Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Narudi kusema kuwa kulea ni kazi kubwa sana. Na mtoto anahitaji ukaribu mkubwa sana na wazazi. Ukiwa karibu naye kuna mambo unamfundisha asirudie makosa yako na kuna mawaidha atajifunza kutoka kwako. Ishu si kuajiriwa bali ni kujenga mtu anayejua kupambania Maisha yake. Mtu ambaye hata ukishaondoka duniani anaweza akasimamia majukumu yako.
Mi hapa kuna kitu sijaelewa mkuu! Ni kwamba unapinga uuzaji chipsi au bodaboda kwa wasomi,kwamba ni biashara isiyoweza kumtoa mtu? Mbona madalali wanasomesha watoto hadi huko chuo kikuu? Mtoto aliesoma kwa udalali wa baba yake kesho aje hapa aseme kwamba udalali si kazi?
Je,una uhakika gani kwamba anaemiliki bodaboda leo hawezi kumiliki gari lake binafsi la kubeba abiria?
Una uhakika gani kwamba anaeuza chipsi leo kesho hawezi kuwa na restaurant kubwa?
 
Sipingi kuuza chipsi na udalali ninachopinga ni kusomesha mtoto kwa hela nyingi akaishia kuuza chips au kuwa dalali. Bora hio hela ya ada ungempa afungue biashara. Ni upumbavu kumsomesha mtoto aje kuuuza chips au kuwa dalali.
 
Umeandika upuuzi,mi nimemaliza chuo nimerudi kitaa 2018,IQ changanya na degree yangu...aliyekomea la7 au F4 wengi net worth yangu imewazidi mbingu na aridhi.

Elimu yaan degree imenipa uwezo wa kutambua Baya na zuri Hususani mambo ya kuhalibu uchumi wangu.

Mfano,sibabaiki namatako yamjini yawadada, siteseki na pombe...kwangu nikiangalia Yanga na Madrid roho inalizikaa. Bina degree kunauwezekano wa 90%wa Mimi nisingejua nin haifai.

Hivyo Elimu ni silaha ya Maisha hutababaishwa na vitu au watu.
 
Elimu ni silaha. Kupambana ni kwako mwenyewe.
Tatizo vijana wanasubiri waitwe kwenye ajira.
 
Kaka ubora wa elimu utaupima kwa namna ambavyo huyo mhitimu anaweza kuitumia elimu yake kutatua changamoto za jamii yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira,
It's not a realistic perspective. Degree ngapi zinalenga kukutana na jamii moja kwa moja?. Bos/ muajiri sio jamii. Na matumizi ya elimu katika jamii huathiriwa pia na quality y kilichobaki kichwan na alivyoelewA darasani.

Hii kesi watu hawajaielewa vizuri. Kuna kitu Kiko hapo kinasumbua sana. Na hiki kama hakipatiw majibu hakuna kitu tutafanya. Elimu hii unaiona sio kitu na inayoendesha mifumo tunayoishi nayo. Inaonekana sio Bora kwa WALIOKOSA AJIRA PEKEE. Mbona waliopata ajira haijadiliwi?
 
"Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".
Wanapata elimu na kuelemika.
Hivi unadhani muuza nguo Karume mwenye degree atakuwa sawa na la saba?
Usomi upo kwenye reasoning, arguments, decisions, finding solutions, smartness during activities etc
 
Sipingi kuuza chipsi na udalali ninachopinga ni kusomesha mtoto kwa hela nyingi akaishia kuuza chips au kuwa dalali. Bora hio hela ya ada ungempa afungue biashara. Ni upumbavu kumsomesha mtoto aje kuuuza chips au kuwa dalali.
Aise! Bado hapa napingana na wewe kwa sababu kuu mbili:
-Kosa kubwa wanalofanya watu ni kusoma ukiamini kwamba lazima uajiliwe. Wakati ilikuwa bora usome ukijua na wewe unaendda kuajiri wengine.

