Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

"The universe does not carry debts. It always returns back to you what you gave it.” ―Drishti Bablani
 
Unafurahia usiyoyajua na huyajui yaliyomo. Makonda ni wa leo na kesho, naona anawachezesha kwata
Ni kweli Makonda anafanya spinning tu hakuna wa kumgusa.

Kwanza mpaka muda huu hakuna anayejua yuko wapi. Huenda yuko hata Huko Newziland anakula zake raha watu huku wanapayuka tu🤣
 
Tena kwa uandishi huu, uwezekano ni mkubwa kwamba hata kazi ya kubeba mafaili ya Lumumba huwezi kupewa!
Kuna wanaokemea huu ujinga wa watawala na bado wanaongoza kwa kula mema ya nchi hii. Kua uyaone siyo maghorofa!
Ww ni mjinga, umejaza sumu ambazo hata huelewi umelishwaje. nakupa tu pole
 
R.I.P Wilson Kabwe, former Mkurugenzi Wa Jiji la Dar...
Huyu mzee nae alikuwa mtu mbaya sana. Alitesa sana watu alipokuwa mkurugenzi jiji la mbeya kabla hajaamishiwa jiji la Mwanza.

Ndio maana alikufa kifo kibaya.
 
We naye pumbafu , jinga sana , Kwa hiyo yeye alivyoua , kutesa , kuteka , kudhulumu ,kudhalilisha , kunyanyasa na kuumiza hao watu alikuwa anafukiria nini au yeye anathamani Sana kuliko hao walioumizwa na ufedhuli wake huyo jibwa
Umemezeshwa sumu, kazi yako Ni kula tu hata akili huna.
Makonda kamuua nani? Kamtesa nani?
 
We acha tuu ndugu yangu. Haya mambo watu wanayachukulia powa, lakini Makonda aliumiza watu na wakaumia kweli kweli. Unajua kama janga halijakupata, siyo rahisi kuelewa.

Mimi siku zote najiweka kwenye viatu vya Lissu aliyotendewa na utawala wa mwendazake, najiuliza ningefanyaje? mpaka leo sina jibu. Mwenyezi Mungu atupe nguvu! Imagine mpaka watu wanafika sehemu ya kumsimanga Lissu kwamba ali-fake zile risasi? Imagine!

Napenda siasa. Lakini nachukia dhulma kwa nguvu zangu zote. Hawa wanasiasa wanaodhulumu haki za walalahoi watachomwa moto hapa hapa duniani! Karma is real!
Pia mimi nafikiria yule mwenda wazimu asingekufa taifa letu tungekuwa na Hali Gani?

Ilifikia kina masanja mkandamizaji kunadi wapinzani wasipite kwenye madaraja au barabara zilizojengwa awamu ya Tano.

Tushukuru mungu alisikia kilio chetu.

Hata mie ni muhanga was mwenda zake
 
hakuna wakumdhuru paul.na hakuna wa kumletea zengwe.paul ondoa shaka ,Kuna shuka limekuhifadhi,atakaye lifunua Basi atakacho kutananacho atarudi kuja kutuhadithia
 
Mku huu ushauri ni mzuri sana.
Ila kubwa zaidi awaombe Watanzania Msamaha huu utamsaidia sana kwani tulio na huruma ni wengi.
Aombe msamaha kama aliowahi kuomba Rais Moi hili asipolifanya ninaamini atakuja kujutia wakati huo yuko Jela au la japokuwa simwombei hili limkute kabisa kwani ameshajifunza kuendana na mazingira au anayoyapitia aliyekuwa Mku wa Wilaya ya Hai
Mzee baba kuomba msamaha ni kukiri kosa kuwa umefanya . Na Sheria haitambui huruma ...
 
Na wewe ukiwemo ulikuwa mpambe wake.

Leo unamgeuka jemedari wako?

Mbona mtakimbiana mwaka huu.

Bado kesi haijafika mahakamani

sikuwahi na sitawahi kuwa mpambe wa mtu..

ukifanya jambo sahihi nitakuunga mkono, ukienda alijojo nakupiga mawe pia..

mimi ni mpenzi wa sera za kikatili kwa watu wapumbavu, ila sishabikii tabia za hovyo kwenye jamii...Makonda kama Makonda kwenye utaratibu wa ubabe kwa watendaji na watu wapumbavu alikuwa sahihi... ila Makonda kama Makonda kwenye tabia zake binafsi na kulewa madaraka kiasi cha kwenda nje ya key naye ni MPUMBAVU tu...
 
Makonda haruhusiwi kuingia US, kwa sababu ya "kuwanyima watu haki ya kuishi".

Muuaji mnamshauri akimbie bila ya kufikishwa mahakamani? Siungi mkono yeye kuviziwa mafichoni, lakini ni halali kabisa kwa yeye kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma dhidi yake.

Waliopo kwenye vyombo vya dola, wanaeleza kwamba mtu huyu aliongoza kikundi cha kuwateka, kuwaua na kuwapoteza watu waliokuwa wakimkosoa marehemu na serikali yake, na kwamba kikundi hicho kiliaminika na kupewa nguvu na marehemu kuliko taasisi rasmi ya TISS. Kikundi hiki kiliwajibika moja kwa moja kwa marehemu. Kikundi hiki, kwa kauli za Siro, zaidi kilifahamika kama "Watu Wasiojulikana", japo walikuwa wanajulikana.

Huyu ni vema akamatwe mapema, ajibu tuhuma dhidi yake, awataje watu wake aliokuwa akiwatumia kuendesha uharamia. Mmoja tunaambiwa yupo mahabusu kule Kusini mwa nchi kwa kosa la kumpora fedha mfanyabiashara na kisha kumwua.

Sabaya wakati akiwapora watu fedha kwa nguvu, alikuwa akiwaambia kuwa, hii inaitwa Makonda style! Sabaya naye ni shahidi muhimu dhidi ya Makonda.

Sanane kapotezwa
Azory kapotezwa
Kanguye kapotezwa
Lisu alimanusura
Mo alitekwa na kuachiwa
Roman alitekwa na kuachiwa
GSM waliporwa mamilioni ya pesa kwa vitisho mbalimbali
Mengi aliporwa mamia ya mamilioni kwa kudanganywa
Familia ya Chacha kule Mwanza waliporwa kiwanja Capripoint
Kuna watu wengine waliporwa fedha kwa ahadi kuwa ataongea na marehemu walegezewe kodi na wawe karibu na Serikali.

Makonda atendewe haki, asiviziwe mitaani, apelekwe mahakamani kama alivyofanyiwa Sabaya, akajibu tuhuma mbalimbali, ikiwemo za mauaji. Makonda ni mwovu mkubwa, kwa kiasi kikubwa, zaidi ya Sabaya. Mwanafunzi wake wa uovu, Sabaya, yupo jela, mwalimu wake yupo huru. Hii siyo haki.
Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga.

Ni wazi ana mwisho mbaya sana

Sioni kama ataponea kokote

Hata akikimbia nchi hitmen wako kibao dunia hii akipewa dollar 20k anamaliza mambo chap!!

Jamaa alikuwa Nazi kweli kweli yaangi thugocracy practitioner [emoji2]

Sitoshangaa akiwa hitter somewhere why not!? ..yeye mwenyewe hitted people from nowhere!! And felt proud about it .

Atajiju
 
ULIWAHI KUWAONA MATEJA? HAO WANAOSABABISHA HIYO HALI NA BASHITE YUPI BORA AISHIE NDUGU?
 
Back
Top Bottom