Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

sumaye ekimrara lowasa.jpg
 
Hawa wazee wapumzike wamelitumikia taifa muda mrefu, ni uamuzi mzuri sana kwake - active politics zinatakiwa nguvu, ari kubwa ambazo zinatakiwa kufanywa na vijana na watu wa umri wa makamo wenye kujitoa kwa jasho na damu - Mzee wetu alishafikia level ya juu kabisa ya utendaji ndani ya Serikali - apumzike ale pesheni yake na wajukuu... hii mikiki mikiki ya mahakamani, mahabusu, sero awaachie kina Mnyika, Lissu, Lema, Sugu, Mdee, Heche.

Hata mashamba yake naona sasa yatarudishwa rasmi, na jumba letu jeupe mara moja moja ataanza kualikwa.
 
Hana miaka hata mitano anataka uenyekiti.......

CHADEMA walibugi 2015 kwaio wanachofanya sasa ni kusahihisha yale makosa, kwa gharama yoyote including kumfyeka sumaye! Wyatt Mathewson,
 
Amnyimaye punda edesi kampunguzia mashuzi.

CHADEMA itaimarika sana kuanzia sasa kuliko ilivyokuwa. Uwepo wa Lowasa uliwanyima sana uhuru CHADEMA, wa kusema baadhi ya mambo.

Mwaka 2015 ulikokota kila mtu bila kujali anakuja na nini. Bahati mbaya wote waliokokotwa wanarudi walikotokea.

Namwamini sana Nyalandu. Na hata namna alivyoondoka CCM na kujiunga CHADEMA, na namna anavyotenda kazi tofauti na hawa wote walioletwa na upepo wa Lowasa.

Mbowe na Tundu Lisu tunawatakia uongozi mwema. Sina mashaka, mtachaguliwa kwa kura nyingi. Mnakijua vizuri sana hiki chama. Chama hiki kinabeba mateso yenu, damu zenu, mali zenu na mahanagaiko yenu. Pembeni yenu kuna makamanda wasiotiliwa mashaka - Halima, Msigwa, Heche, Lema, Lijuakali, Mwalimu, n.k. ambao imani yao haitiliwi mashaka.

Yaliyotokea 2015 na madhara yake yatoe funzo na yakiimarishe chama ili ya namna hiyo kamwe yasirudiwe.
 
Watu walijitenga Everton wakaenda kuipa nguvu Liverpool, watu wakahama mancity wakatengeneza Manchester United , watu walihama Yanga wakatengeneza Simba

Wapinzani wa kweli watatoka CCM Tu na nothing else, Mbowe aliyeishia kupata zero form six hawez fanya lolote Zaid ya kuongeza viti viwili vya ubunge kila uchaguz....Dr slaa alipotoka CCM alionyesha impact kubwa Sana, lakn ndoto zake za kugombea uraisi zikazimwa kihuni na mtu ambaye Hana maono na elimu ni zero
 
Wakati anaondoka chadema alitoa hoja zake nyingi sana,lakini kubwa ni ile ya kupinga kumpokea Lowassa na Sumaye ambaye kwa maoni yake alisema Sumaye hana "tija" yoyote kuhamia CDM.....naam Dr.Slaa was absolutely right.
kwa sasa DR. Slaa yupo wapi na Lowassa yupo wapi? Choo alichokikimbia sebureni akiwa CDM naona sasa kimemfuata chumbani.
 
kwa sasa DR. Slaa yupo wapi na Lowassa yupo wapi? Choo alichokikimbia sebureni akiwa CDM kinamfuata.
Unataka kusema Dr. Slaa hivi sasa ni CCM? Cheo chake sio cha kisiasa. Yeye ni mtumishi wa serikali tu.
 
Tukisema Mbowe ni dictator nyumbu hawaelewi, ila sasa wanaanza kuelewa, kilichomkuta Zitto ndio kimemkuta Sumaye, huko CDM ukitaka tu kugombea uenyekiti - taifa, lazima ufukuzwe au utaitwa msaliti au utazimwa ktk kura za awali ndani ya CDM
 
Mambo matatu muhimu:
1. Policy makers wa CHADEMA watafakari kuhusu hatua waliyochukua kuwapokea watu wa CCM. Hii iwe fundisho, Viongozi wa CHADEMA wawe wanafanya risk assessment kwa kila jambo wanalokuwa wanataka kufanya.
2. Kulingana na siasa za namba moja, ni sahihi kwa yeyote aliyekuwa na makando kando kuufyata. CCM wanajulikana, nani msafi?
3. Kujiunga na upinzani haijawahi kuwa rahisi ukiachilia kutahamalaki kwa chuki za waziwazi hii leo nchini.
 
Back
Top Bottom