-Kuuza chipsi au kuendesha bodaboda ni kazi kama kazi nyingine. Zisingekuwa na mshiko, hao wasomi wasingezifanya.

Ukiongea na watu walioajiliwa, nani ana furaha? Labda mpiga dili au yule anayepewa gari bure,mafuta bure, na marupurupu mengineyo. Sasa,nafasi ni 5. Wanaoiombea ni 1000. Mfano tu nimetoa. 995 wataenda wapi?

Wazazi wana kosa gani?
Hivi mfano,nchini kuna wachina na wahindi wangapi? Wanaomiliki biashara zinazoonekana za kawaida? Kwao, hizo fursa hazipo. Lakini namna ya kuzitumia zinapopatikana, wanajua.
Kama wanakuja na kuzifanya hapa,na wateja wanapata, si kwamba wenyeji hawazionibau hawazitumii?

Mzazi anakupa alicho nacho.
Kama ilivyo kwa taifa. Linakudai ila wewe hulidai chochote.
Hapa labda ungeanzisha thread ya kujuzana fursa zilizopo, kujadili namna ya kuzitumia, kabla wageni hawajapewa kipaumbele, wasomi wananufaikaje,wasiosoma wenyewe itakuwaje!
Hata mwenye kibanda cha kuuza miziki msomi anatunza familia na badae anafikia malengo yake.
Si wote sawa, ila kumbuka,kuna na wengine wanafanya hizo kazi ila nyuma ya pazia kuna mengi.
Bao wazazi unaosema,wakati mwingine wanauza mashamba na mifugo yao ili wakasomeshe. Je wahusika umewauliza kwa nini wanatesa wazazi wao labda?

Maana swala la chips na bodaboda wanalijua wahitimu.
Katika utafiti ulioufanya,uligundua tatizo ni nini? Na unashaulije!
 
Nilidhani mtu unasoma ili uelewe..., Kazi ni ili upate ujira wa kuweza kuishi...

Nadhani mindset zenu / zako zikifahamu hilo basi stress zitapungua kitaa...; hayo mambo ya kuwa Bodaboda ni Service sababu usafiri ni mbovu (kuhusu chips hio ni huduma) Tatizo labda ungesema shughuli nyingi hazina ujira wa kutosha...., By the way nikuulize kwanini unaishi...

Nilisema huku wazazi wajichange kuwasaidia watoto wao...
 
Kusoma kusiweke mipaka,kuwe labda sababu ya kujipanua kimawazo.

Sijui kwa nini sijaona watu wakipiga deals hasa za nje ya nchi.
Au pengine iwe ni jambo waliotangulia wanafanya kisirisiri. Matunda na mboga mboga ni vitu vinavyolipa sana kwa wanaosafilisha kwenda ugaibuni.
Changamoto kubwa inakuwa mtaji kwa wengine, uelewa na soko lenyewe.
Cha kujiuliza ni kwamba kwa nini waafrika hatuigi wenzetu waliofanikiwa!?
Kuna watu wamesoma,wakaajiliwa,badae wakaona hawana wanachokipata wakaamua kukiajili. Hawa ukiongea nao, ukisema umeajikiwa watakudhalau sana.
Kwa sababu kwenye ajira,kuna mengi unayoyakosa. Jiulize kuamka saa kumi na moja unawaza kwenda kazini. Hata kama nyumbani kuna mambo hayajakaa sawa(kwa wenye familia),unachojali ni boss asikutangulie. Chai umeacha nyumbani wanakaribia kuandaa,lakini gharama zake zitatoka kwenye mshahara. Na hiyo pesa unayotumia wewe mmoja, ingesaidia pakubwa ungekuwa na familia.
Jioni unarudi umechoka,unaanza kuulizwa ripoti na kufokewa.

Hapa huna hata mda wa kukutana na watu tofauti na kuanzisha connection mpya.
Kwa waliobahatika kujiajili,wawe mashahidi kwa wenzao. Kwa walioajiliwa,na wenyewe wawaze namna ya kujiajili.
Sasa,unakuta labda mtu yupo Mwanza,au Kigoma. Ajira ni Dar. Nauli na mambo mengine hata kama angekuwa na ndugu,kuipata hiyo pesa kwenye si kazi ndogo. Je,kwa yule asie na mwenyeji?
 
