Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu

Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu

Mipango haramu sometimes huusisha watu wengi ili itimie.
Kashapokeleshwa chake,mbele ya Rupia!!!Siyo bure.Huyu Mzee anaenda kupoteza Hadhi aliyojijengea kwa miaka lukuki.Sina uhakika huko CCM Mpya kuna Zimwi gani linalofanya hata tuliowaamini kuwa manguli wa siasa safi nao wanagwaya!
Watanzania tutambue habari iliyopo mbele ya Taifa letu linalosambaratshwa kwa kasi ya mwanga.Tuchukue hatua sasa.
 
Tuheshimu Katiba iliyopo japo ina mapungufu. Kama tunataka kupanua muda wa ukomo wa uongozi wa nchi, basi tuanzie kwenye mchakato wa Katiba.

Halafu tukiongeza muda iwe ni haki ya watu wote kugombea including Jakaya Kikwette na Mwinyi waliopo hai. Tusijidandanye kwamba JPM anapendwa au amefanya mambo makubwa kuliko wengine. Ngoja tuweke uwanja sawa tuone kama anaweza kupata hata 10% ya Jakaya Kikwette.

JPM kwa huu uchaguzi wa 2020 kiukweli aliiba uchaguzi wote. Yaani kura zilitengenezwa na ma DSO wa kila wilaya. Halafu vyombo vya habari haviko huru kuandika ukweli. Vikiandika vinafungiwa na Dr Abbas Katibu Mkuu Habari.

TUSIDANGANYIKE, kuna watu wana vision kuliko MAGUFULI na wanaweza kuifanya Tanzania ikapiga hatua bila kuua wakosoaji wala kunyang'anya fedha za matajiri
 
Akimalizia mazungumzo yake kwenye mdahalo wa CCM unaorushwa mubashara TBC muda huu Mzee Butiku ameuliza "mbona Uingereza malkia yupo....., mbona Angela Merkel yupo miaka 16? Mradi tufate taratibu"

=======

MZEE BUTIKU: Mimi nampenda sana Rais Magufuli, ngoja niseme hili hapa leo. Watu wengi wanasema mkali, mimi ningependa awe mkali zaidi. Kweli ningependa huko aliko mkali zaidi kwasababu tusipojipanga vizuri na chama cha mapinduzi kisipojipanga vizuri kikasimia serikali yake vizuri, hatuwezi kuvuka sasa hivi katika dunia ya sasa hivi ya ushindani, dunia ya Marekani, dunia ya Wachina, Wahindi, dunia ya watu wanaoongezeka haraka, hatutavuka.

Kwahiyo mnataka Rais ambae ni mpole lakini ni mkali.

Hili la kutoka kutotoka ni la utaratibu, ameniuliza jana mtu wa Deustchwele mambo ya kung'atuka, sikutaka kuzungumza hilo. Nikasema mambo ya kuacha ni mambo ya kuzungumza tu, mbona waingereza, wazungu wameongoza miaka mingapi? mingi masultani haya yamekaa yanaendesha nchi zao, nani aliwauliza? Waongo tu, Waingereza hapo wana malkia, nani anamuuliza? Huyu mama Makel mwaka huu wa ngapi? Wa 16, kwa hiyo watanzania tuwe huru tukitaka kuzungumza mambo haya ya wakati, wakati ukifika tunazungumza tu, ni mambo ya kuzungumza mkitaka kuamua mnafanya.

Lakini yasitupotezee muda, sijui 10, 5, sijui atoke lini! Priority ya sasa hivi ni maendeleo ya wananchi. Lakini tufate utaratibu, hapana mazungumzo ya holela hapa, mazungumzo yanafata utaratibu.
Halafu huyu eti ndiye mwenyekiti wa Wakfu wa Mwalimu Nyerere!

Hivi alichokisema, kinaakisi matakwa na mawazo ya Mwalimu juu ya jambo hili?

Nani asimame apige kelele juu ya Kuiheshimu Katiba kama wazee na taasisi kama hii zinahofu kuisimamia?
 
Halafu huyu eti ndiye mwenyekiti wa Wakfu wa Mwalimu Nyerere!

Hivi alichokisema, kinaakisi matakwa na mawazo ya Mwalimu juu ya jambo hili?

