Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Hivi Ni visingizio vya dini... Kama kitu hakieleweki hakieleweki tu..hamna Cha kusema huwezi elewa, mbona vingine vinaeleweka. Walioandika hivyo vitabu wameandika hisia zao ndo maana kwa elimu na Sayansi ya saa hivi unaona mapungufu.
Real kabisa
 
Inaonekana unamuamini Mungu wa Spinoza, ambaye aliumba ila hajishughulishi na kilichomo ndani ya ulimwengu.
 
Bro mbona unachanganya habari nani aliyekuambia wewe una Majini?

Majini ni viumbe wa walioumbwa na Mungu kama wewe

Quran 15:26
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.

15:27
Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.


Wapo wachamungu wataenda peponi na wapo waovu wataenda Jahannam

Mungu anasema ameweka Jahannam Kwa ajili ya watu waovu na Majini waovu

Shida ni kwamba wewe ni mjinga Yani haujui kitu ila Kwa ujinga wako unajiona unajua Kila kitu

By the way haya ni maandiko ya kitabu Cha Mungu umezaliwa umeyakuta na utakufa utayaacha

Sasa kushindana na kitu kinachoishi milele alafu wewe ni mpita njia tu hapa duniani ni ujinga
 
Mkuu kuna hoja nimepata kwako.

Sina hakika kwa sababu sijasoma Bible yote maana ni kubwa pia.

Hivi ni kweli Hukumu ya moto (Jehanam) imeanza kuonekana kwenye Agano jipya tu kwenye agano la kale haijatajwa kabisa ee..!

Na vipi wanavyosemaga kuwa "Mbingu na Jehanam vyote viliumbwa pamoja tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu huu" ?
 
Unapinga hayo kwa hoja zipi
Uko google hata Mimi naweza kwenda kuandika

Kuwa wewe Ni kiumbe unayebishia spiritual being kwa kutumia human being logic au vp
 
Kwenye kuchagua vitu vya kusoma naungana na wewe, Wakristo wanachagua vitabu vya kujifunza zaidi huku vingine vinavyoonekana kuwa vigumu kufundishika wakivitelekeza.

Kitabu cha ufunuo wa yohana bhana, mimi nimefunzwa yale mafumbo nikayaelewa sawa kwa kiasi chake.

Lakini najiulizaga kwanini kitumie mafumbo kitabu kizima, na tafsi zake huwa wanazitoa wapi ? Maana kwenye Biblia hazijatafsiriwa.

Mfano UFUNUO ya yohana mla nilikuwa nafundishwa yule mnyama mwenye vichwa, vinne, sijui pembe kumi n.k.

Kwamba mle kuna Marekani, Roman Empire,Europian Union, Papa sijui ametwajwa ndiyo mpinga kristo.

Wewe haya yote tafsiri hizi umejuaje nawakati mle haijafafanuliwa ?
 
Ila brother naona we unahitajika kuzingatiwa.

Hoja zako zina-make sense, yaani zinamfanya mtu asiwe na maswali mengi kila unavyojibu, na nafikiri ni kutokana na uzito wa hoja zenyewe.

Unafaa kuzingatiwa wewe, hauifungi akili yako kwenye mwavuli wa dini.
 
Exactly ni yote mizimu, ila ya kwao eti wanaiita mitakatifu.
 
Swali langu kwako.

Kama aliyeasi alikuwa ni jini siyo malaika, ina maana malaika na majini wote walikuwepo mbinguni na walikuwa wamechangamana pamoja ?
 
Kusema kweli unaangalia na tabia za mataifa tajwa na wanyama/mafumbo yanayotajwa,
Papa sio mpinga Kristo ila Yuko ndani ya Circle ya kuandaa A New World Order ya kuongozwa na Mtu mmoja.
Kuna sehemu ile ya Babiloni Mkuu, nikujaribu kuangalia ile napata picha ya Taifa la Marekani pamoja na Ulaya wakiwa ndani ya Babiloni Mkuu, wao ndo wafadhili wa uchafu kama ushoga, usagaji na kubadili jinsia, plastic surgery na pia wanafadhili vita mbalimbali duniani.
Pia kitabu Cha Ufunuo kinaelezea kuanguka kwa Babiloni Mkuu, naona nilichukua pattern mbalimbali naona Taifa la Marekani litaanguka kuwa world super power huko mbeleni kupitia Vita Moja kuu itakayotokea duniani kote huku Urusi ikifanikiwa kuingia kwenye borders za Marekani .
Ufunuo wa Yohana 17:17-18
[17]Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
For God hath put in their hearts to fulfil his will, and to agree, and give their kingdom unto the beast, until the words of God shall be fulfilled.
[18]Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.
And the woman which thou sawest is that great city, which reigneth over the kings of the earth.

NA ILI MNYAMA AJE INABIDI UNITED STATES OF AMERICA AANGUKE
 
Kujiuliza swali la Mungu ni mkamilifu? Ni vizuri kuanza na wewe ni nini? Nini ni kinakufanya uwe kamili?
1. Mwili (The body) H.sapiens
2. Akili (Mind) Kipawa cha maamuzi.
3. Roho ( Spirit) Uhai
4. Utashi (The will) Shauku
Mwili ni kibebeo cha hivyo vitatu ambavyo kwa hali ya kawaida vyote havishikiki sio physical it an energy. Kila kimoja kibidamu kina udhaifu ambao bado hubebwa na mwili. Mungu hana mwili wa kibinadamu. Ukamifu wake upo kwenye Roho ambayo imeviongaza vingine vyote. Tuanzie hapo.
 
Sawa mkuu utanipa mrejesho... Tho ishu ya shetan n kwamba viumbe wenye akili malaika na wanadamu tuna utashi(free will) shetan na wazaz wetu wa kwanza waliamua kuasi...
Kuna meng ya kuandika mkuu..
 
Sijaingia deep sana kwenye uislam nijue, ndiyo maana nimekaa kukufatilia ili nijifunze kitu toka uislam, but kuna swali nimekuuliza ebu jaribu kupitia
 
Tufanye Binadamu tumweke pembeni maana yeye ana mwili.

Vipi kuhusu Lucifer na wenzake walioasi, maana wao ni roho pia (hawana mwili).
 
Nionyeshe evidence ya hao majini na sio kuleta kitabu Cha story.
 
Nieleze roho ni Nini na ikowapi. Maana wanasayansi wanasema hayo yote yapo kwenye ubongo Sasa we unayesema roho nielezee iko wapi.
 
Hahaha kwa Nini Hilo taifa lisiwe Roman empire, au uingereza kipindi Cha ukoloni ambao walichukua robo tatu ya dunia. Na kingine hivyo vitu unaviita ushafu Ni kwako na mwanzilishi sio marekani ye mwenyewe kavikuta vipo katika historia ya binadamu. Soma historia za empire mbalimbali utaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…