Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

Kishakusanya za kutosha kwa miaka mingi, sasa ndiyo anagundua kama ni dhambi. Arudishe basi na pesa zote alizopata alipokuwa akitenda dhambi ya kuimba nyimbo mbali mbali za taarab.
Hapo chacha, sijui na wake zake wataacha kuimba
 
Hahahaaaaaa
Dah! Haya maisha bhana!
Eti Mtu akishapiga Maisha akafungua Miradi mbali mbali yakumuingizia Kipato ndipo anapomrudia Mola!

Hapa kitaani kwetu kuna jamaa alikuwa mfanyabiashara ya Madawa ya Kulevya miaka (9) mingi kinoma akajenga Majumba 4 yakupangisha plus Guest 3
Then hivi majuzi naye kasema Amemrudia Mola hivyo hafanyi tena Biashara haramu.

Allah anasema "TUBU INNALLAH TAUBAT NASUA"

Yani "fanya toba ya kweli na usirudiye makosa yako"

Hakusema piga kazi haram upate pesa za kutosha halafu ufunguwe Miradi mingi ikuingizie Pesa ndipo "UFANYE TOBA"
 

Haswaa umenena mkuu mashauzi ndie anayeendelea kuuharibu anaimba rhumba anasema ni taarab
halaf viguo anavyovaa kwenye taarab hadi hasira anavaa vinguo ambavyo ni.kinyume na maadili
 
Huyu Mungu anayefuatwa mpaka pale tu Mtu anapojisikia kufanya hivyo, yupo kweli?
 
Wiki 2 zilizopita nilienda magomeni alikuwa hayupo ila nyimbo zake kuna muimbaji mwengine aliimba sauti zao zimefanana.na alikuja late akaimba baadae akaondoka.kumbe mzee ameshajitoa.kwa hiyo jahazi itakuwa basi tena
 
Reactions: BAK
Hujaambiwa muziki ni haramu ila kile ukitoacho kwa kupitia muziki ndicho haramu,Je una uhakika Mungu alitoa vipaji vya mziki,unasoma wapi au umepata wapi hili
Tunaposema Mungu ni muumba wa vyote ina maana vipaji vya mziki havihusiki?
 
Niulize mara ngapi?

Kasoma nyakati, kupiga shoo moja 2,000,000 sasa hivi atapata wapi wakati FM Academia wanapiga bonanza la bure Toroka uje?
Mkuu ilisemekana ile ajali ya five star miaka ile iliyoua wasanii wengi yeye ndio aliitengeneza kwa hofu ya kufunikwa na marehemu ISSA KIJOTI aliefariki kwenye ajali hiyo maana marehemu alikuwa anakuja juu sana kisanii. Na hili lilipelekea Mzee kukataa kushiriki wimbo uliotungwa na wasnii wa taarab wa kumuenzi marehemu Issa.
 
Hapa kwenye dini hii yetu ni shida tu, kila uapande una dhambi yao, wengine kuburuza nguo kwa mwanamke na mwanaume kuvaa kipensi nndio sawa, wengine kuvaa suruali ndefu na wanawake kuvaa nguo ndefu zisizo buruza chini ndio sawa, wengine kufunika nyuso ndio dini wengine kuacha uso wazi wanja(suna) uonekane ndio sawa. Tafrani tupu. Eti gitaa ni dhambi ila ngoma ni halali haaaa. tafrani.
 
Bwana weeeee, unapomkataa shetani yakatae na mambo yake. Huwezi kuendelea kulamba fedha za trade mark ya shetani huku unajifanya ni wa Mungu.

Labda tu Mzee Yusufu angetoa angalizo kwa wafuasi wake kwamba 'alikuwa akifanya dhambi kwa hiyo nao waache'
 
Bwana weeeee, unapomkataa shetani yakatae na mambo yake. Huwezi kuendelea kulamba fedha za trade mark ya shetani huku unajifanya ni wa Mungu.

Labda tu Mzee Yusufu angetoa angalizo kwa wafuasi wake kwamba 'alikuwa akifanya dhambi kwa hiyo nao waache'
Tunaacha taratiiiibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…