Kuna mambo mawili ya Slow slow yamenishangaza
1. Mgombea mmoja Jana akichukua form alibadili salamu yake, ameonyesha humbleness ya hali ya juu kama kweli ameona kosa lake la kuishusha chini salamu inayomtanguliza Mungu
2. Leo mic imezimwa, naipongeza taasisi kwakuona kuwa heshima ya Mkuu haitakiwi kupunguzwa na yeyote. Tumeapa Kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ngao inayobebwa Kwa awamu na Kwa ridhaa ya watanzania
Kesho nini kinafuata? Tanzania njema inachomoza taratibu bila kujalisha nani atakuwa kwenye usukani, watanzania Wana nafasi ya kuamua tena, glory be to God!
Slow slow unatisha ila naomba nikuambie na wewe ulituonyesha uko arrogant wakati una power, lugha kama "unajua viet wewe", na juzi tena umerudia huyu ni wakuzungumza na Mimi? Kwani wewe nani tusizungumze na wewe? Kama hata Mungu katupa nafasi ya kuzungumza naye seuze wewe kiumbe chake? Ishara ya kiburi tabia kuu ya wote walioanguka kama Malaika wa Nuru i.e Kerubi aliye aminiwa kuwa mpiga sifa mwenye vipaji vya uimbaji mbinguni. Mimi naKuambia haifai hiyo Kwa mtu unayesema Yesu kwako ni Bwana, unahitaji rehema, tubu sasa Ili jina la Mungu lisitukanwe kwaajili yako....Be humble hata kama Mungu amekupa upendeleo, Yeye aweza kukufanya kama mfalme Nebukardneza ukaenda kula nyasi porini kama ng'ombe.
Lakini naiombea nchi yangu amani pamoja na wote wanaoipigania Kwa nia njema bila kujali maslahi binafsi, tupo pamoja. Tanzania njema is a must, it's a decree?