Nani asimame apige kelele juu ya Kuiheshimu Katiba kama wazee na taasisi kama hii zinahofu kuisimamia?
Butiku - " Madaraka yote ya serikali na ya chama cha mapinduzi yanatoka kwa wananchi"
 
Kutegemea huruma kwa Magufuli no sawa na kusubiria Shetani aokoke.

Chukulia mfano wa tukio liliompaya Lissu. Kumvurumisha binadamu mwenzio risasi 36 mchana kweupee ni moja kati ya TUKIO BAYA SANA NA LA KIKATILI kupindukia. Na kibaya zaidi mtu huyo huyo akiwa kitandani anapigania UHAI WAKE unatumia MAHAKAMA na BUNGE kumsulubu kikamilifu.

Nakwambia probably wewe ukiambiwa ufanye hivyo hata kwa MBWA tu HUTAWEZA.

Kipindi hiki cha Information Age, ignorance ni choice, sio matokeo ya uchache au ukosefu wa vyanzo vya knowledge.

Fanya utafiti upate kujua kuwa assassination of politicians (waliomo serikalini/nje ya serikali) and civil rights leaders duniani ilikuwepo zamani, ipo sasa na itaendelea kuwepo miaka ijayo. Nakushangaa kwa kushangaa assassination attempt wakati kuna successful assassinations kibao!
 
Butiku anataka kurudisha vurugi za kina Cyprian Musiba, Kinana, Nape na wengine!
 
Ana Uwezo wa kufanya lolote wakati wowote kwa kuwa watu wamekubali kujipa uvumilivu na subira ya ten years

Kuna Wana Ccm wengi wapo kwny Mawe kwa kuwa tu hawapatani nae ila wanajipa matumaini kuwa kabakisha miaka minne kama wale waliovumilia wakati wa Mkapa, Jakaya na Mwinyi

Ikidhihiri kuwa jamaa hatoki maana yake na wao ndio mwisho wao wa Siasa na hapo ndio utapoona usichoamini

Naamini JPM anajua hilo na ataheshimu muda wake ukifika ataondoka!

JPM anaweza kupata 100% kwny NEC na CC lakin anajua hizo asilimia haziakisi uhalisia wa vifuani
Hata hivyo ukiachana na precedent ya marais wa huko nyuma kuondoka madarakani, hakuna kitu kingine cha kumzuia.

Watanzania washapigika kikamilifu, njaa na kukata tamaa. Tayari wako KIBRA.

Wanaishi kwa matumaini tu.

Ni yeye tu aamue kubaki au kustaafu, hakuna wa kusema chochote wala kumzuia.

Kama ni katiba anaivuruga kila siku.( Angalia suala la Wabunge wa CHADEMA maarufu kama COVID-19 ).

Kwasasa ana uwezo wa KUFANYA CHOCHOTE wakati WOWOTE.
 
Tunaweza kuona Kama Ni utani kumbe wako serious!

Huwenda sisi wananchi tusiwe na la kufanya iwapo wataamua kufanya lolote.

Lakini Ni kawaida ulimwengu unaongozwa na kanuni, na moja wapo ya kanuni ya asili ya ulimwengu ni haki.

Basi Kama ni haki yao kufanya hivyo na iwe hivyo, lakini Kama si haki yao na wakifanya hivyo basi ulimwengu utatulipia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania Urais ni miaka kumi tu! Hatutaki ya Rwanda yatufike. Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 55, haiwezekana mtu mmoja tu ndiye awe na uwezo wa kuingoza! hata Kichuguu anaweza kuiongoza Tanzania kwa ufanisi sana!
 
Mizee mingine bure kabisa yenyewe ipo kimaslahi tu ni hiyo hiyo ndio ilikuwa ikimshawishi Nyerere na hata wengine waliofuata na mara zote ni njaa ndio zinawasukuma, ni aibu kubwa kwa mtu mzima kujitoa ufahamu na kujipendekeza kwa mtu uliomzidi umri
Diplomatic mzee wa watu, mbona hata vijana wanao fanana kimawazo na huyo wako wengi tuu. Muono wa kisiasa hata ukikera wengi kuna wachache wakuushabikia watakuwepo.Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom