Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

Mzee Sumaye: Niliambiwa mapema ndani ya Chama chetu hakuna Demokrasia, ukigusa uenyekiti wa Mbowe utashughulikiwa

kwahiyo mlitaka iwe kama ccm,kama hakuna aliyechukua fomu basi ni kupita bila kupingwa hata kama wanachama hawamtaki?
Ni nani alimshauri Mzee Sumaye kuhamia CHADEMA?

Hakujua kuwa CHADEMA ina mwenyewe? Ninapatwa na wasiwasi kuhusu IQ yake!

Unamtingisha Mbowe halafu unategemea kubaki na cheo ndani ya chama chake! Thubutu!

Ninamuhurumia sana huyu Mzee!

Baada ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA kuna uwezekano wa kufukuzwa au kuondoka CHADEMA hasa ikichukuliwa kuwa amechukua fomu kupambana na Mbowe katika kiti cha Mwenyekiti Taifa!
 
Mimi ni miongoni mwa watu waliosikitishwa na Sumaye kuukosa uongozi wa Kanda ya Pwani kwa mara ya nyingine , bali naheshimu maamuzi ya wengi , sometimes mabadiliko hayakwepeki hasa kwa sababu ya aina ya siasa zinazofanyika kwenye awamu ya 5 .

Awamu hii inahitaji kuwa na kiongozi wa kanda ambaye ni Kijana mwenye uwezo wa kijasiri wa kupambana na hujuma zote , hata kwa kutumia ubabe ikibidi , wakati wa siasa za kistaarabu umekwisha , tunapochagua viongozi wa kanda hili lazima liangaliwe.

Bali kutokana na uzoefu wake wa uongozi , Sumaye achukuliwe kwenye kitengo cha ushauri , asiachwe tu , anao uzoefu mkubwa sana kwenye siasa za nchi hii , Uzee ni hazina .
 
hayo maigizo CHADEMA mnayoigiza yana gharama kubwa sana.MTU alikuwa pekee yake Leo unadai kashindwa, aibu gani hiyo mnatuletea? huo ni uchafuzi
 
Kati ya mawaziri wakuu ambao walikuwa hawapandi kwangu ni huyu sumaye na sokoine,
lakini sumaye ametokea kuwa mtu mwenye busara na msimamo thabiti
Inasemekana sokoine alikuwa moto zaidi ya nyerere
 
Sababu ya kukatwa Sumaye ni analogy (Mfanano) na yaliyowahi nitokea.

Naomba niongee katika analogy na hakika utaelewa kwanini Sumaye amekatwa.

Niliwahi kuwa katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais UDSM, ila makundi ambayo yalikuwa hayaelewani na hayataki mtu wa pande mwingine ashinde ni CCM na Chadema.

Chadema waliandaa watu wao na CCM waliandaa watu wao kugombea Urais na wazi CCM ndio ilikuwa na wajumbe wengi wanaopitisha wagombea katika screening.

Sasa shida mimi sikuwa Chadema wala CCM ila angalau nilikuwa na nguvu kwa umma wa wanafunzi chuoni.

Wajumbe wa Chadema waliniahidi kunipitisha kuliko kumpitisha wa CCM,pia wajumbe wenyeitikadi ya CCM walijua mimi sipo Chadema hivyo waliahidi bora wanipitishe mimi kuliko wagombea wa Chadema ingawa sikuomba msaada wao, walitaka wenyewe kunipitisha wakihisi wangeweza kuniweka upande wao sababu nilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Kwangu mimi hii ilikuwa safe position, ni sawa na Sumaye alivyoachiwa kusimama peke yake sababu anaheshimika,hivyo alikuwa katika safe position sababu kura ilikuwa ni NDIO au HAPANA, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda sababu tayari walimpa imani ndio maana hakuna aliyeshindana naye.

Turudi kwangu sasa baada ya mimi kujua nina safe position ya wajumbe wenyeitikadi ya vyama vyote.

Siku moja kabla ya screening saa moja jioni nikiwa napita maeneo ya Extension (Hall one) nikitokea Cafeteria nikakutana na Charles William huyu alikuwa mwana mikakati mzuri wa chaguzi hizi, pia mwanachama wa Chadema ndio alikuwa mtu anayeogopwa sana na UVCCM UDSM.

