Nakuelewa vizuri kabisa mkuu lakini bado tunarudi pale, unaongea nadharia ambazo ukiziweka kwenye practical kutoboa its very rare if not impossible.
Unakosea sana kulinganisha ulaya na Tanzania, ulaya ukikutwa mtaani bila kazi ya kufanya ilo ni kosa la uzululaji na kitachofanyika hapo unapewa kazi ya kufanya tena yenye malipo kima ambacho utaweza ku-afford kupata mahitaji muhimu, hapa Tanzania kosa la uzululaji utaishia kufanyiwa harrasments na polisi pamoja na kuwekwa lockup tena kukuachia wanaweza wakataka rushwa.
Huo mchongo wa kuchakata takataka uliutolea mfano si utahitaji kununua mtambo na cost zingine za uendeshaji mfano umeme? Jobless mwenye certificates tu kabatini anaweza ku-afford izo costs? Unarudi kule kule niliposema mtoa mada kawalenga wahitimu wasiokua na chochote na wewe unawalenga wenye kipato ila wanataka kuongeza vyanzo vya mapato. Ni rahisi kutengeneza milioni 10 ukiwa na milioni 2 kuliko kutengeneza elfu 50 ukiwa hauna chochote kabisa.
Sina uhakika kama ushawahi kufanya izo mishe unaziongelea hapa na kujua kibongo bongo uyo muuza chipsi au kibarua kiwandani analipwa shilingi ngapi na kufanya uchambuzi kuona kama iyo hela inamtosheleza mahitaji yake pamoja na kuweka akiba. Wauza chipsi, bodaboda, waosha magari n.k ni washkaji zetu tunaishi nao mtaani hali zao tunazijua izo mishe hazina maokoto kama ambavyo mnazikuza. Unachokipata kinaweza kisitosheleze hata mahitaji ya msingi achilia mbali kuweka akiba.
Ni ujinga kumsomesha afisa ugavi mpaka ngazi ya degree halafu unamtaka kuapply elimu yake kwenye ubodaboda, mtu ana degree ya human resource halafu unamwambia aitumie elimu yake kwenye kazi ya u-barmaid.! It makes no sense. Elimu yetu unamuandaa mtu kufanya kazi katika structural organization/institute sio izo mishe za mtaani ambazo zinaenda unformality,
Kkama tumeamua ku-establish uchumi wa wachuuzi na ajira zisizo rasmi basi tufunge vyuo vyetu kwa sababu hakuna maana tena ya kuzalisha wasomi. Unamsomesha mtu business management mpaka ngazi ya juu halafu aje mtaani kuuza maandazi! Hivi biashara ya maandazi inahitaji utaalamu gani wa kuuendea chuo kikuu? Mhitimu wa business management anatakiwa kusimamia project kubwa.
Hata ivyo izo mishe unazozichukulia poa na kuona zinapatikana kirahisi rahisi kuweza kuwa sehemu ya mtu kuanzia mfano car wash, saidia fundi, konda n.k kwa sasa zina ushindani na zinapatikana kwa kujuana. Nafikiri mkuu ulitoboa enzi za mwinyi au mkapa kipindi ambacho decent jobs zilikua nje nje sana hauna objectively experience ya sasa kwenye suala la ajira mtaani
Tukubali mfumo wetu ni mbovu, tuwape kazi wataalamu waje na njia ya kutunasua tulipokwama kwa kutupa short terms and long terms strategies sio huu ujinga wa kumpongeza mama ntilie mwenye masters. Mtu kusoma mpaka masters na kuishia kuwa mama ntilie wa mtaani maana yake kuna tatizo kubwa sana kwenye system uliyomuandaa kuwa ivyo.
Mkuu,
Mimi silinganishi Ulaya/US na Tanzania. Mimi nakueleza nchi hizo zimepitia njia gani kufika hapo zilipo ili na sisi tufike hapo.
Kuhusu kazi zinazodharaulika, si lazima uanze kwa kununua mtambo wa kurecycle uchafu kwa mfano. Ni wazi huyu graduate ambaye hata nauli ya kwenda mjini inamsumbua hawezi kupata mtaji huo kirahisi.
