Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Si mnahamasisha vijana wakatae ndoa jamani Ndio madhara hayo
 
Wazazi wanapenda kulewa wajukuu kutoka kwa watoto wao wakiume tena wanafurahi sana na wanawachagulia majina ya kuwaita wajukuu zao, tena utasikia huyu mjukuu wangu namuita jina la Babu yangu mzaa mama au mzaa Baba tena laki Mira.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo mzigo ni kwa watoto wa upande wa kike tu!!!
Basi sawa.
 
Wanazalishwa mno bila mpango, bila malengo, unakuta binti wa miaka 24 tayari ana watoto wa 3 baba tofauti. Ok wakwanza basi tumsamehe tuelewe ilikua bahati mbaya ila wapili na watatu 🥺 hapana kwa kweli
Hapo hamna tena cha bahati mbaya hivi huwa hawajui zile siku za hatari kupata mimba kweli
 
Ndio imekua hivyo tena wanawapigia chapuo na pesa za wajukuu anatoa kutoka kwenye malipo yake ya kiinua mgongo ili wajukuu wasife na njaa mama kakaa tu watoto wanalishwa na Bibi na Babu wakati baba zao wapo
Lakini hiyo tabia inategemea na kabila gani kuna baadhi ya makabila binti akishazalishwa bila ndoa au akaachwa na mume harusiwi kukanyaga kwao tena anafukuzwa yeye atakua pakwenda, yani afadhali binti awe ameachana na mume kidogo kidogo kaka zake wanaweza kumnunulia eneo wakamjengea akaishi, yani mfano kabila la wakurya mwanamke ukishaolewa tu ujue ulipo olewa ndiyo kwenu uko yani mali za wazazi wako huwezi kurithi ata kama wazazi wameacha mali nyingi kiasi gani mtoto wakike hurusuwi kurithi mali za wazazi wako, wanarithi ni watoto wakiume tu, Mwanamke anarithi Mali za mume wake na siyo mali za wazazi wake.

Sasa wengine huko nyanda za chini kusini na huko Pwani hawana tamaduni hizo wao ni kuzalishwa na urithi wanataka wale wajukuu wapewe wakati baba hawajulikane yaan wajukuu ndio wanakula pension za wazee na hapo bado hawajasomeshwa kwa pension za wazee na urithi wapewe binti yupo tu nyumban,
 
Mi nadhan tukubali mapema watoto wa kike kuwa na boyfriend mmoja kama wazungu
Mtoto wa kike akienda hata sokon unapata mawazo
 
Mkuu hili limekuwa tatizo sugu mabinti hawajui tu ni wazazi Huwa wanapatwa na aibu sana mwanae azalie nyumbani tunatakiwa kusimamia pia maadili ya kiimani na maadili ya kiafrika ila ni kazi nzito ila Haina namna

Upande wa pili wanawake wanadai kuwa ndoa ni mzigo hivyo wanatafta wa kuzaa nae then aendelee kuwa huru , na vijana wa kiume wakidai ndoa ni utumwa kataa ndoa mwisho wake ni nini

Mungu atunusuru
 
Mtihani sana siku hizi kisichana kipite miaka 15,16,17,18 bila kubeba ujauzito ni nadra sanaa

Yaani wanapata ujauzito kabla ya kuelewa ujauzito ni nini?

Cha ajabu wanapewa ujauzito na watu wazima yaani wamewapita kupitiliza.
 
Wanazalishwa mno bila mpango, bila malengo, unakuta binti wa miaka 24 tayari ana watoto wa 3 baba tofauti. Ok wakwanza basi tumsamehe tuelewe ilikua bahati mbaya ila wapili na watatu [emoji3064] hapana kwa kweli

Mabint waruhusiwe kuwa na boyfriend tatizo vijana wa kiume uwiii Ndio itakuwa umemkabidhi chakula
 
Back
Top Bottom