Aise! Bado hapa napingana na wewe kwa sababu kuu mbili:
-Kosa kubwa wanalofanya watu ni kusoma ukiamini kwamba lazima uajiliwe. Wakati ilikuwa bora usome ukijua na wewe unaendda kuajiri wengine.

-Kuuza chipsi au kuendesha bodaboda ni kazi kama kazi nyingine. Zisingekuwa na mshiko, hao wasomi wasingezifanya.

Ukiongea na watu walioajiliwa, nani ana furaha? Labda mpiga dili au yule anayepewa gari bure,mafuta bure, na marupurupu mengineyo. Sasa,nafasi ni 5. Wanaoiombea ni 1000. Mfano tu nimetoa. 995 wataenda wapi?

Wazazi wana kosa gani?
Hivi mfano,nchini kuna wachina na wahindi wangapi? Wanaomiliki biashara zinazoonekana za kawaida? Kwao, hizo fursa hazipo. Lakini namna ya kuzitumia zinapopatikana, wanajua.
Kama wanakuja na kuzifanya hapa,na wateja wanapata, si kwamba wenyeji hawazionibau hawazitumii?

Mzazi anakupa alicho nacho.
Kama ilivyo kwa taifa. Linakudai ila wewe hulidai chochote.
Hapa labda ungeanzisha thread ya kujuzana fursa zilizopo, kujadili namna ya kuzitumia, kabla wageni hawajapewa kipaumbele, wasomi wananufaikaje,wasiosoma wenyewe itakuwaje!
Hata mwenye kibanda cha kuuza miziki msomi anatunza familia na badae anafikia malengo yake.
Si wote sawa, ila kumbuka,kuna na wengine wanafanya hizo kazi ila nyuma ya pazia kuna mengi.
Bao wazazi unaosema,wakati mwingine wanauza mashamba na mifugo yao ili wakasomeshe. Je wahusika umewauliza kwa nini wanatesa wazazi wao labda?

Maana swala la chips na bodaboda wanalijua wahitimu.
Katika utafiti ulioufanya,uligundua tatizo ni nini? Na unashaulije!
Wewe ndo haujaelewa wahindi na wachina wanakaa karibu na watoto wao ndo maana hawapotezi hela nyingi kwenye shule. Mhindi akiona mtoto yupo vizuri kwenye sekta fulani anampa mtaji mapema. Ninachopinga ni kumpeleka mtoto shule ya gharama halafu mzazi anaweka miguu juu akijua kashamaliza. Halafu naomba uje na ushahidi hapa kuna Mhindi au Mchina anauza chips au bodaboda ? Mzazi ambae ana uwezo wa kulipa ada ya shule binafsi akikaa karibu na watoto wake kamwe hawawezi kuishia kuuza chips au kuwa boda boda. Tusimamie majukumu yetu kama wazazi tuwe serious.
 
Mkuu,

Nakubaliana nawe kuanzisha biashara ya mamilioni wakati mtu labda hata nauli tu ya kwenda mjini tatizo ni njozi

Lakini, kwa huyo unayemuita msomi aliyegraduate karibuni halafu hana ajira ni bora kabisa hata akaajiriwa kwenye kibanda cha kuuza chipsi kuliko kukaa bila kazi. Ilimradi anapiga mahesabu ya kujiongeza.

Yani kama mtu ana talent, ile kuwa na sehemu ya kwenda kufanya shughuli kila asubuhi tu inaweza kumletea connection nyingine kubwa huko huko akaunganisha mambo juu kwa juu. Kuliko kungojea kazi za ofisini ambazo hazipo.

Yani kama mimi nawafanyia interview watu wawili, wote wame graduate mwaka mmoja uliopita, wote wana kila kitu sawa, nitawauliza huu mwaka mmoja tangu u graduate umefanya nini?

