Mkuu kuna kitu hamjamuelewa mtoa mada. Kwa kifupi anamuongelea yule mhitimu alietoka chuo akiwa hana chcohote mfukoni. Hizi mambo za kuuza chipsi, bodaboda n.k zinahitaji pesa mtaji wa chipsi kwa makadirio ya chini kabisa inaweza kuwa almost milioni 1, pikipiki mpya inagonga sio chini ya milion 2.5. Mhitimu atatoa wapi iyo pesa? Nadharia nyingi za watu hapa wanamuelezea mtu ambae tayari ana ajira sasa anataka kupanua kuongeza vyanzo vya mapato hapo muhusika atajibana mshahara wake atafungua biashara halafu ataapply usomi wake lakini anaemuongelea mtoa mada ni mhitimu ambae hana chochote zaidi ya certificates tu. Uko juu nimeona
Sean Paul anaponda wasomi kwa kuchagua kazi yeye ana biashara ya chipsi ambayo anapiga hela zaidi ya msomi alieajiriwa at the same time anasema alishaajiriwa kama mtu wa sales akaacha akaingia kwenye kujiajiri unaona huyu alipata ajira kwanza akajichanga ndio akajiajiri hayupo katika kundi analoliongelea mleta mada.
Mkuu,
Nakubaliana nawe kuanzisha biashara ya mamilioni wakati mtu labda hata nauli tu ya kwenda mjini tatizo ni njozi
Lakini, kwa huyo unayemuita msomi aliyegraduate karibuni halafu hana ajira ni bora kabisa hata akaajiriwa kwenye kibanda cha kuuza chipsi kuliko kukaa bila kazi. Ilimradi anapiga mahesabu ya kujiongeza.
Yani kama mtu ana talent, ile kuwa na sehemu ya kwenda kufanya shughuli kila asubuhi tu inaweza kumletea connection nyingine kubwa huko huko akaunganisha mambo juu kwa juu. Kuliko kungojea kazi za ofisini ambazo hazipo.
Yani kama mimi nawafanyia interview watu wawili, wote wame graduate mwaka mmoja uliopita, wote wana kila kitu sawa, nitawauliza huu mwaka mmoja tangu u graduate umefanya nini?
Mmoja akiniambia kwamba nilikuwa najishikiza katika kibanda cha chipsi cha mtu nikajifunza mambo mawili matatu kuhusu business na customer care, halafu mwingine akaniambia nilikuwa natafuta kazi inayoendana na usomi wangu sikupata, mimi nitamuona huyo aliyejishikiza kwenye kibanda cha chipsi ana initiative, naweza kumuajiri huyo kirahisi kuliko aliyekuwa anasubiri kazi ya kufunga tai.
Aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Tanzania, Ali Mufuruki, aliwahi kuliongelea hili jambo, kwa kusema kuwa uki graduate maana yake si kwamba hutakiwi kufanya kazi fulani, alitolea mfano watu wanaoosha magari mjini wanatengeneza pesa nzuri tu. Sifikiri kwamba kazi ya kuosha magari inahitaji mtaji mkubwa sana. Ila watu hao ma graduate wanaona aibu, wakionwa na wenzao waliosoma nao itakuwaje? Si wataonekana wameshindwa maisha sasa? Hili ni tatizo kubwa, watu hawaishi maisha yao wanavyotaka, wanaishi kwa kuangalia macho ya watu wengine yatawaonaje.
Sasa, usomi wako unatakiwa kukufanya uweze kupiga mahesabu ya kusema kwamba, mimi sitaki kuosha magari au kukaanga chipsi, (yani hata nikikaanga chipsi au kuosha magari, iwe kisomi, kampuni kubwa). Lakini biashara ninayotaka kuifanya inahitaji mtaji wa shilingi milioni mbili na nusu, ambayo sina. Na ajira za ofisini hakuna. Ninachoweza kufanya hapa ni kukubali hii kazi ya kuosha magari, nikichange mpaka nipate huo mtaji wangu, halafu nikishapata mtaji nitajiongeza na kufanya biashara ninayoitaka.
Kimsingi, Ali Mufuruki alionya dhidi ya tabia ya hao wanaoitwa wasomi kudharau kazi za mikono na zile zinazoonekana hazihitaji kisomo, hata kama zinaweza kumpa mtu kipato cha kujikimu na hata kupata mtaji wa kuanzisha mambo mengine makubwa.
Na hii mentality ya "kazi ni kazi, vibaya wizi" watu wengi waliosoma Ulaya/Marekani/Asia wanaielewa, kwa sababu huko wenzetu wengi washafuta ujinga siku nyingi, mtu kupata degree si msomi, ni kitu cha kawaida tu, na unaweza kukuta mtu ana degree yake ya gardening anapiga kazi ya landscaping, huko kwetu tunashangaa mtu ana degree anashughulika na uchafu wa udongo tena? Ulaya/Marekani Watu wanafanya kazi na kujilipia chuo, kwa hiyo si ajabu mwanafunzi wa chuo kuwa anafanya kazi car wash.
Tena mtu anaona fahari kabisa kwenye kazi yake. Marehemu Le Mutuz alikuwa anaona fahari sana kuwa yeye aliweza kufanya kazi ya "Waste Management" ikampa kipato kizuri. Tena mtu anaweza hata kujivunia kazi kifalsafa kwamba kazi yake ina mchango mkubwa sana katika kuboresha mazingira, pengine kazi hiyo ikawa na umuhimu mkubwa zaidi ya banker anayefunga tai na kutoza watu riba inayosaidia natajiri kuzidi kutajirika, na masikini kuzidi juwa masikini.
Yani mtu anaweza kujenga hoja ya kisomi kabisa kwamba kazi ya kuzoa takataka na kuzifanyia recycling ina umuhimu jatika jamii kuliko kuwa afisa wa benki anayefunga tai na kukaa ofisini kwenye kiyoyozi.
"Wasomi" wetu wangapi wanachangamkia kazi za kuzoa taka? Zinadharaulika nankuonekana ni za watu duni kabisa. Wakati ukideal na electronic waste recycling tu kuna hela nyingi sana hapo.
Yani ukienda hata Nairobi tu utaona tofauti kubwa sana ya mentality kwenye mambo haya, huhitaji hata kwenda Ulaya au US.
Sisi kwetu bado tunalimbuka, mtu anayehitimu ki degree chake cha kwanza naye automatically anajiona msomi, wakati Jenerali Ulimwengu anatuambia kamaliza Form Ten tu. Sasa huyu naye analimbuka kuwa yeye ni msomi, hawezi jufanya kazi ya kuuza chipsi na kuosha magari.
Hata kama kazi hiyo anaweza kuifanya kwa mwaka tu na ikampa mtaji wa kufanya mambo yake mengine anayotaka.