Na hii inasikitisha sana yaani unapewa adhabu kwa kuwa wewe umemsikiliza Mkeo

Na hii inasikitisha sana yaani unapewa adhabu kwa kuwa wewe umemsikiliza Mkeo

Sasa kama nyoka ndio maana yakw hivyo, kwanini muumbaji alipotoa laana ilikua ni laana ya nyoka kabisa huyu huyu nyoka sio dushe

Kwamba atajua adui wa binadamu, atamn'gata kisigino nae binadamu atamponda kichwani na mawe. Sasa mbona kalaaniwa kweli
Asiyejua maana hatoambiwa maana...
Kwani mtu akifumaniwa na mtu ambae hajahalalishwa nae hua wanatakaga kumfanya nini...
 
Sasa kama nyoka ndio maana yakw hivyo, kwanini muumbaji alipotoa laana ilikua ni laana ya nyoka kabisa huyu huyu nyoka sio dushe

Kwamba atajua adui wa binadamu, atamn'gata kisigino nae binadamu atamponda kichwani na mawe. Sasa mbona kalaaniwa kweli
Hahaha sio mchezo hii inatafakarisha sana
 
Masuali hayaepukiki mkuu, yaani kuna masuali tangia wadogo tunajiuliza mpaka leo tushakuwa watu wazima hatujapata majibu. Na mengine ndio hivyo ukiuliza sana unaambiwa unapata dhambi
Yaan acha kabisa mkuu ukijiuliza kosa na ukiuliza kosa pia yaan sasa wao watuambie tufanyaje hapo
 
Bado walikua wanasubirishwa kwanza mpaka muda sahihi...

Eva ndiyo akawahi kubalehe...
DDuuuh, wanawake kwa kweli tuna viherehere. Na nguvu ya ushawishi
Sasa Adam alivyokazana na Eva yeye bado alikuwa hajabalehe? Unataka kusema hakupizi?
 
Wakuu kuna kitu kinanitafakarisha sana yaani kila nikikaa natafakari sana.

Yaani Mwanaume ni marufuku kumsikiliza mkeo hilo kosa adhabu yake ni ya milele na ilikua imeanzishwa na Muumba Mwenyewe lakini ukiangalia kwa undani utagundua Mwanaume Adamu alionewa tu hakua na kosa lolote.

Hivi ebu turudini pale bustanini Adam alipokua anaishi na Mkewe Hawa au tumuite Eva. Huyu Hawa au Eva aliingia kwenye kurubuniwa na kajamaa kamoja kakamtongoza wakafanya ya kufanya huko machakani wakamalizana fresh kisha Bibie akapewa na katunda akachukua akapeleka kwa Mumewe Adamu.

Sasa ukifika hapo inabidi utulie kwanza maana huyu Bibie alipofika kwa Adamu hakuna sehemu Biblia au Kitabu kingine chochote kinasema kwamba Eva au Hawa alimwambia ndugu Adamu wapi alipolichuma hilo tunda au amepewa na nani. Kwa nilivyoelewa mimi na hata km ningekua mimi ndio Ndugu Adamu yeye alichojua ni kwamba huyu Hawa amechuma hilo tunda katika miti ambayo wameruhusiwa wachume.

Sasa kinachonipa tafakari zaidi ni Hakimu au Jaji anaekuja kuamua hio kesi ya Makatazo aliyoyaweka kwamba msifanye hivi. Ambae ni Mungu aliewaumba.

Ukiangalia kwa mujibu wa simulizi hio utaona Mungu anapokuja na kukuta mazingira hayapo yaan Adamu na Mkewe Hawa au Eva wamejificha Mungu anaanza kuuliza wapo wapi?

Mwanamke Hawa au Eva anakula buyu hajibu kitu ila kwa kua Adamu ndio Baba mwenye mji anaona bora aitike na kueleza kilichotokea kua amejificha kwa sababu yupo uchi. Mungu anauliza kwanini unasema upo uchi? Adamu anajibu huyu Mwanamke uliyeniletea ameleta tunda hapa nimekula ndio nikaanza kujiona nipo uchi.

Mungu akaanza kutoa adhabu kwa wote ila kuna kitu hapa mimi naona km hakikukaa sawa sababu kwa mujibu wa maelezo mimi naona Adamu hakua na kosa lolote. Kwanini nasema hakua na kosa kwa hio Mungu alimwambia Adamu kabla kwamba asimsikilize Hawa au Eva mkewe au hakumwambia hivyo?

Km hakumwambia Adamu kwamba asimsikilize Eva au Hawa kwanini anakuja kumuadhibu kwa kosa lisilokua la kwake? Kwanini Mungu aliamua kumuonea Adamu?

Kwanini Mungu alimtengenezea Adamu mtego wa Hawa au Eva kumuwekea Mwanamke pale bustanini ili tu amfukuze bustanini inamaana Mungu alimchoka Adamu?

Au ulikua mpango wa Mungu kuwafanya Adamu na Hawa waishi nje ya bustani ila namna ya kuwatoa ni kumtengenezea mtego Adamu na kumpa lawama zisizomuhusu na adhabu isiyomuhusu?

Kwa nilivyoona mimi kupitia kifungu hiki Adamu alionewa tu hakua na kosa lolote maana yeye wakati Eva au Hawa anatongozwa huko Machakani mpaka anatoa na kupewa tunda Adamu hakuwepo, sasa Mungu anamuadhibu vipi Adamu kwa kosa la kula tunda? Au anamuadhibu kwa kosa la kutohoji kwamba hili tunda wewe Mwanamke umelichuma kwenye mti gani? Badala yake yeye alichukua tu akalibugia bila kuuliza?

Hii inamaana kwamba Adamu alibeba kosa alilolifanya Hawa au Eva? Yaan aliadhibiwa kwa kosa lisilomuhusu?


Mwanzo 3:9-12

BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

Mwanzo 3:17-24

Kisha akamwambia huyo mwanamume,

“Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo, ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile; kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa. Kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako.

Ardhi itakuzalia michongoma na magugu, nawe itakubidi kula majani ya shambani. Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.”

Adamu akampa mkewe jina “Hawa”, kwani alikuwa mama wa binadamu wote.

Mwenyezi-Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!”

Basi, Mwenyezi-Mungu akamfukuza Adamu nje ya bustani ya Edeni, ili akailime ardhi ambamo alitwaliwa. Alimfukuza nje, na kuweka mlinzi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia iendayo kwenye mti wa uhai.

Nakaribisha maoni yenu nyinyi mnaonaje?
Dominika Njema.
NI sahihi wewe mwanaume umepewa sheria ambazo hutakiwi kuzivunja na tumeambiwa utoe elimu juu Hilo kwa MKEO kwamba hapaswi vunja sheria hizo




Sasa anavunja anakushirikisha na wewe unavunja.


Kama adamu asingevunja kwa kukubali kula tunda basi mke angepotezwa akaumbiwa mpya
 
Back
Top Bottom