Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Duh, wanne wote wamezalia nyumbani?
Dada wa Kwanzaa anawatoto wanne ,,wa pili wapo watoto wawili wa Tatu 3,,wa nne Ivo Ivo nilisha wahi wafukiza wamerudi tena wazazi wapo kimya so naona ntagombana na ndugu Kuna mdau kasema nihame ,,japo siishi nao Mimi Nina kwangu
 
Dada wa Kwanzaa anawatoto wanne ,,wa pili wapo watoto wawili wa Tatu 3,,wa nne Ivo Ivo nilisha wahi wafukiza wamerudi tena wazazi wapo kimya so naona ntagombana na ndugu Kuna mdau kasema nihame ,,japo siishi nao Mimi Nina kwangu

Yaani wazee wako wanaelea wajukuu 12? Pheeew! Hilo ni balaa kubwa asee, sina la kuongeza hapo.
 
Ni muhimu zaidi pia kuzuia makosa yasiendelee kufanyika, inasikitisha sana watoto kuzaa na kulea watoto wenzao. Hili ni jambo linalozidi kuongeza utegemezi na umaskini mkubwa katika nchi.
😟😟Unakuta vitoto kwa bibi wala hazina matunzo mazuri zaidi ya kula tu ...Shule haviendi na mavazi ndo tafarani kabisa
 
Aisee hii isikie kwa watu tu isikukute inauma sana basi tu ni wazazi hawana jinsi ila inauma na inaleta fedheha mnoo. Ifikie kipindi mabinti jamani wajielewe, muwapunguzie wazazi hii kitu, usomeshwe, utunzwe bado ulete mimba nyumbani aisee! 😡 !
 
Binti yangu hawezi kuzalia nyumbani wakati baba yake nipo! Hiyo haiwezekani! Na yeye anajua hilo. Nawaombeni wazee wenzangu kataeni ujinga huo wa mabinti kuzalia nyumbani, ni aibu! Wewe baba ambaye binti Yako anazalia nyumbani jitathimini, unapaswa kuwa mkali
Tema Mate Chini Mkuu.
 
Tatizo sio mtoto mmoja tuseme bahati mbaya.
Unakuta Mdada ana watoto wawili mpk watatu hapo kwao..
Familia Iko kimya
 
Kwa binti asiyejielewa lazima hili limkute au lisipo mkuta basi kachomoa mimba
 
Nimehamasika kuanzisha Uzi huu baada ya kusoma Uzi wa mdau analalamika dada zake wote wamezalia nyumbani.

Bila shaka atakuwa na uchungu juu ya Jambo hili na ndivyo ilivyo kwa wazazi wengi wanaolea binti zao na mwisho kupewa majukumu mengine ya kulea wajukuu.

Hili ni tatizo kubwa kwasasa wanawake wanapaswa kujitambua na kujua nyakati zimebadilika na suala la malezi ni jukumu zito. Msichana usipo jitambua ni mzigo kwa wazazi wako.

Naandika haya nikiwa Kama mzazi wakiume. Ninyi mabinti ninani aliyewaloga? Hata hivyo serikali inalojukumu la kuanzisha kampeni za uzazi wa mpango kunusuru mabinti na uchumi wao na wazazi wao
Alafu maisha jinsi yalivyo ya ajabu,hao mabinti wakiwa ndani ya ndoa kushika mimba inakuwa kasheshe ila hawa ambao hawajaolewa hawa basi inakuwa ni shida balaa ukigusa tu basi walete.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom