Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Hili pandikizi bora lirudi kwao kwenye zizi la wasiokuwa na mikia.

Huyo Sumaye ni mwanaccm aliye mapumzikoni cdm, amezoea ushindi wa mteremko huko ccm wa kupita bila kupingwa. Sasa kaingia kwenye mazingira hata ukiwa mwenyewe lazima kura zipigwe, na watu wamemkataa anaanza siasa na utetezi wa kuccm. Arudi ccm haraka akafanye siasa za mbeleko na hila. Eti anasema watu wamekwenda kuhamasisha, sasa kwenye siasa alitarajia kusiwe na kuhamasishana? Kosa ni kufanya ukatili, uhayawani na wizi wa kura, sio watu kuhamasishana ww usichaguliwe.
 
Mambo ya kawaida haya. Sijui kwanini Sumaye hakuwa na mpinzani kwenye uchaguzi huu. Nadhani uongozi wa chama unamthamini sana na ndiyo maana ulijaribu kumpa upendeleo huo wa kugombea bila mpinzani. Hata hivyo inaelekea kitendo hicho pengine kimewakwaza baadhi ya wanachama. Kwa maoni yangu Mzee Sumaye asikubali kukatishwa tamaa na yalitokea kwani ndiyo demokrasia. Hata Baba wa Taifa alishindwa kabisa kumwezesha chaguo lake kupata urais! Mchango wa Mzee Sumaye katika medani ya demokrasia katika nchi yetu inahitajika sasa kuliko ilivyokuwa 2015.
 
ukawa2020,

Haaa, nilisema juzi, Sumaye kafanyiwa uhuni na Mbowe ili ashindwe asiende kugombea uenyekiti, watu humu hawakunielewa, sasa Sumaye kasema mwenyewe kuwa ndani ya Chadema hakuna demokrasia kabisa.. Mmeona jinsi udikteta na hakuna kabisa demokrasia huko CDM, ila wenyewe wanajiona wanajua sana kumbe maneno tu
 
Hivyo ni dhana yako tuu, hapo mchezo no kuja kumuomba Sumaye aombe kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti taifa bara ana uwezo wa kufanya kazi ngazi ya kitaifa.
Prof Safari hafai tena?!
 
Unajibu swali ambalo hujaulizwa!

Umeona swali ni gumu ukaamua kujitungia swali lako mwenyewe na kulijibu!

Hakun analogy ya aina yoyote!

Sumaye hakupitia kuteuliwa popote pale kwanza!

Alichukua fomu na kaenda kwenye sanduku moja kwa moja!

Sanduku limeongea kua halimtaki!

Ulivyo mpumbavu kupita maelezo unasema “kakatwa”?

Sanduku linakata mtu?

Kura hazikutosha,full stop!

Lawama wape wapiga kura basi kama vipi!

Na wewe kumlaumu mpiga kura ni uchizi kabisa!

Ndio maana ulipitapita kwa kufaulu marks za ugoko kumaanisha kwamba darasani ulikua hujui kujibu maswali kama ulivyoonesha hapa!
Umemueleza vizuri, natumaini atakuelewa. Nondo kama tulivyo sote humu, yuko huru kutoa maoni yake lakini huwa nikisoma maandiko yake humu na vipisi vya articles anazoandika kwenye gazeti huko na kuleta humu, dah! Huwa nacheka sana aisee 😊😊 sina uhakika kama huko chuo alikuwa anapata marks za ugoko kama unavyosema lakini naona kabisa bado hana exposure ya kutosha ya kuandika haya ma comments na ma articles marefu kiasi hicho! Kwa mfano kuna siku mtu alimwambia humu, hakuna baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa, kuna UN Security Council, period, lakini kwenye Twitter huko nao wakawa wanarudia huo ujinga wa ulinzi blah blah. Nothing personal, ila kuna mtu anajaza upepo this kid.

Ushauri mdogo kwa vijana mnaochipukia kama Nondo na Yericko Nyerere , ukitaka kuwa mwandishi mzuri,writer, author , political analyst, political commentator, political pundit..etc. Exposure ni muhimu sana, someni vitabu vingi na majarida mbalimbali,someni kila siku na kufuatilia habari, current news yaani, jifunzeni geopolitics za kila mahali,political economy, economics, foreign policy za nchi mbalimbali, international relations, et cetera . Kama una passion ya kuwa mwandishi wa habari za ujasusi,the same applies, read. Kidegree kimoja cha PSPA hakitoshi.
 
Safi sana,hii ndo demokrasia.I wish wamkatae Mbowe pia.

Kumbe hujajua, hakuna demokrasia huo mchezo ni Mbowe anacheza behind the scene, so eti itokee kwa Mbowe tena hakuna kitu kama hicho, hakuna demokrasia ni hujuma tupu Sumaye kafanyiwa kisa uenyekiti, mbona huelewi na Sumaye kasema hapo wazi sbb za yeye kukosa kura?
 
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Hakujua kuwa CHADEMA ina mwenyewe? Ninapatwa na wasiwasi kuhusu IQ yake!

Unamtingisha Mbowe halafu unategemea kubaki na cheo ndani ya chama chake! Thubutu!

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa au kuondoka CHADEMA hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe katika kiti cha Mwenyekiti Taifa!
Niliwahi kusema Sumaye alishindwa na mama mery nagu tena akiwa waziri mkuu, sembuse leo yuko nje ya system? wajumbe 78 siunawaficha hotelini mwezi mzima tena unawapeleka Pemba. wakija wanakura mkononi zilishapigwa tayari nikufika na kutumbukiza
 
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Hakujua kuwa CHADEMA ina mwenyewe? Ninapatwa na wasiwasi kuhusu IQ yake!

Unamtingisha Mbowe halafu unategemea kubaki na cheo ndani ya chama chake! Thubutu!

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa au kuondoka CHADEMA hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe katika kiti cha Mwenyekiti Taifa!
Zitto nitafutahi kuona comment yako japo kwa maneno 4
 
Ndio maana baada ya sarakasi kwa Dr Slaa niliamua kuwa huru ili nione mambo kwa uhalisia badala ya ushabiki. Chadema hakuna chama pale. Huyo Sumaye soon anarudi alikotoka! Msishangae Lissu pia akafanya maamuzi ya kuwashangaza! Asirudi CCM lakini atatoa picha kamili. Kuna kakikundi kameihodhi Chadema na ni untouchable!
 
Unajua hii ni "part of human life" popote duniani. Hakuna mtu atashindwa kupata kile alichotaka katika uchaguzi asiwe na sababu. Ndo maana uchaguzi kila mahali uwe wa kitaifa mpaka kata aliyeshindwa uchaguzi hawezi kukosa sababu haijawahi kutokea.
 
Huyo Sumaye ni mwanaccm aliye mapumzikoni cdm, amezoea ushindi wa mteremko huko ccm wa kupita bila kupingwa. Sasa kaingia kwenye mazingira hata ukiwa mwenyewe lazima kura zipigwe, na watu wamemkataa anaanza siasa na utetezi wa kuccm. Arudi ccm haraka akafanye siasa za mbeleko na hila. Eti anasema watu wamekwenda kuhamasisha, sasa kwenye siasa alitarajia kusiwe na kuhamasishana? Kosa ni kufanya ukatili, uhayawani na wizi wa kura, sio watu kuhamasishana ww usichaguliwe.
Unajua sikuwa najua kama Mbowe ni hatari namna hii. Du... hawa ndiyo wanasema wapewe nchi? Magufuli kanyaga twende. Piga mpaka wachakae wafanyabiashra hao...
 
Ndio maana baada ya sarakasi kwa Dr Slaa niliamua kuwa huru ili nione mambo kwa uhalisia badala ya ushabiki. Chadema hakuna chama pale. Huyo Sumaye soon anarudi alikotoka! Msishangae Lissu pia akafanya maamuzi ya kuwashangaza! Asirudi CCM lakini atatoa picha kamili. Kuna kakikundi kameihodhi Chadema na ni untouchable!
Wahenga wanasema hivi " Usiku huwezi kuona mwanga mpaka uwashe taa" Kwahiyo na Mze Sumaye ndo kaona mwanga baada ya kuwasha taa.
 
ukawa2020,
Kwakweli hapa CHADEMA wamekosea sana. Kama mgombea alikuwa peke yake kulikuwa na haja gani ya kupiga kura?? Alikuwa peke yake hakuwa na upinzani hivyo alipata bila kupingwa. Kama mnafanya hivi, mtaaminika VP kwa wananchi kuwa chama inafuata demokrasia?? Mngemwacha Sumaye awe mwenyekiti na angeendelea kugombea nafasi ya uenyekiti sanduku la kura ingeamua. Nafikiri kuna watu wamelupwa kufanya yote haya ili chama ionekane haifuati demokrasia. mmekosea sana na hakuna njia ya kuirekebisha. Mmeigawa chama
Mawazo ya kijani haya. Apite bila kupingwa ndio mdudu gani huyo? Sasa kuna ubaya gani kama kapigiwa kura za ndio na hapana? Hiyo ndio demokrasia. Yaani ulitaka apewe tu uenyekiti kwenye sahani?
 
Unajua sikuwa najua kama Mbowe ni hatari namna hii. Du... hawa ndiyo wanasema wapewe nchi? Magufuli kanyaga twende. Piga mpaka wachakae wafanyabiashra hao...

Hapo unaona umepiga bonge la propaganda, ungesema kura zimeibiwa au siku ya uchaguzi kulikuwa na machafuko ningekuelewa. Sumaye kama alihonga kama alivyozoea huko ccm kuwa ukiwa mwenyewe unapita bila kupingwa, basi imekula kwake. Hiyo ndio demokrasia, akiona vipi arejee ccm akaendelee na siasa za mbeleko na kupita bila kupingwa.
 
Ndio maana baada ya sarakasi kwa Dr Slaa niliamua kuwa huru ili nione mambo kwa uhalisia badala ya ushabiki. Chadema hakuna chama pale. Huyo Sumaye soon anarudi alikotoka! Msishangae Lissu pia akafanya maamuzi ya kuwashangaza! Asirudi CCM lakini atatoa picha kamili. Kuna kakikundi kameihodhi Chadema na ni untouchable!

Sumaye anaweza kurudi alipotoka maana hata mpaka sasa hana tija yoyote. Hata Lissu akipenda anaweza kwenda anapotaka hiyo ni haki yake, na ukiona hajahama una kwenda kumshawishi ahame, lakini Sumaye kashindwa kwa uchaguzi uliokuwa wa haki. Labda kama mnataka tuamini ukiwa mwenyewe basi una haki ya kushinda.

Kama ww ulihama cdm hiyo ni haki yako na hakuna anayejali, ila usitake kuleta hasira zako kwa upotoshaji wa Sumaye kushindwa. Labda utuambie kwenye huo uchaguzi kulikuwa na machafuko, au box la kura lilitolewa nje ya chumba cha kupigia kura na kwenda kutoa za Sumaye.
 
Back
Top Bottom