Ufahamu huo baki nao wewe...!
Mimi sio Mwana siasa...!
Kilichofanya Maghufuri apendwe na Raia wa kawaida wa nchii hii, ni kwa sababu alikua anawasikiliza, alichofanya Maghufuri hata kingefanywa na PM, baada ya Maghufuri kufariki, angepata nafasi mioyoni mwa wananchi masikini.
Nkizulumiwa kiwanja nikaenda Mahakani nikashindwa kesi, baadaye nikaja kuambiwa ukiendelea mbele, tutaitoa roho yako, then kesho kuna kiongozi akaja akanisikiliza, Nikarudishiwa Kiwanja changu, hayo mambo ya Sheria na utawala Bora yatanisaidia nini....!?
Kama nilipewa Tenda na Minispaa na leo ni maka 10 nawadai hawataki kunilipa, hakuna office sijawahi kwenda mpaka mkoani, na hakuna msaada, then Mkurugenzi ananambia coz unapeleka malalamiko mpaka kwa mkuu wa mkoa, basi hutokaa ulipwe.... Then kesho anakuja Kiongozi kama Maghufuri ama Makonda, ananisikiliza, anatoa amri nilipwe, na kweli kesho yake nalipwa.....! Aaah...! Hayo mambo ya Sheria na Utawala bora baki nayo kwenye makaratasi....!
Wananchi masikini wanataka mtu wa kuwasikiliza na kutatua changamoto!
Ukitaka ku win mioyo ya Masikini, Wasikilize then tatua changamoto zao.... Simple!
Otherwise njoo na mambo yako uone kama sisi masikini tutakuelewa.
Mfumo mzima wa utawala nchii hii ulishaferi, na Viongozi hawana mawazo ya maana, ndo utakumbuka mawazo ya Mwanasheria mkuu mbele ya Rais, mawazo yasio na tija yoyote, Viongozi wa umma hawatimizi majukumu yao....!
Ni bora twende hivi tunaenda, ndo maana natamani Makonda angekua hata PM kwa faida ya Masikini.