Ninachoongelea mimi ni hii concept ya "to get a foot in the door". Kupata sehemu ya kuanzia. Unaweza kupewa kazi ndogo sana ukilinganisha na kisomo chako, ukaikubali, halafu watu wakagundua kipaji chako ni kikubwa, wakaona huyu mtu tunamu underutilize. Yani ile kupewa kazi ndogo inakuwa kama mtihani wa maisha tu umepewa, kwamba, likija zali dogo utaliweza? Mara nyingine watu wanataka mazali makubwa wakati mlango wa kufikia zali kubwa unakuwepo katika zali dogo, sasa hapo ukilikataa zali dogo kwa kusema mimi msomi sana hili zali dogo nalidharau, inawezekana ukawa umejikosesha connections za kutumia hilo zali dogo kuunganisha kwenda kwenye zali kubwa.
Unaongelea ujinga kumsomesha afisa ugavi mpaka kwenye degree halafu aka apply elimu yake kwenye kazi ya bodaboda, hapo ndipo Waafrika tunaposhindwa, hii mentality ndiyo inatufanya tuwe masikini.
Yani hatujui kwamba nia ya elimu ni kumuwezesha mtu kupambana na mazingira yake, hatujui kuwa kama kazi za afisa ugavi hazipo, basi afisa ugavi ataichukua ile kazi ya bodaboda iliyokaa ki local local, ataiangalia kisomi, atai analyze ki statistics, ataifanya iwe efficient zaidi, ataiwekea technology ya ku track pikipiki, ataiwekea app, atafanya mfumo wa malipo online, mara tu kashaleta kitu kipya kinapata investors. Anakuwa anafanya biashara ya bodaboda kisomi. Anakuwa na ofisi kubwa, anaajiri watu, mara tu kawa CEO. Elimu yake inaonekana imefanya kitu kikubwa.
Si ndiyo wanavyofanya watoto wa Kimarekani kila siku wanatuletea ma Uber sijui ma Lyft yanakuja ku conquer biashara dunia nzima. Mpaka mtu unashangaa, ayaaa weee, hivi kwa nini sisi hatukufikiria kitu hiki?
Ni kwa sababu tunadharau sana. Tunasema mimi? Mimi msomi nikafanye kazi ya bodaboda? Kumbe mtu ukiwa smart enough, karibu popote pale utakapotupwa unaweza kuona challenges za ku solve na kutengeneza big deals.
Sisi wengi hatuko innovative, hatutaki kujifunza, hatutaki kuwa humble, granted na mifumo yetu ya support, mikopo etc nayo ni mibovu, lakini siku hizi ukiwa na idea nzuri unaweza ku hook up hata na investors wa nje.
Tunadharau. Wasomi wengi sana wamekariri mambo, ukiwaleta kwenye mtaa kuwa innovative, kubadilika na mazingira yanavyobadilika, wanashindwa.
Mimi ndiyo maana hata kuwaita wasomi napata shida, msomi ni mtu anayeweza kubadilika na mazingira.
Unasema mission hazipatikani kirahisi, mimi nishasaidia watu hapa thousands of dollars, hapahapa JF. Wameleta ideas, nimeona what is two thousand dollars to me, hiyo hela natumia weekend bila hata kujua, huyu mtu nikimpa mtaji anaweza kutoboa maisha, nimesaidia.
Lakini, kuna nyuzi ngapi za ku pitch business ideas hapa JF?
Wasomi wa Bongo wengi wana dharau sana.
Mimi nilikaa na mshkaji tukatoa challenge ya kuandika some academic papers, kuwe na zawadi, mshkaji akatangaza USD 300 kama zawadi, akisisitiza nia si kutoa hela nyingi, nia ni kuanzisha mashindano yatakayowapa wanafunzi tuzo na kujenga CV, kuwapa kitu cha kuwatofautisha.
Licha ya msisitizo huo, mimi nikaona kuwa USD 300 bado ni ndogo kwa zawadi, nika double zawadi kwa kusema nitatoa USD 300 zaidi. Zawadi ikawa USD 600.
Nakwambia vijana waliliangalia angalia tu lile shindano, mpaka mwisho wakalipotezea.
Nikasema labda wako poa hawa.
So, hayo mambo ya kusaidia vimitaji vya milioni mbili tatu hivi, hata hapa tunaweza kufanya, even 10 million kama kuna kitu cha maana, tena mtu akiwa na idea nzuri watu wanaweza kufanya kama investment.
But, do we even get the ideas?