Mmoja akiniambia kwamba nilikuwa najishikiza katika kibanda cha chipsi cha mtu nikajifunza mambo mawili matatu kuhusu business na customer care, halafu mwingine akaniambia nilikuwa natafuta kazi inayoendana na usomi wangu sikupata, mimi nitamuona huyo aliyejishikiza kwenye kibanda cha chipsi ana initiative, naweza kumuajiri huyo kirahisi kuliko aliyekuwa anasubiri kazi ya kufunga tai.

Aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Tanzania, Ali Mufuruki, aliwahi kuliongelea hili jambo, kwa kusema kuwa uki graduate maana yake si kwamba hutakiwi kufanya kazi fulani, alitolea mfano watu wanaoosha magari mjini wanatengeneza pesa nzuri tu. Sifikiri kwamba kazi ya kuosha magari inahitaji mtaji mkubwa sana. Ila watu hao ma graduate wanaona aibu, wakionwa na wenzao waliosoma nao itakuwaje? Si wataonekana wameshindwa maisha sasa? Hili ni tatizo kubwa, watu hawaishi maisha yao wanavyotaka, wanaishi kwa kuangalia macho ya watu wengine yatawaonaje.

Sasa, usomi wako unatakiwa kukufanya uweze kupiga mahesabu ya kusema kwamba, mimi sitaki kuosha magari au kukaanga chipsi, (yani hata nikikaanga chipsi au kuosha magari, iwe kisomi, kampuni kubwa). Lakini biashara ninayotaka kuifanya inahitaji mtaji wa shilingi milioni mbili na nusu, ambayo sina. Na ajira za ofisini hakuna. Ninachoweza kufanya hapa ni kukubali hii kazi ya kuosha magari, nikichange mpaka nipate huo mtaji wangu, halafu nikishapata mtaji nitajiongeza na kufanya biashara ninayoitaka.

Kimsingi, Ali Mufuruki alionya dhidi ya tabia ya hao wanaoitwa wasomi kudharau kazi za mikono na zile zinazoonekana hazihitaji kisomo, hata kama zinaweza kumpa mtu kipato cha kujikimu na hata kupata mtaji wa kuanzisha mambo mengine makubwa.

Na hii mentality ya "kazi ni kazi, vibaya wizi" watu wengi waliosoma Ulaya/Marekani/Asia wanaielewa, kwa sababu huko wenzetu wengi washafuta ujinga siku nyingi, mtu kupata degree si msomi, ni kitu cha kawaida tu, na unaweza kukuta mtu ana degree yake ya gardening anapiga kazi ya landscaping, huko kwetu tunashangaa mtu ana degree anashughulika na uchafu wa udongo tena? Ulaya/Marekani Watu wanafanya kazi na kujilipia chuo, kwa hiyo si ajabu mwanafunzi wa chuo kuwa anafanya kazi car wash.

Tena mtu anaona fahari kabisa kwenye kazi yake. Marehemu Le Mutuz alikuwa anaona fahari sana kuwa yeye aliweza kufanya kazi ya "Waste Management" ikampa kipato kizuri. Tena mtu anaweza hata kujivunia kazi kifalsafa kwamba kazi yake ina mchango mkubwa sana katika kuboresha mazingira, pengine kazi hiyo ikawa na umuhimu mkubwa zaidi ya banker anayefunga tai na kutoza watu riba inayosaidia natajiri kuzidi kutajirika, na masikini kuzidi juwa masikini.

Yani mtu anaweza kujenga hoja ya kisomi kabisa kwamba kazi ya kuzoa takataka na kuzifanyia recycling ina umuhimu jatika jamii kuliko kuwa afisa wa benki anayefunga tai na kukaa ofisini kwenye kiyoyozi.

"Wasomi" wetu wangapi wanachangamkia kazi za kuzoa taka? Zinadharaulika nankuonekana ni za watu duni kabisa. Wakati ukideal na electronic waste recycling tu kuna hela nyingi sana hapo.

