Amnyimaye punda edesi kampunguzia mashuzi.
CHADEMA itaimarika sana kuanzia sasa kuliko ilivyokuwa. Uwepo wa Lowasa uliwanyima sana uhuru CHADEMA, wa kusema baadhi ya mambo.
Mwaka 2015 ulikokota kila mtu bila kujali anakuja na nini. Bahati mbaya wote waliokokotwa wanarudi walikotokea.
Namwamini sana Nyalandu. Na hata namna alivyoondoka CCM na kujiunga CHADEMA, na namna anavyotenda kazi tofauti na hawa wote walioletwa na upepo wa Lowasa.
Mbowe na Tundu Lisu tunawatakia uongozi mwema. Sina mashaka, mtachaguliwa kwa kura nyingi. Mnakijua vizuri sana hiki chama. Chama hiki kinabeba mateso yenu, damu zenu, mali zenu na mahanagaiko yenu. Pembeni yenu kuna makamanda wasiotiliwa mashaka - Halima, Msigwa, Heche, Lema, Lijuakali, Mwalimu, n.k. ambao imani yao haitiliwi mashaka.
Yaliyotokea 2015 na madhara yake yatoe funzo na yakiimarishe chama ili ya namna hiyo kamwe yasirudiwe.