Kenya 2022 Mzee Odinga Kaamua: Kwa hizi Evidence Ruto Atapona kweli?

Kenya 2022 General Election
Hivi si mshindi anatakiwa kupata 50% + 1 kwa hiyo hata kama hiyo 2 decimal points . 99 ikiwa rounded 50 bado siyo halali kutangaza ushindi. Kama nimekosea kuelewa nieleweshwe.
 
Hawezi kukuelewa huyo, akili yake imekaa ki-CCM
 
Hivi si mshindi anatakiwa kupata 50% + 1 kwa hiyo hata kama hiyo 2 decimal points . 99 ikiwa rounded 50 bado siyo halali kutangaza ushindi. Kama nimekosea kuelewa nieleweshwe.
Upo sahihi kabisa Mkuu
 
Una ufahamu wowote kuhusu election petition? Mahakama haiangalii ukubwa wa kosa bali inahitaji tu kuthibitisha "beyond reasonable doubt" kwamba palikuwa na udanganyifu full stop.

Hata kama uliiba kura mbili ambazo zisingeweza kubadilisha matokeo ikithibitika ziliibwa basi badi zina nullify the whole process. That's law.
 
Kwamba wewe mpemba wa Wete sijui Chake Chake unajua masuala ya ndani ya chaguzi za Kenya kuliko waliokuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho?

Odinga sio mjinga hadi aseme ana ushahidi wa kutosha juu ya uchaguzi kuhujumiwa.

Ruto ni mafia ni mzoefu sana kwenye sarakasi za uchaguzi hivyo uwezekano wa kupora kura u mkubwa.

Uchaguzi wa 2017 ilikuwa hivi hivi kuna watu walizungumza kama wewe kwamba uchaguzi umefanyika kwa njia huru wakuwa wana tume huru hivyo Odinga hata akienda mahakamani hatoshinda.

Nakumbuka mahakama ilikubaliana na hoja zake zote na uchaguzi ukafutwa bahati mbaya Odinga akasusia marudio ya uchaguzi hivyo Uhuru kupeta kirahisi.
 
Huyu mzee uchaguzi kila sikua analalamika tu, akubali kuwa uraisi sio zali kwake
Huoni kwamba ana hoja za msingi juu ya malalamiko yake? Uchaguzi wa 2007 mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya alikiri wazi kushinikizwa kumtangaza Mwai Kibaki kama mshindi wa Urais tofauti na uhalisia.

Mwaka 2017 Odinga alienda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu na mahakama ya upeo ilikubaliana na hoja zake na kuufuta uchaguzi wote hivyo kuamuru marudio.

Odinga alisusia marudio kwasababu alihoji kwanini yafanyike marudio wakati mshindi halali anajulikana ni Odinga kwanini asiapishwe kuwa Rais?

Sasa malalamiko yake yana msingi kabisa maana amekuwa akishinda chaguzi nyingi tatizo baadhi ya Wakenya wachache wafia ukabila hawataki mjaluo aongoze nchi ndo shida ilipo.
 
Fomu zipi hazikuwa verified? Mi nazungunzia fomu 34A ambazo ndiyo fomu kutoka vituoni na ndio msingi wa matokeo yote kwenye fomu nyingine

Fomu 34A kuna copy zake zote online ambazo mtu yoyote unaweza kujumlisha na kupata matokeo na hardcopy za 34A zote zilipelekwa Bomas na pia mawakala wa Odinga walipewa, kama kuna uchakachuaji wowote wangesema ni wapi

Nimesoma huo ushahidi wao wa awali hakuna sehemu yoyote ambayo wameonyesha matokeo ya kwenye 34A yamebadilishwa tofauti na walipewa mawakala wao
 
Kasome petition kule zimewekwa fomu 34A ambazo Zina conflict kwenye tallying. Nyingi ni za Mount Kenya ambako Odinga hakua na mawakala wengi.

Kingine form34A za kwenye portal ni provisional ila zinazotambulika ni zile verified pale BOMAS, na mpaka matokeo yanatangazwa hawakuwa wameverify 34 A za majimbo 27!! Kinyume na sheria.

Mahakama itatupa mbivu na mbichi
 
Petition nimeisoma mkuu, kwenye petition hakuna ushahidi wowote kuwa kuna utofauti wa matokeo ya fomu 34A zilizopo kwenye server na zilw hardcopy, hakuna.!

Hiyo ya mount Kenya ulikosema, wanachodai wao ni kuna kaunti ya Kirinyaga ambapo matokeo ya kura za urais yalikuwa na total votes nyingi zaidi ya 22,000 kuliko total votes za ugavana, kitu ambacho nacho ni uwongo kura zimewekwa wazi, za urais na ugavana zinatofautiana kwa 900 pekee

Kutokuwa na mawakala hilo ni kosa lake mwenyewe na sio proof kuwa aliibiwa kura

Na hao wanaosema hawaku verify matoeo ya majimbo 27 ni wale makamishna 4 ambao ni famba wasiojua hata hesabu, kila kitu kilikuwa verified
 
Petition umeisoma kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…