Yani ukienda hata Nairobi tu utaona tofauti kubwa sana ya mentality kwenye mambo haya, huhitaji hata kwenda Ulaya au US.

Sisi kwetu bado tunalimbuka, mtu anayehitimu ki degree chake cha kwanza naye automatically anajiona msomi, wakati Jenerali Ulimwengu anatuambia kamaliza Form Ten tu. Sasa huyu naye analimbuka kuwa yeye ni msomi, hawezi jufanya kazi ya kuuza chipsi na kuosha magari.

Hata kama kazi hiyo anaweza kuifanya kwa mwaka tu na ikampa mtaji wa kufanya mambo yake mengine anayotaka.
Nakuelewa vizuri kabisa mkuu lakini bado tunarudi pale, unaongea nadharia ambazo ukiziweka kwenye practical kutoboa its very rare if not impossible.

Unakosea sana kulinganisha ulaya na Tanzania, ulaya ukikutwa mtaani bila kazi ya kufanya ilo ni kosa la uzululaji na kitachofanyika hapo unapewa kazi ya kufanya tena yenye malipo kima ambacho utaweza ku-afford kupata mahitaji muhimu, hapa Tanzania kosa la uzululaji utaishia kufanyiwa harrasments na polisi pamoja na kuwekwa lockup tena kukuachia wanaweza wakataka rushwa.

Huo mchongo wa kuchakata takataka uliutolea mfano si utahitaji kununua mtambo na cost zingine za uendeshaji mfano umeme? Jobless mwenye certificates tu kabatini anaweza ku-afford izo costs? Unarudi kule kule niliposema mtoa mada kawalenga wahitimu wasiokua na chochote na wewe unawalenga wenye kipato ila wanataka kuongeza vyanzo vya mapato. Ni rahisi kutengeneza milioni 10 ukiwa na milioni 2 kuliko kutengeneza elfu 50 ukiwa hauna chochote kabisa.

Sina uhakika kama ushawahi kufanya izo mishe unaziongelea hapa na kujua kibongo bongo uyo muuza chipsi au kibarua kiwandani analipwa shilingi ngapi na kufanya uchambuzi kuona kama iyo hela inamtosheleza mahitaji yake pamoja na kuweka akiba. Wauza chipsi, bodaboda, waosha magari n.k ni washkaji zetu tunaishi nao mtaani hali zao tunazijua izo mishe hazina maokoto kama ambavyo mnazikuza. Unachokipata kinaweza kisitosheleze hata mahitaji ya msingi achilia mbali kuweka akiba.

Ni ujinga kumsomesha afisa ugavi mpaka ngazi ya degree halafu unamtaka kuapply elimu yake kwenye ubodaboda, mtu ana degree ya human resource halafu unamwambia aitumie elimu yake kwenye kazi ya u-barmaid.! It makes no sense. Elimu yetu unamuandaa mtu kufanya kazi katika structural organization/institute sio izo mishe za mtaani ambazo zinaenda unformality,

Kkama tumeamua ku-establish uchumi wa wachuuzi na ajira zisizo rasmi basi tufunge vyuo vyetu kwa sababu hakuna maana tena ya kuzalisha wasomi. Unamsomesha mtu business management mpaka ngazi ya juu halafu aje mtaani kuuza maandazi! Hivi biashara ya maandazi inahitaji utaalamu gani wa kuuendea chuo kikuu? Mhitimu wa business management anatakiwa kusimamia project kubwa.

Hata ivyo izo mishe unazozichukulia poa na kuona zinapatikana kirahisi rahisi kuweza kuwa sehemu ya mtu kuanzia mfano car wash, saidia fundi, konda n.k kwa sasa zina ushindani na zinapatikana kwa kujuana. Nafikiri mkuu ulitoboa enzi za mwinyi au mkapa kipindi ambacho decent jobs zilikua nje nje sana hauna objectively experience ya sasa kwenye suala la ajira mtaani

Tukubali mfumo wetu ni mbovu, tuwape kazi wataalamu waje na njia ya kutunasua tulipokwama kwa kutupa short terms and long terms strategies sio huu ujinga wa kumpongeza mama ntilie mwenye masters. Mtu kusoma mpaka masters na kuishia kuwa mama ntilie wa mtaani maana yake kuna tatizo kubwa sana kwenye system uliyomuandaa kuwa ivyo.
 
