Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mh.Sumaye jikaze,vumilia taratiibuu

umeshaamua kuwa mpinzani,tulia apo hapo kama unanyolewa

Kwani ulifuata uenyekiti wao? Si in uwaziri Mkuu!? Si ndioo

Pole sana Mh...

..ila waliokuita Mr Zero sio watu wazuri...yaani from hero to zero INA kuhu

Mdogo wangu acha tabia hizo au hujui ni Waziri mkuu mstaafu na anasoma hapa
 
IMG_1512.jpg
 
Laana ya Dr Slaa ni Kali na sasa hivi imeongezeka laana ya Sumaye tena.

Chadema kwisha kabisa
Mimi nadhani apa ndiyo Demokrasia... Kwani mpaka ashinde yeye? Bora imepigiwa kura ,je CCM nani atachukua fomu ya uwenyekiti mwakani?
 
Yaani Suma Lee, ex Prime Mini ulikuali kuingizwa mkenge na watoto wa mjini? Sasa ndio utajua 'the meaning of DISCO JOKERS' Na kwa hotuba yake leo utaingia KING tu. "TUNAKUHITAJI" Maadamu useme Uenyekiti huuhitaji😅😅😅
 
utaratibu wa ccm vs kupewa adhabu kwa kugombea kiti cha boss..

Ikiwa ni utaratibu haina noma.
Ila ikiwa kuna kushugulikiwa hapo demokrashia iko chooni.
Mimi nadhani apa ndiyo Demokrasia... Kwani mpaka ashinde yeye? Bora imepigiwa kura ,je CCM nani atachukua fomu ya uwenyekiti mwakani?
 
Hivi kweli uzoefu wote alionao Sumaye hajui kuwa uchaguzi una matokeo ya kushinda na kushindwa?
Wajumbe wametumia haki yao kumkataa mgombea pekee.
 
Amuulize member Na uenyekiti Wa ccm.sumaye anatafuta uongozi kwa nguvu
 
Mbona umechukia sana? Kumbe mnahubiri ambavyo nyinyi wenyewe hamuwezi kufanya? How convenience to Bring JPM on the subject? Mnafikiri kuongoza nchi ni sawa na kuongoza sacos ya CHADEMA? Mmekaa kuongea mambo ambayo mengi yamejaa majungu na uzandiki tena wengi kwa majina ya bandia. Kama nyie wanaume/wanamama wa shoka tuanze hapa kuweka majina yetu halisi.

Mbowe huyu alikuja hapa kujinadi kabla ya kuinunua JF kwamba tutumie majina yetu ya kweli, akaanza yeye mwenyewe baada ya wiki moja akakimbia na hajarudi tena. (I mean yumo humu kwa jina lake la ... .... ... (kapuni) maana anafahamu hawezi kufanya kile ambacho anahubiri.
Nalifahamu hilo jina analotumia.
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Cdm wameshabadili Uongozi ngazi mbalimbali wakawaweka akina mashinji, kwa maslahi ya kisiasa ya kubadili Sura lakini nafasi hizo zimeonyesha kUPwaya hadi sasa.

Nafasi aliyonayo Mbowe; inaweza kumgharimu Maisha yake,Mali zake binafsi kwasababu ya misimamo kama ya Bob Wine.

Ukimuweka mtu ndumila kuwili. CC wakigundua, lazima watawachezesha sindimba. Mbowe ni aina ya viongozi bora wasioyumba na waerevu sana katika siasa na katika kuchagua maneno ya kusema. Ni mwana diplomasiia wa aina yake.
Mbowe Bado ana uwezo wa kuongoza Chama Katika siasa za kistaarabu na hizi zilizoandamwa na Vurugu na mauaji. Mnyonge mnyongeni. Haki yake mpeni.

Demokrasia pekee haifanyi uweze kuchagua kiongozi bora. Wako madikteta kama Morsi wa Egypt, Adolf Hitler, ambao walichaguliwa kwa demokrasia tena kwa popular votes.

