Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Umeelewa swali la mtoa mada au umekurupuka tu uonekane umekitetea chama!? Kila mtu anajua chama ndicho chenye serikali ila issue hapa ni nguvu hizo za katibu itikati na uenezi anazitoa wapi? Je hayo ndo majukumu yake? Wapi katibu mkuu, wapi makamu mwenyekiti?
 
Nguvu za Mheshimiwa Makonda zinatoka kwa wananchi wanaoiunga mkono CCM na Serikali yake. Ndio hayo ni majukumu yake kabisa na hakuna alipokiuka .huyo ndiye msemaji mkuu wa chama kilichounda serikali iliyopo madarakani.

Kwa hiyo acha kukurupuka na kuropoka ropoka tu hapa ujinga wako.
 
🤣🤣🤣 shida ni ccm mkuu
 
Kama Samia alitaka mtu wa kusukuma utendaji wa kiserikali, angemteua katika cheo cha kiserikali kinachosimamia mawaziri, wakuu wa mikoa nk, kama Biteko. Hili la Makonda kujipa nguvu na kujiamini nakuhakikishia halikupangwa, huenda hata Samia anashangaa lakini hana la kusema
 
Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.
Hawa woote ni genge moja wamekuingiza Mkenge hii ni Movie yao na wao ndio Characters kila mtu anachez part yake.

Wasikuhadae na vsimu na vimaneno neno wanatoa mitandaoni.
Lao ni moja.

Failure yao ni moja hakuna wa kumkebehi mwenzake.
 
Makonda ziara zake kama amewakojolea Chadema🤣🤣

Mbumbumbu wa Chadema wanaweweseka
Kawakojolea Chadema? Umeona katika ziara hata moja Makonda kawapigia simu Chadema? Anawakojolea watu wake hao hao wa CCM, mawaziri, wakuu wa mikoa nk, anaowaamrisha kesho uwe hapa, bila kujua huyo mtu kesho anaweza kuwa na appointment na raisi. Ndio maana kuna mmoja alisema mimi huyu hawezi kabisa kuniamrisha, ambapo ni kama kusema huyu hawezi kabisa kunikojolea!

Makonda anachofanya katika ziara zake ni kuonyesha udhaifu wa serikali ya CCM katika kusimamia uongozi wa nchi na kutatua matatizo ya wananchi. Lakini ni watu wenye akili tu kama kina Ftama Karume wanaona hilo, sio watu kama wewe na wengine wanaoshabikia hizi ziara. Wao hawaoni tatizo bali wanaona Makonda anasuluhisha.

Yaani Makonda akipita Mwanza na kusikiliza watu wawili au wanne, anakuwa ametatua matatizo yote ya wananchi wa Mwanza ndio maana anaenda Shinyanga? Hivi watu mmesoma shule gani?
 

Kwamba mfumo wote huo ushindwe kufanya kazi, ila mtu mmoja anayepita siku 2 ndio amalize hayo matatizo uyasemayo?! Yaani ni sawa na kusema mtaani kwenu hakuna maji, na wanaopaswa kushughulikia upate hawawajibiki, kisha aje mmoja kati Yao akupe maji ya kunywa ww mwenyewe hapo mtaani, ndio uone huyo ni mtatua kero ya maji?

Kama kweli yeye ni mtatua kero, chama chake ndio Kiko madarakani aweke ni jinsi gani kero za wananchi wengine nchi nzima zitatuliwa, au Kila mwenye kero atamsubiri Hadi yeye amfikie?
 
Hii comment Mods naomba waiprint alafu waifanyie lamination kabisa

Mhariri
 

Hii nchi imefika hapa kutokana na aina ya watu wauelewa finyu kama wa huyo unayemjibu. Yaani hayo maigizo anaita utatuzi wa kero, na kibaya zaidi hata hao wanaosemwa kutatuliwa kero zao wanaandaliwa kwanza!
 
