Naona mzee machache kaacha mali familia ipo kwa pilato
 
Kwa hiyo Yanga wana msibamsibal
 
Wengine tukifa tusipowakumbusha ndugu zetu tunaweza kusahaulika mochwari.

RIP.
 
RIP. Wanawezaje kutunza na kukuza utajiri vizazi hadi vizazi?
Mkuu sisi waswahili tuna matatizo sana vichwani mwetu.

Mtu mmoja kwenye ukoo au wawiki wakiwa na pesa nyingi au mali nyingi ikitokea mmoja wa wana ukoo akawa anashirikiana nae bega kwa bega basi itaanza fitina na wivu usio na maana yeyote ile zaidi ya kufarakana na hatimae kujengeana uhasama wa kifamilia.

Roho mbaya na chuki ndio imetawala mioyoni mwetu kwa wengi wenye mawazo na fikra za kimasikini.

Kiuhalisia wenzetu wanarithishana mali kuanzia mababu mpaka vitukuu na watu hauwezi kusikia wakiwa na mgogoro kati ya watoto wa baba mkubwa na mdogo au mjomba na shangazi.

Hii ni kitu mimi imeshanikuta kwenye familia zetu hizi na kupelekea watu kukuwekea,

chuki na wengine kuwaacha na hatimae watu kufilisika na kisha kuanza kuona kwamba wametengwa lakini chanzo cha yote ni ubinafsi na kujiona kwamba,

wao kama wao wanaweza kusimama peke yao ila ukweli siku zote ikitokea kwenye familia mmeanzisha jambo na muanzilishi ni mwenye taaluma hiyo na yeye ndio anarun na kuwafundisha wenzake basi shikamaneni haswaa na si kuvurugana kama ilivyo kwa familia nyingi sana za kiswahili zilivyo.

Na ndio maana utaona mfano akifa mzee aliyekuwa akiendesha kampuni au biashara kubwa tuu utaona inaathirika moja kwa moja sababu ni waliomzunguka walikuwa ni watu wenye kujali unafaika wake pekee bila kujali maslahi mapana ya familia/ukoo wote na unakuta mzee huyo hao aliokuwa akiwaamini ndio hao hao wenye roho mbaya ambayo hapo awali hawakuionesha.
 
Lala mahali pema mzaa chema.
Nina miaka zaidi ya arobaini ya kuishi Dar. Sijawahi kuona muislamu asiye na pesa au wathifa akizikwa hapo atakapo zikiwa mpendwa wetu.
Je. Kisutu Kuna nini?

Mama yangu mdogo amezikwa hapo ila kwetu sisi ni Kapuku na hatuna wadhifa wowote
 
Masikini wengi tu miaka na miaka wanazikwa Kisutu

Wale tuliozaliwa na kukulia katikati ya jiji bila ya kujalisha kipato chako utazikwa Kisutu au makaburi ya Tambaza
Lala mahali pema mzaa chema.
Nina miaka zaidi ya arobaini ya kuishi Dar. Sijawahi kuona muislamu asiye na pesa au wathifa akizikwa hapo atakapo zikiwa mpendwa wetu.
Je. Kisutu Kuna nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…