Ni Lazima akili kubwa itumike na management, kutoa elimu kwa wanachama ili wakifanya maamuzi wasiendeshwe na hisia na mihemuko bali uhalisia uliopo sasa.

Mbowe ni kichwa kinachohofiwa na hadi na HQ ya CC pale Lumumba.

Sishangai wana Lumumba, wakishiriki ku-vote ili wamtoe kama wanavyounga mkono chokochoko.

Na akitoka watashehereka kua wana CDM hawamtaki Mbowe na wamemchoka.

Lakini wao, wanajua kabisa MwenyeKiti wao hawamtaki lakini hawawezi kumtoa kwa domokrasi, kwa sababu wanamuogopa kama ukoma. Siasa imejaa Unafiki.

Hata Sijajua hata kwanini Nimejiingiza hapa kujadili maigizo haya.....


Bora wala usingeingia kujadili kwenye huu uzi kuhusu hiyo nafasi ya Mbowe maana utaishia kukwazika. Hizo sifa zote uliposema kuhusu Mbowe acha tuzikubali hata kama sio zote za kweli. Lakini ufahamu cdm ni taasisi, hapa ulipo ni kama unajidhalilisha na kudhalilisha cdm taasisi kwamba hakuna mtu anaweza kuwa mwenyekiti zaidi ya Mbowe. Kiongozi makini na asiyeyumba anaweza kuokoteza mgombea wa urais miezi miwili kabla ya uchaguzi!? Kibaya zaidi mgombea mwenyewe sio lolote sio chochote, hata hivi tunavyoongea karudi huko huko alikotoka. Dhambi hiyo hiyo ya kuokoteza ndio imefanya cdm ikimbiwe na viongozi kurudi ccm kwa kauli ya kwenda kuunga mkono juhudi.

Tuwe wakweli bila kujali unakubali au unakataa, faida za Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm ni chache kuliko hasara. Kiongozi kakaa madarakani miaka 15 ameshindwa hata kuandaa utaratibu wa kupata kiongozi wa kumrithi huyo ni kiongozi imara kweli? Kiongozi amekaa madarakani zaidi ya miaka 15 hata kujenga ofisi yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani kashindwa, huo uimara uko wapi? Tunataka Mbowe akae pembeni, sio kwamba hakuwa na mazuri yake, bali tunataka sasa aingie mtu mwingine afanyie kazi mapungufu yake, yeye hapo alipo ni so outdated hana jipya analoweza kutoa kwa sasa. Cdm ni taasisi sio kundi la wahuni wanaomsujudia Mbowe.
 
Sumaye ndio kasema.... na ndio muathirika wa udikteta wa chadema...

Unanionea mimi bure tu bro..

Sumaye ni nani, huyo ni shushu wa ccm ndani ya cdm. Kapigwa chini kwenye chama anatafuta sababu za kuokoteza, kwenye huo uchaguzi kulikuwa na fujo? Box la kura lilitolewa nje ya kituo kwenda kuwekwa kura za kumpinga? Aondoke haraka sana cdm, huko cdm hatumuhitaji kiongozi aliyechoka kiumri, kimawazo na pia hana mvuto kabisa kisiasa. Akamalizie uzee wake huko alikolia ujana wake. Sijui hata cdm walitokana wapi na hayo mazee matapeli ya siasa za kichovu toka ccm. Alaamiwe Mbowe na genge lake kwa kuchukua hela ya lile zee jingine tapeli la kisiasa, na kumpa nafasi ya kugombea urais hadi saa hii haiba ya cdm imechafuka.
 
Mzee Sumaye

Siasa za Afrika unazijua kwa undani? Hilo unalolizungumzia huko kwenu CHADEMA ndilo pia lipo kule ulipotoka CCM na hata ukienda kwa Museveni utalikuta.

Jambo jema kwako ulitakiwa kusoma alama za nyakati, ungepumzika kwa heshima kama mwenzako Lowassa, bado hujachelewa rudi nyumbani tunakusubiri.
 
Back
Top Bottom