Mzungu kasahau kipochi chenye pete. Hivi zinaweza kuwa na thamani gani?

Mzungu kasahau kipochi chenye pete. Hivi zinaweza kuwa na thamani gani?

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Sasa mkuu unaomba wasirudi au??


Ushauri mzuri nenda kwa sonara zunguka hata sonara watatu waambie unauza hizp pete alafu sikia watakwambia sh ngapi
Yaa nakaa one week baada ya kupeleka namba na taarifa.
Baada ya hapo nafanya uwezekano wa kuziuza
 
Watu wote waliowahi kuokota kitu cha thamani wakarudisha walishakufa masikini kwa msongo wa mawazo. We uliza bei ikiwa nzuri uza. Ikiwa bei yakipuuzi rudisha mgahawani tembea mbele. Siyo urudishe kitu cha pesa ambayo utaipata kwenye kinua mgongo cha kazini kwako kizembe. Maisha yatakupiga mpaka utazikumbuka.

Baada ya kuuza niombe namba unitumie hata ten ili tugawane hayo majini. Tambua uchawi hauendi kwa mentali na dawa ya jini ni gunia la bange
Naunga mkonyo hoja, yani mi niwe nimepigika niokote kitu kina thamani eti nirudishe? Mtaniua
 
Ukilkota kitu poleka polisi ndio sheria inavyosema kitendo cha kuendelea kukaa nacho kinatengeneza nia ya wizi ( implied mens rea) ile methali ya kiswahili ya cha kuokota sii cha kuiba imekosewa na haifai kuwa katika vitabu vya kiada.

Umiliki hauwezi kuwa wako huruhusiwi kukifanyia kitu chochote wala kumpa mtu yoyote kama zawadi au kuuza( NEMO DAT QUOD NON HABET)

Sheria inasema ukiokota kitu chochote cha thamani peleka polisi maelezo yako ya kuokota yataandikwa kwenye kitabu kiitwacho LOSS AND FOUND PROPERTY REGISTER) na utapewa namba ya taarifa ( kibongobongo RB)

Sheria inahitaji kitu hicho kurndelea kuhifadhiwa kwa kipindi fulani cha muda , na baadaye kama mwenye mali hajajitikeza mali hiyo itatangazwa kuuzwa kwa mnada basda ya kutolewa amri ya mahakama. Fedha iliyopatikana mwokotaji atapewa asilimia fulani

Kuna madhara makubwa ya mtu kuokota kitu na kujimilikishia kwani vitu vingi huibiwa na kutupwa au vielelezo mbalimbali vya kesi za mauaji hutupwa. Sasa wewe ukikamatwa nacho na kiliibiwa au kutumika kwenye uhalifu baden of proof (onus probandus) itahamia kwako uonyeshe uhalali wa umiliki wake tofauti na hivyo mahakama itakuchukulia kama wewe ndio uliofanya kosa kama mauaji au wizi ( DOCTRINE OF RESENT POSSESSION)
 
Duuu
Zamani wenzako nao walikuwa wanasema wamepata ajali na wazungu wakaokota madini hawajui thamani yake!!!🤣🤣
Peleka polisi watakusaidia
H kitambo hii mambo🤣🤣 apeleke polisi tu watamsaidia kujua thamani🤣😃😃
 
Bei sh ngapi umepata????
Sijui ndugu, ila Leo naenda kutoa taarifa pale kiungwana, ukute walirudi kuulizia, wiki moja ikipita itabidi tu niviuze, unaweza kuta ni mtu mwingine alidondosha na sio wale wazungu niliokuwa nawadhania
 
Mkuu hizo pete ni za majini aseh, haiwezekani ktk comments zote hakuna hata mmoja aliyeulizia picha.
 
Duuu

H kitambo hii mambo🤣🤣 apeleke polisi tu watamsaidia kujua thamani🤣😃😃
halafu aliyeokota anajifanya mshamba hajui kitu anaomba msaada
 
Mkuu hizo pete ni za majini aseh, haiwezekani ktk comments zote hakuna hata mmoja aliyeulizia picha.
Picha imebidi nizifute maana nimebadili mawazo kulingana na ushauri niliopewa na wadau humu
 
Sijui ndugu, ila Leo naenda kutoa taarifa pale kiungwana, ukute walirudi kuulizia, wiki moja ikipita itabidi tu niviuze, unaweza kuta ni mtu mwingine alidondosha na sio wale wazungu niliokuwa nawadhania
Jua thamani yake kwanza unaweza kuta ni pete za machinga
 
Jua thamani yake kwanza unaweza kuta ni pete za machinga
Sio pete za machinga ndugu, hizi lazima zitakuwa na thamani fulani, hata kama sio kubwa. Ni pete ambazo watanzania wengi hawawezi miliki.
 
Nenda ukakabidhi hiyo pochi hapo mgahawani watarudi kuulizia mali yao hapo.
Huo ujinga ndio siwezi kufanya.
Nitatoa taarifa nimeokota kipochi kidogo basi
Sisemi kilichopo ndani
Mwenye navyo ndio itabidi anisanue ndani kunanini
 
Hawana shobo za kuvaa vitu expensive wakiwa barani kwetu,usishangae ukakuta hazifiki hata buku.
 
Back
Top Bottom