Mzee Makamba aliwaza nini kusema ''Watu wazuri hawafi''?

Mzee Makamba aliwaza nini kusema ''Watu wazuri hawafi''?

Hivi aliyetoa hii kauli alimaanisha nini na kwa nini? Je, waliokufa kwenye familia yake au ukoo wake wote ni wabaya?

Ingekuaje watu hawa wangepewa mamlaka ya kusimamia kugawa pumzi ya uzima na hewa safi tunayopumua kila siku?
Kwakweli kwa kauli hii alikosea sana na ni Kufuru kwa Mwenyezi Mungu anayetujalia uzima
 
Katika Philosophy MTU mzuri huwa hafariki

Mfano tazama katika familia yako utapata jibu

Pia tazama kuhusu Mandela na Nyerere.

Mzee Mkamba he was right to speak that ila watu wameshindwa kuelewa hili jambo .

Binadamu mzuri mwenye utu huwa anaondoka katika mwili wa nyama Ila yeye anaendelea kuishi.
Uzuri wa Mandela na Nyerere ni upi hasa
 
Wazuri hawafi inamaanisha watu wema wanaacha legacy ambazo hata wakifa zinakumbukwa kwa muda mrefu...

Chukulia mfano mtaani kwenu kuna shida ya maji, aje mtu ajenge kisima kikubwa kihudumie mtaa mzima, huyo mtu hata Akifa legacy yake inabaki.
Ni sawa, Mtu hukumbukwa kwa Mema au Mabaya yake hapa Duniani hata baada ya kufa

Ila sidhani kama huyu Mzee alimaanisha hilo, uchawa ndio uliompelekea kusema hayo
 
Na yeye tuna subiri keshokutwa watangaze RIP WAZURI HAWAFI.sasa hivi wako kimya

Rip mzee
Sasa wewe unaishi ukisubiri RIP ya mwingine na yako hujui ni lini? Kuna ajali ishaua watu huko barabara ya bagamoyo, daladala na lori zimegongana. Watu wamekufa ambao hawakufikiri kuwa siku yao ni siku ya leo.
 
Wazuri hawafi inamaanisha watu wema wanaacha legacy ambazo hata wakifa zinakumbukwa kwa muda mrefu...

Chukulia mfano mtaani kwenu kuna shida ya maji, aje mtu ajenge kisima kikubwa kihudumie mtaa mzima, huyo mtu hata Akifa legacy yake inabaki.
"Wazuri hawafi ndio maana Kikwete na Kinana BADO WAPO"

tafsiri yako haiendani na alichosema Makamba
 
Kwa hiyo kikwete hana legacy yeyote ndani ya nchi hii?
Ebu jaribuni kupunguza chuki za kipumbavu hazitakusaidia kupunguza ugumu wako wa maisha.
Hizi ni akili za kimaandazi tu! Kama mtu mzuri hafi inalenga watu waliokufa na wakaacha legacy, ilikuwaje mzee wako Makamba akataja ambao hawajafa? Kwa nini hakuwataja kina Nyerere?

Mzee wako alitamka neno la kijinga
 
Sasa wewe unaishi ukisubiri RIP ya mwingine na yako hujui ni lini? Kuna ajali ishaua watu huko barabara ya bagamoyo, daladala na lori zimegongana. Watu wamekufa ambao hawakufikiri kuwa siku yao ni siku ya leo.
Na ndiyo maana tunaendelea kukemea kauli ya mzee wako Makamba!

Mamia kwa maelfu ya watu wanaokufa kila leo, kwake yeye hao wote ni wabaya??

Walale pema na pole sana kwa wafiwa, poleni Watanzania wenzetu

Mzee aombe radhi iwapo amebakiwa akili japo kidogo
 
Na ndiyo maana tunaendelea kukemea kauli ya mzee wako Makamba!

Mamia kwa maelfu ya watu wanaokufa kila leo, kwake yeye hao wote ni wabaya??

Jinga kabisa
Ushasema ni mzee. Uzee unakuja na mambo mengi, huwezi jua kichwa chake kilimaanisha nini.

Juzi kulikuwa na msiba kuna mzee mmoja kafiwa na mdogo wake watu wanampa pole anauliza nani kafariki, anashangaa kuna msiba? Wakati na yeye yupo msibani. Ubongo ushafuta.

Mwinyi kuna siku aliuliza jukwaani hapa ni wapi? Inamaana ubongo ulishafuta kuwa yupo wapi na anafanya nini hapo.
 
Hivi aliyetoa hii kauli alimaanisha nini na kwa nini? Je, waliokufa kwenye familia yake au ukoo wake wote ni wabaya?

Ingekuaje watu hawa wangepewa mamlaka ya kusimamia kugawa pumzi ya uzima na hewa safi tunayopumua kila siku?
Mara nyingi kufuru hutoka wakati wa over excitement!!!

Sasa Mzee alifurahi alipoona mwendazake kaenda na ana amani ya kutosha akaanza kubwabwaja!!

Makada was chama wakongwe wanaondoka sana ,hatujui huyu na kauli yake kama atatoboa!!

"Wazuri hawafi" italeta shida sana!!
 
tazama kuhusu Mandela na Nyerere.
Huyo Nyerere wako Kuna waislamu kibao hapa Bongo hawamkubali achilia mbali watakao kwambia mapito waliyopita watu enzi za vijiji vya ujamaa na sera zake mbovu za kiuchumi zilizopelekea yeye kujiuzulu na vp stori za kina bibi titi na Kambona.
Mzee Mkamba he was right to speak that ila watu wameshindwa kuelewa hili jambo .
Kama angekuwa sawa mweshimiwa Rais asingemuombea msamaha. Kwahiyo hakuwa sawa.
Binadamu mzuri mwenye utu huwa anaondoka katika mwili wa nyama Ila yeye anaendelea kuishi.
You are right lkn hata watu wabaya hukumbukwa kwa ubaya wao.
 
Ushasema ni mzee. Uzee unakuja na mambo mengi, huwezi jua kichwa chake kilimaanisha nini.

Juzi kulikuwa na msiba kuna mzee mmoja kafiwa na mdogo wake watu wanampa pole anauliza nani kafariki, anashangaa kuna msiba? Wakati na yeye yupo msibani. Ubongo ushafuta.

Mwinyi kuna siku aliuliza jukwaani hapa ni wapi? Inamaana ubongo ulishafuta kuwa yupo wapi na anafanya nini hapo.
Ulichokifanya mkuu ni kuni 🤣🤣🤣

Asante nimeongeza siku za kuishi aisee

Ila Mzee Makamba, alikosea sana
 
Back
Top Bottom