Mimi silinganishi Ulaya/US na Tanzania. Mimi nakueleza nchi hizo zimepitia njia gani kufika hapo zilipo ili na sisi tufike hapo.

Kuhusu kazi zinazodharaulika, si lazima uanze kwa kununua mtambo wa kurecycle uchafu kwa mfano. Ni wazi huyu graduate ambaye hata nauli ya kwenda mjini inamsumbua hawezi kupata mtaji huo kirahisi.

Ninachoongelea mimi ni hii concept ya "to get a foot in the door". Kupata sehemu ya kuanzia. Unaweza kupewa kazi ndogo sana ukilinganisha na kisomo chako, ukaikubali, halafu watu wakagundua kipaji chako ni kikubwa, wakaona huyu mtu tunamu underutilize. Yani ile kupewa kazi ndogo inakuwa kama mtihani wa maisha tu umepewa, kwamba, likija zali dogo utaliweza? Mara nyingine watu wanataka mazali makubwa wakati mlango wa kufikia zali kubwa unakuwepo katika zali dogo, sasa hapo ukilikataa zali dogo kwa kusema mimi msomi sana hili zali dogo nalidharau, inawezekana ukawa umejikosesha connections za kutumia hilo zali dogo kuunganisha kwenda kwenye zali kubwa.

Unaongelea ujinga kumsomesha afisa ugavi mpaka kwenye degree halafu aka apply elimu yake kwenye kazi ya bodaboda, hapo ndipo Waafrika tunaposhindwa, hii mentality ndiyo inatufanya tuwe masikini.

Yani hatujui kwamba nia ya elimu ni kumuwezesha mtu kupambana na mazingira yake, hatujui kuwa kama kazi za afisa ugavi hazipo, basi afisa ugavi ataichukua ile kazi ya bodaboda iliyokaa ki local local, ataiangalia kisomi, atai analyze ki statistics, ataifanya iwe efficient zaidi, ataiwekea technology ya ku track pikipiki, ataiwekea app, atafanya mfumo wa malipo online, mara tu kashaleta kitu kipya kinapata investors. Anakuwa anafanya biashara ya bodaboda kisomi. Anakuwa na ofisi kubwa, anaajiri watu, mara tu kawa CEO. Elimu yake inaonekana imefanya kitu kikubwa.

Si ndiyo wanavyofanya watoto wa Kimarekani kila siku wanatuletea ma Uber sijui ma Lyft yanakuja ku conquer biashara dunia nzima. Mpaka mtu unashangaa, ayaaa weee, hivi kwa nini sisi hatukufikiria kitu hiki?

Ni kwa sababu tunadharau sana. Tunasema mimi? Mimi msomi nikafanye kazi ya bodaboda? Kumbe mtu ukiwa smart enough, karibu popote pale utakapotupwa unaweza kuona challenges za ku solve na kutengeneza big deals.

Sisi wengi hatuko innovative, hatutaki kujifunza, hatutaki kuwa humble, granted na mifumo yetu ya support, mikopo etc nayo ni mibovu, lakini siku hizi ukiwa na idea nzuri unaweza ku hook up hata na investors wa nje.

Tunadharau. Wasomi wengi sana wamekariri mambo, ukiwaleta kwenye mtaa kuwa innovative, kubadilika na mazingira yanavyobadilika, wanashindwa.

Mimi ndiyo maana hata kuwaita wasomi napata shida, msomi ni mtu anayeweza kubadilika na mazingira.

