johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mzee Makamba amesema Wanaccm Wana Iman kubwa sana na Rais Samia na 2025 atashinda kwa kishindo
Mzee Makamba ametaka CCM kupitisha Azimio la kumpitisha Rais Samia kuwa mgombea Urais pekee kea ticket ya CCM 2025
Makamba amesema hakuna haja ya kuogopa kwani Watu wazuri na wanaopendwa hawafi ndio sababu mzee Kinana yupo na mzee Jakaya yupo
Makamba amesema Wapinzani akina Chadema ajenda zao ni 2 tu Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi lakini Wananchi hawali Katiba. Kule kwetu kwa mfano Wananchi wanataka Maji, Umeme, Huduma Bora za Afya na Elimu ambazo zimo kwenye ilani ya CCM hivyo Wapinzani wasahau kabisa habari ya Ushindi 2025
Hata hivyo Rais Samia amesema Mzee Makamba ameteleza tu ulimi kwa Kauli hiyo ya kwamba Watu wazuri hawafi kutokana na kuwa emotional
Chanzo: TBC