Mzee Kikwete: Wanaolalamikia kupanda kwa bidhaa ni unafiki mkubwa

Hahahaaa!!! Safi sana kwa jibu lako na wakati ni huu wa majibu ya namna hii.
Mungu akuweke miaka mingi mnooo
 

Please punguza dhihaka. Kama wewe umeshiba usimtukane mwenye njaa. Eti asilimia 90 ya watanzania wanashindana bar? Unajua unachokiongea?.
 

duuh . inasikitisha
 
Amuache vp wakti jiko ni lake lile remote ipo kazini
 
Hapa naamini Kikwete amekuwa quoted out of context.

Kikwete ni mwana diplomasia wa kimataifa hawezi kuongea utumbo huo.
 
Rais huyu tuliye naye sasa hana majibu yoyote kwa matatizo yetu. Rais huyu walifika wale viongozi wa dunia intellectuals kuongea naye,wanachagua maneno mepesi ili aelewe.
Nchi haina mwelekeo,haina nidhamu ya kazi. But that is about to change.
 

Acha uongo, unataka kulinganisha Tanzania na uingereza?. Tatizo wananchi mnakalia kuwatetea wanasiasa baadala ya kuongea Lugha moja. Shauri yenu kama mpo tayari kufa na njaa lakini mumfurahishe mwanasiasa.
 
Chumi zote zimeathirika na matukio ya dunia,ndiyo mfanano wake,chuki zako zinatokana na ujinga

Kwa hivyo uchumi wa Tanzania Unalinganisha na uingereza?. Tuache uongo.
 
Babaako nae angejiunga tanu youth league Kisha CCM,na Kama angekuwa kaelimika walau kidogo,basi angepata nafasi za juu na mishahara Kama kikwete aliyopata,Ila mzee wako ngumbaru na we mwenyewe ngumbaru

Unatukana wazazi wake kwa Nini?. Hizi dharau zenu za kijinga hazina nafasi. Huyo Kikwete mwenyewe kapata urais kwa kuomba kura kwa maskini nchi nzima, Leo unaongea kana kwamba urais alijipa mwenyewe.
 
Hali ilianza kuwa ngumu alipokuja Mbowe

Nyie bakini na siasa kwenye mambo ya kitaifa yasiyo hitaji siasa au vyama. Unamuingelea Mbowe Kama ndiye Rais wa nchi. Wananchi tubadilike, tunalala njaa lakini kutwa kumsema Mbowe na kuwachekea na kuwasifu wenye mamlaka ya kubadilisha Hali ya Maisha.
 
Serikali zinatakiwa kupanga kwa emergencies.

Ndiyo maana kuna Strategic Grain Reserve, Strategic Petroleum Reserve etc.

Yani serikali ilitakiwa kuwa na stock kubwa, kwenye matatizo ya njaa au ukosefu wa mafuta, serikali inaachia mzigo wake wa reserve ili kusaidia kupunguza makali ya kupanda bei.

Marekani ni mabepari na hawapendi serikali kuingilia biashara, lakini Biden alifungua reserves za serikali z amafuta kupunguza ukali wa bei ya mafuta.

Tukubali tu kwamba serikali yetu haijajipanga kwenye mambo kama haya na mtu kama Kikwete baada ya kukaa serikalini miaka yote hiyo, kusema hivi bila aibu, anaonesha tatizo la uongozi kwetu lilivyo kubwa.

Soma habari za White House kuhusu mpango wa Biden kukabili mfumuko wa bei ya mafuta Marekani, sasa Kikwete hajui serikali inatakiwa kufanya hivi?

 
Uhujumu unaofanyika passively ndio huo. Tuna mengi ya kuboresha kabla ya kuwaza mapya na maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…