Unasema mission hazipatikani kirahisi, mimi nishasaidia watu hapa thousands of dollars, hapahapa JF. Wameleta ideas, nimeona what is two thousand dollars to me, hiyo hela natumia weekend bila hata kujua, huyu mtu nikimpa mtaji anaweza kutoboa maisha, nimesaidia.

Lakini, kuna nyuzi ngapi za ku pitch business ideas hapa JF?

Wasomi wa Bongo wengi wana dharau sana.

Mimi nilikaa na mshkaji tukatoa challenge ya kuandika some academic papers, kuwe na zawadi, mshkaji akatangaza USD 300 kama zawadi, akisisitiza nia si kutoa hela nyingi, nia ni kuanzisha mashindano yatakayowapa wanafunzi tuzo na kujenga CV, kuwapa kitu cha kuwatofautisha.

Licha ya msisitizo huo, mimi nikaona kuwa USD 300 bado ni ndogo kwa zawadi, nika double zawadi kwa kusema nitatoa USD 300 zaidi. Zawadi ikawa USD 600.

Nakwambia vijana waliliangalia angalia tu lile shindano, mpaka mwisho wakalipotezea.

Nikasema labda wako poa hawa.

So, hayo mambo ya kusaidia vimitaji vya milioni mbili tatu hivi, hata hapa tunaweza kufanya, even 10 million kama kuna kitu cha maana, tena mtu akiwa na idea nzuri watu wanaweza kufanya kama investment.

But, do we even get the ideas?
 
Nimekuelewa mkuu, katika support yako kwa vijana kama ulivyoongelea hapo juu, endapo nafasi ikitokea naomba uniangalie mkuu. Nina idea nyingi kichwani lakini nakosa tu wa kunishika mkono financialy.
 
Umeandika upuuzi,mi nimemaliza chuo nimerudi kitaa 2018,IQ changanya na degree yangu...aliyekomea la7 au F4 wengi net worth yangu imewazidi mbingu na aridhi.

Elimu yaan degree imenipa uwezo wa kutambua Baya na zuri Hususani mambo ya kuhalibu uchumi wangu.

Mfano,sibabaiki namatako yamjini yawadada, siteseki na pombe...kwangu nikiangalia Yanga na Madrid roho inalizikaa. Bina degree kunauwezekano wa 90%wa Mimi nisingejua nin haifai.

Hivyo Elimu ni silaha ya Maisha hutababaishwa na vitu au watu.
Kwa nini somo hili linakuwa gumu sana kueleweka?

Kwa nini watu hawaelewi kuwa, lengo la elimu si kukupatia ajira ili maisha yako yawe mazuri, lengo la elimu ni kukuwezesha kupambana na mazingira yako yoyote yale.

Yani hata ikitokea miti yote imeteleza, mwenye elimu na asiye na elimu wote wakafanya kazi moja ya chini kabisa ambayo imeonekana ya kudharaulika kabisa, mwenye elimu awe na uwezo wa kuongeza kitu kwenye ile kazi na kuifanya iwe ya ufanisi zaidi.

Au mwenye elimu aelewe mambo makubwa zaidi ya kiuchumi yaliyompita nguvu, asisononeke kwa kudhani amelogwa, ajue kwamba anahitaji kufanya nini kujikwamua.

Kwa nini watu wanafikiri lengo la elimu ni kupata ajira ya kisomi?
 
Akili matope km ingekua rahisi hivyo si wote wangekua hawahangaiki kwenye 10 ni 1 hivi unaona hilo gap na hio 1 nyuma kuna nguvu ya mtu fulani inampa support bila hivyo hafiki popote unanielewa sijui au bado mpaka upigwe kidole ndio uelewe?
We dogo una akili mgando, huamini kwenye hustles. Unaamini kwenye connections na huko kutiwa dole.

Pambana chalii, nilichogundua graduates wengi ni wavivu mno, hasa wale fresh from school.
Mpama mtaa uwachape ndo wanakubali kuhustle kitaa ila ile fresh kabisa hawezi zama kitaa nae atataka kazi za kiyoyozi.
 
Back
Top Bottom