G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,505
- 40,002
Hivi hii aibu tutaipeleka wapi siku tunaambiwa Breaking News kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa ajiunga CCM? Tena eti Polepole anakupa maelekezo ukajiunge tawini? Hapana hiki ni chama na kina wanachama wake waaminifu na watiifu kwa chama.
Hivi kwa haya yote tuliyokumbana nayo bado tukafanye majaribio tena kwenye ngazi ya uenyekiti taifa?
Mzee Sumaye bado unakula pensheni ya Rais Magufuli na kila mwezi anakusainia. Siku akigoma hadi urudi kama alivyofanya kwa matibabu ya Lowassa? Hapana kwa hiki kipindi cha huu utawala usio na haya tunahitaji chuma kweli kweli. Tunaomba wanachadema nguli mjitokeze kuwania nafasi kwani kwa hii miaka minne kama ni dhahabu basi mmejipika kweli kweli kisiasa.
Sitokaa niamini kweli kama Sumaye ni Chadema na sidhani kama anafaa kuwa mwenyekiti wa chama taifa. So sorry Mzee wangu! Endelea kuwa tu miongoni mwa wazee wa chama kwa sasa!