Nilipokutana naye tulisalimiana tu kama dakika 3, kumbe kuna viongozi wa UVCCM wakina Ngassa waliniona, wakasema hee Nondo kumbe yupo na watu wa Chaso (Chadema) hawa maadui zetu.

Kikao kikafanyika usiku usiku kuwapa taarifa wajumbe kuwa Nondo ambaye tulisema tutampa kura sababu yeye sio Chadema tumemkuta anaongea na yule bwana Mipango wa upande wa Chadema, hivyo nendeni kesho jina la Abdul Nondo apewe zero anawezekana anatufanyia mchezo ili baadaye akishapita atugeuke.

Hii ndio iliyotokea kwa Sumaye kukatwa.

Sasa hapa kuna mambo 2 .

1. Kama makisio na dhana yao ya mimi kuungana na Chadema (Chaso) dhidi ya UVCCM - UDSM yalikuwa sahihi na yenye ushahidi basi UVCCM - UDSM walikuwa sahihi kunikata kwa maslahi yao binafsi na tawi la chama chao.

2. Kama makisio ya mimi kuungana na Chadema (Chaso) dhidi ya UVCCM - UDSM hayakuwa sahihi na hayakuwa na ushahidi wowote, walinikosea sana kwa kuninyima kura sababu tu ya dhana.

Na hakika walinikosea sana, sababu walinikata kwa dhana kisa mimi kuongea na tu na Charles William mambo tofauti na sio waliyokuwa wakidhani.

Hii nilihadithiwa na aliyekuwa mwenyekiti UVCCM - UDSM Ndugu Ngassa baadaye sana baada ya uchaguzi kupita.

Ila mimi ninashauri kama yaliyotokea ni dhana tu dhidi Sumaye basi Sumaye arudi katika kinyang'anyiro tena, uchaguzi ukiitwa. Kama sio dhana ni kweli na kuna ushahidi basi Mh.Sumaye aepuke hayo makosa madogo madogo. Pia arudishe imani kwa hao wajumbe.

Mwisho, haya wananchi hawayajui wao wanajua Mh.Sumaye ameshindwa hivyo hana uwezo. Njia bora izidi kuangaliwa katika utatuzi wa masuala kama haya ili kukiacha chama imara bila manunguniko.

Abdul Nondo
 
....kwani Sumaye ana kinga gani ya kikatiba au vinginevyo mpaka iwe lazima ashinde uchaguzi?, kashindwa sababu hapo kuna option tatu, kushinda, kushindwa, au kufanana kwa idadi ya kura, yeye kashindwa. Hamna maana kusema ukigombea peke yako lazima ushinde, no way!.

.... na wewe huko UDSM ulitumia nafasi ya kutokuwa na upande ukadhani ndio utashinda kirahisi, kumbe hukukumbuka side effects za kuwa peke yako, moja wapo ndio hiyo, ukionekana umefanya jambo lolote,likatafsirika vibaya upande wa pili ujue huna mtetezi, unapotezwa km ulivyopotezwa. Zaidi nakuona km mtu uliejiamini lazima ushinde, coz una kura toka pande mbili zinazohasimiana, ukasahau hata kushindwa kupo na ndio matokeo pia, unalia lia hapa ulikosewa, wala hukukosewa na yeyote.
 
Uchaguzi uliofanyija Jioni hii Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani, Chadema umekanilika

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye Peke yake ndipo zikapigwa kura za Ndio au hapana

Matokeo: Kura za Ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48

Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi!
Huwa nayaelewa sana maneno ya Paschal Mayala
 
Sababu ni Mfalme mbowe a.k.a Mugabe a.k.a Museveni a.k.a Nkurunziza kaguswa


Majibu yake rasmi kapitie pitie wapinzani wa hao viongozi yanawakutaga nn ndo utajua.


CHADEMA NI GENGE LA WAPIGA HELA,WATAKUFINYANGA FINYANGA UTAPOINGILIA MASLAHI YA MATUMBO YAO.
 
Back
Top Bottom