Nguvu ya Makonda iko kwenye ujinga wake. Namaanisha kuwa ni wale watu wajinga ambao unaweza kumwambia ''nenda kamzabe mama yako yako makofi'', na akaenda kufanya kweli. Kwa kifupi nataka kusema kuwa mwenyekiti amemchagua yeye kwa sababu anajua ni mjinga na yuko tayari kujitoa ufahamu afanye lolote bila kujali madhara yake. Hivi mtu mwenye akili zako unaweza kufanya ujinga anaofanya wa kudhalilisha watu na wakati kuna kesho? Hajiulizi kama Samia kesho hayupo ni nini kitampata? Kuna watu walikuwa wanasema baada ya kufa Magufuli basi atakuwa amejifunza, lakini ukweli ni kwamba ndiyo amezidisha. Tuombe Mungu uzima uje uone mwisho wake utakavyokuwa mbaya.
 
Unajua wewe ni mtu ninaemuona kibaraka mmoja wa kujipendekeza ambae anatafuta kila namna ya kujipendekeza kwa Samia na CCM yake angalau wakurushie ugali wa uteuzi wa namna fulani, lakini hata wao wamekudharau ndio maana hadi leo bado unahangaika na propagaganda zako na hakuna hata anaekujali.

Endelea, labda kuna siku kuna mjinga fulani atakukumbuka.

Sasa kama una akili kawaambie hao watu unaojikuwadi kwao kwamba wenye akili wanasema hivi, ziara na kujitutumua kwa Makonda hakusaidii bali kunabomoa CCM mbele ya watu wenye akili, na anasababisha migongano ndani ya chama na serikali. Kwa mfano, akimwamrisha waziri live mbele ya watu, aende mahali fulani, kumbe huyo mtu ana appointment na raisi, itakuwaje? Anamdhalilisha raisi mbele ya wateule wake, lakini hilo hamlioni nyie.

Kuna watu Makonda anawaumbua bila kuona kwamba anapofanya hivyo anamuumbua aliyewateua.

Makonda anachofanya katika ziara zake ni kuonyesha udhaifu wa serikali ya CCM katika kusimamia uongozi wa nchi na kutatua matatizo ya wananchi. NI watu semi-iliterate ambao wataona anatatua matatizo. Wewe kwa akili yako, Makonda akipita Mbeya na kusikiliza watu kumi siku hiyo, anakuwa ametatua matatizo ya wananchi wa Mbeya? Umesoma lakini wewe?

Mie ngoja nikuambie ukweli. Kinachowaangusha Chadema na kushindwa kuwaondoa CCM madarakani ni kwa sababu hadi leo Chadema hawajatambua wapiga kura wa Tanzania ni kama nilivyosema kwenye signature yangu hapa chini,

Usimdharau mjinga, mwelimishe. La sivyo atajikusanya na wajinga wenzake na watatumia nguvu yao ya wajinga wengi kukuchagulia mbunge au hata raisi mjinga kama wao .

na hii ni kutia ndani watu kama wewe Mwashambwa. Chadema wanapaswa kubadilika na kuongea na wajinga wa nchi hii katika lugha iliyo nyepesi mjinga kuelewa, kama wanavyofanya CCM, japo CCM hawafanyi kwa lengo la kuelimisha wajinga, bali kuwadumaza katika ujinga wao ili waendelee kuwa wajinga katika pindi za uchaguzi. Kuna watu tunajua hilo.
 
Haya ni mawazo ya watu wasio na upeo kwenye mambo ya uongozi wa nchi, wanaodhani kuwa nchi inaongozwa kama kijiji. Hivi huoni kuwa tatizo la Tanzania ni rais na wateule wake wote akiwemo huyo Makonda? Makonda atawasikiliza wangapi? Kwa nini usililie mfumo ambao matatizo yatatuliwa kuanzia ngazi za chini na hayasubiri mtu mmoja anayezunguka? Kweli kukosa akili ni hatari sana.
 
Ajabu sana kwa kweli, ila mkuu naona unajua au uelewa wako mpana kwa masuala haya
Pia linawezekana hilo
Tutaona mbio zake zitafika wapi maana ameanza kukimbia na jukwaa kama Luca alivyosema 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…