacha ualimu cjui watoto wetu watafundishwa na nani.
 
Alafu mbona Kuna mkanganyiko hapa kwenye hii mada!. Hatuwezi kupima ubora wa elimu kwa kigezo cha ajira. Hapa tutakuwa tunajadili 'Hamna'. Msingi wa elimu unataka Nini?. Tatizo la ajira linasababishwa na nn?.


Hatuwez kupima ubora wa elimu iliyopo kwa kigezo cha ajira.
 
Mzee wa kuchambia CV za wenzako[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wabongo bwana..sijui mnaona hizo kazi ndogo hazina hela ama vpi...mnadhan kukaa ofisin kuvaa vizuri ndo kuwa na hadhi inayoendana na elimu yako?...na ndo maana wasomi wengi wanaogopa kufanya vikazi hv vidogovidogo wanaogopa kudhalilika

Kuna dogo mmoja nipo nae pale mtaani..ni form 4 tu...kahangaika sana kujitafuta lkn mambo yakawa hayamwendei poa...

Siku moja nipo likizo akaja home kunisalimia..baada ya mazungumzo ya hapa na pale akaniambia changamoto zake za ujasiriamali( alikuwa anauza maji stand pugu b4 haijaamishwa)..sasa katika kupiga stori tu nikamwambia kwa nn asipige biashara ya chips(ilikuwa kama utani tu hata sikuitilia maanani)

Bhana wee..yule dogo wiki iliyofata akanifata akaniambia amepata eneo...kafungua kibanda..utani utani tu...

Wiki iliyopita j2 nilirudi likizo home..nikamfata pale kijiweni kwake(saa 4 huyo usiku)..akaniambia bro..mm hapa nafunga sa 10 asubuhi...nauza mpk nashngaa...kwa siku akitoa kila kitu anakunja si chini ya 90k..yani hiyo ni siku hajauza sana...kuna siku anapiga mpk 140k huko(hasa weekend)

Sasa kwa mwez hyo ni sh ngap?ww unaekaa ofisin unalipwa laki 7 kila siku kugombania daladala na yeye anaetoka kwake anaenda kazini kwa miguu dk 0 kashafika nan anaishi vizur?

Hzi biashara ndogondogo zinalipa..inshu ni location..ukiipatia location..utashangaa mwenyewe mpk unajiuliza siku zote ulikuwa WAPI
 
Yes tunakubaliana hapa, je kutoamini kwamba kuna nguvu ya Mungu katika maisha ya binadamu ni sawa?
Unauliza kama kutoamini kuwa kuna nguvu ya Mungu ni sawa? Au ni kuamini kitu kilicho kweli?

Tushaona imani unaweza kuamini hata uongo, kitu cha muhimu ni ukweli. Kwa nini unajikita kwenye imani bado?

Hayo ni maswali mawili tofauti.

Swali la kwanza, kuamini, au kutoamini kwamba kuna nguvu ya Mungu (hizi ni pande mbili za shilingi moja ile ile) sio tu ni sawa, hii ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Pia, hii ni haki ya binadamu iliyopitishwa katika Universal Declaration of Human Rights. Azimio hili limepitishwa na Umoja wa Mataifa December 10 1948.

KIla mtu ana haki ya kibinadamu ya kuamini au kutoamini nguvu za Mungu wake anavyotaka. Na katika kuongelea imani, maadam tunaongelea imani tu, hakuna imani iliyoishinda nyingine, maadam haiingilii uhuru wa wengine.

Kwa hivyo, ukitaka kuamini nguvu za Mungu wako ambaye ni mti wa mbuyu, una haki hiyo, na hilo ni sawa. Ukitaka kuamini Mungu wako ni Yesu Kristo Masiha, una haki hiyo, na hilo ni sawa. Ukitaka kuamini Mungu wako Allah, ni haki yako, na hilo ni sawa, ukitaka kuamini miungu yako isiyo na idadi, una haki hiyo, na hilo ni sawa, ukitaka kutoamini Mungu yeyote, kama mimi, ukasema hizi habari za Mungu zote ni ujinga mtupu, hiyo nayo ni haki yako ya kibinadamu, ni sawa tu.

