Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu


Nyerere ambaye ndiye architect (mbunifu) wa katiba inayompa Rais wa JMT absolute power, alishabaini ujio wa Rais dikteta wa kiwango hiki na zaidi atakayesababisha nchi iingie kwenye kilio na kusaga meno!

Na kwa ule mtizamo wa Watanzania wengi wa kuweka mbele maslahi binafsi na kutoaminiana kwenye maslahi ya pamoja, hakuna wa kumzuia JPM kufanya anachotaka. Analijua vizuri sana hilo na anajua hakuna mwenye utashi wala ujasiri wa kupambania maslahi ya taifa. Kubwa zaidi anajua kuwa yeye (kauli yake) ndiyo katiba; ndiyo sheria!
 
Ghafla TAIFA lililokuwa linaonekana kama taifa KUBWA leo linapuuzwa na DUNIA na wajinga wachache wanachekelea.
 
Demokrasia ni maamuzi ya watu wengi, wengi wakisema katiba ibadilishwe basi ibadilishwe. Wakikata wengi basi tuwasikilize. Ila mambo ya Rais akae miaka 10 tu ikiiasha atoke hata kama ni mfanyakazi mzuri naona ni ukakasi. Vitu vizuri vinalindwa

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Ni haki ya simba kunyonya damu ya swala na kula nyama yake, ni wajibu wa swala kumshinda simba mbio na mbinu ili aishi muda mrefu. Hakuna ulimwengu hapo, Jiandae kukimbia au kubali kuliwa.Naomba weka hilo akilini. Usiwe mtu wa kulalamika na kusubiria ulimwengu uamue kukutafutia haki.

MM NIMEJIWEKEA NADHIRI SITALALAMIKA LALAMIKA, KUMBUKA KILA RAIA ANACHOTAFUTA NI MAISHA BORA, RAISI HATA AKITAWALA MILELE KAMA SIPIGANII KUMTOA BASI NITAPIGANA KUWA NA MAISHA BORA CHINI YA UTAWALA WAKE.
 
Mzee Butiku anasema tulishawahi kutengeneza kifaru...tena ile amphibian..

Lakini hasemi tulishindwa wapi.

Bado haamini kama tupo Tanzania ya viwanda.
 
This is unconscionable political intolerance. Mtu hawi takataka kwa sababu tu ametofautiana na wewe kimtazamo!
Mzee Butiku si takataka. Tuheshimu hawa wazee.

Actually kuna wakati anasema mambo mazuri tu. Kuna kipindi aliongea vizuri sana kuhusu wananchi kuacha woga, na kujitambua kwamba viongozi ni watumishi wao. Nilimuona mtu wa maana sana kwa kauli ile, kwa sababu ilikuwa kauli ya principle na hakujali kama utawala wa sasa utamuona "mstaafu mwenye kiherehere".

Angalia video hii hapa. Tena alirudia maneno haya katika kikao cha CHADEMA.

Who else from CCM does that in Tanzania today?


Sitaki kumuita huyu mtu takataka. Ana ujasiri wa kuongea principle kuliko watu wengi sana Tanzania.

Kwa hiyo mimi nafikiri amewakilisha maoni yake. Bila kujipendekeza wala woga.

Lakini, maoni hayo ni potofu.

Kwa sababu ni dtstingbthe obvious (kila kitu kinatakiwa kwenda kwa maoni ya wananchi) but usingbthat to undermine a legitimate constitutional principle that has no reason to be changed (term limits)

Kwa sababu ni logical tautology.

Kwa sababu ni cherry picking arguments.
Yuko tayari kusikiliza, kuheshimu na kutekeleza maoni ya wananchi kuhusu mgombea binafsi? Kuhusu kuvunja muungano? Kuhusu viongozi wa Ikulu ya Nyerere kuchunguzwa?

Kama issue ni maoni ya wananchi tu, mbona swahiba wake Nyerere alirudisha vyama vingi licha ya Tume ya Nyalali kusema asilimia 80 ya Watanzania hawataki vyama vingi?

Kama issue ni maoni ya wananchi tu, mbona CCM wameanza kuiba kura Zanzibar kabla ya vyama vingi, na Butiku hajakemea chama chake kwa kuiba kura na kubadili maoni ya wananchi?

Kama issue ni maoni ya wananchi, mbona muswada wa katiba mpya uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba, unaokubqlika kwa wananchi wengi, umetupwa kapuni?

Kama issue ni maoni ya wananchi, mbona wapinzani wanakatazwa hata kuandamana tu?

Au issue ni maoni ya wananchi kwenye mambo fulani tu, mengine yanaenda kwa amri kutoka juu?
 
"[emoji445][emoji445][emoji441]Butiku hovyo, Butiku hovyo[emoji443][emoji443][emoji443]huyoo mnafiki wa utawala[emoji443][emoji443][emoji445] Butiku hovyo!!"

Ipo siku kikundi cha vijana kitaimba hivi. Mzee ajitafakari
 

Mzee Butiku ana haki ya kumpenda Magufuli tani yake. Hiyo haituhusu; ni mambo yake binafsi. LAKINI sioni kama kuna tija yoyote kwake kumlinganisha Rais wa Tanzania na Malkia wa Uingereza na Chancellor wa Ujerumani.

Kama kweli ameuliza hivyo, asishangae tukimtambua kama mjinga (ignorant) asiye kifani. Kama ndiyo madhara ya kupenda sana mtu basi ajifikirie sana anakoelekea. Kwa mtu wa enzi hizo, aliyepata elimu bora na kuwa kwenye nafasi za juu za utawala wa nchi kutamka ujinga wa kiasi hicho, inatisha!

Ni uamuzi wake kutaka Magufuli aendelee kuwa Rais miaka yoyote ile hata milele. Wako Watanzania kibao wenye kutaka hivyo. Lakini asingejiadhiri kiasi hicho kwa sababu hiyo. Wako wadau hapa ndio kazi yao hiyo rasmi.
 
Ukomo wa urais sio suala la utaratibu, ni takwa la katiba na unapotaja katiba maana yake unagusa sheria...

Ndio maana ni lazima kipengele cha ukomo kibadilishwe kwenye katiba kwanza

Tatizo ni kuwa kiuhalisia, Rais wa JMT ndiye katiba na sheria! Yeye ndiye dola (na mihimili yake yote). Hakuna wa kuhoji maamuzi wala mipango yake. Akiagiza kitu kinachofuatia ni utekelezaji tu.

Mwendo uliopo sasa ni kama enzi za Mfalme Louis XIV wa Ufaransa anavyodaiwa kujigamba kwa watu waliokuwa wakihojihoji madaraka yake: “mimi ndiye dola” (L'état, c'est moi).
 
Utalikubali tu. Mjadala ndo unaanza hivyo. It's just a matter of time!


"But time is a common aspect to all of us", it doesn't matter who you are!!, just the time will tell.

Tears of an oppressed never run in vain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…