Na mimi, licha ya kutoamini Mungu yeyote, tukiwa katika habari za imani, natetea haki za watu wote kuamini wanavyotaka, au kutoamini, ilimradi kuwe na mipaka mizuri ya kutoingiliana.

Hilo ni swali la kwanza, kutoamini katika nguvu ya Mungu katika maisha ya binadamu ni sawa?

Kwa kuwa tumekubaliana awali kwamba ukweli ni muhimu kuliko imani, kwa sababu ukweli upo mmoja tu, na imani unaweza kuamini hata uongo, tunapata swali la pili tofauti. Swali la kuangalia ukweli.

Je, ukiamini katika nguvu za Mungu unaamini katika ukweli? Huyo Mungu yupo kweli?.

Jibu ni, kwa kuanzia Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anayesemwa kuwa ni muumba wa vyote, Mungu huyu hayupo, anaweza kuoneshwa kimantiki kwamba huyu ni muhusika wa hadithi ya kutungwa na watu tu, na hivyo, kuamini katika nguvu zake ni sawa na kuangalia sinema ya James Bond 007 na kujirusha kutoka ghorofani ukiamini kwamba utaruka kwa nguvu za Ki James Bond kutika katika filamu ya Casino Royale.
 
Mkuu Kiranga
Samahani naomba unitag au link ya ule Uzi WA Buddhism.

Nataka nisome upya zile 8 folds of perfections
Mkuu na mimi nimeupoteza uzi kwa maana imekuwa siku nyingi.

Ila kama unataka vitabu vya Buddhism, vya bure, soft copies za pdf, mtandao huu una vitabu vingi sana.

 
Asante mkuu. Jipange tu, na mimi si kwamba najisifu. Maana kazi nilikua nimeajiriwa mpaka mwaka huu huu. Sasa hivi najiona niko huru mno, napata muda hadi wa kuabudu na kureflect maisha kwa upana sana. Sina tena kuwaza kuamka saa 11 asbh niwahi kazini, jioni unatoka unawaza foleni za barabarani hadi unafika home uko hoi.
Nilikua nasimamia sales team, kuna siku unasubiri hadi last person atoke sokoni ndio uondoke, unatoka kazini saa 2 usiku. Kesho imagine saa 1 na nusu upo tena.
Muda wa kuabudu hamna, Jumapili unaamka umechoka unadoji ibada. Jumuiya huonekani. Unaishi kikafiri sana.
Napata muda wa kusocialize mno, misiba mtaani, sherehe, jumuia na kila kitu. Najiona kama niko likizo vile kumbe ndio yameshakuwa maisha yangu.
 
Bora nifanye kazi serikalini nalipwa hio 700K kuliko kuwa muuza chips Kama na kuingiza hio 100K kwasiku kam huyo dogo.

I have dozens of reasons including Workdone muuza chips mpaka anatengeneza 100K kwasiku hio Workdone yake aloyofanya sio kazi bali ni Hell kazi kubwa Sana tena iliyokula muda wake wa siku mzima akitoka Hapo ni kulala, Workdone-Kulala, Kulala-Workdone.

Hio nguvukazi kubwa anayoifanya kwa kupata hio 100K per day Mimi kazi yangu ya kuajiriwa na kutoka saa 8 naiwekeza kwenye Modern Hustling zangu kwenye Technology in few years nameki pesa ndefu nikiwa kwenye viti yeye akiendelea kupokea Oder tu "nataka rojorojo" "nikaushir kavu"

Maisha ya sasa mtu mwenye malengo anahitaji Constant Cashflow kama ajira ya 700K, then anahitaji muda wa kutosha Weekday kunzia Saa 8 hadi usiku, Weekend full day free ana Push ndoto na passion zake za kumtajirisha.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huhitaji degree na mkopo wa HESLB kuuza CHIPS au kuendesha bodaboda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…