Naanza kuamini Bundi kulia usiku Mahali palipo na mgonjwa ni ishara mbaya

Naanza kuamini Bundi kulia usiku Mahali palipo na mgonjwa ni ishara mbaya

Kaka vipi kuhusu pakaa, mimi kwangu kila siku, masaa yote asubuhi, mchana usiku nje kwangu analiaaa.. Nyau nyauuuuuuuuu nyau nyauuuuu,ni paka mweusi, nikimfukuza hata dakika mbili haziishi anarudi tenaa,Wajuzi naombeninmnisaidie kwa hili tafadhali
 
UONGO bundi ni ndege tu hana hayo masuala ya mauzauza ni maruweruwe yako tu yanakusumbua

Na huu ndio ukweli hautaki beba bango andamana

Huku ninapoishi kuna bundi kibao wanalia usiku hakuna hizo Mambo za uchuro
Kisayansi mtu anapokaribia kufa hutoa harufu ya bakteria wanaokula sehem lain lain za mwili kama maini,utumbo mnene na mwembamba, na bundi ndie kiumbe mwenye uwezo wa kusikia haruf itokayo kwenye mizoga..na huita viumbe kwa mlio wake waje kusafisha mazingira kwa kula hiyo mizoga...

Jifunze kusoma maswala ya kisayansi...itakusaidia kuliko kubisha, na ukikuta ni kweli inabidi wewe ndio uandamane..
 
Ni UONGO bundi hana hizo Mambo kinachomfanya bundi afuatilie nyumbani kwenu anawinda PANYA sio habari za mtu kufa sijui mzoga kufanya nini hizo ni porojo tu hakuna ukweli wowote
Bundi hana mda na panya...anakula wadudu zaidi..
 
Bundi ananusa alafu na kuisi mzoga maana mtu uanza kufa taratibu hasa mgongwa na ndio maana bundi ulia sana kwenye nyumba zenye wagonjwa waliozidiwa.
Mbona mahospital hawendi na kila siku wagonjwa wanapelekwa
 
Bundi ni Ndege huyo wa kwako wewe wa kiimani ni wa Kamchape Lambalamba na hao mabwana wanaowalisha huo ujinga wameshapigwa marufuku wakionekana tena wanaleta Imani zao za ajabu ajabu kutisha watu na kuwabambika watu masuala ya UONGO UONGO wanaenda kunyea debe Segerea na Ukonga

Bundi ni Ndege km alivyo njiwa, mwewe, kunguru, na wengineo tofauti yake yeye anafanya mawindo yake ya kujitafutia kitoweo wakati wa usiku ndio anavishwa Imani za ajabu Ila ni Ndege tu
Mkuu Kama huwezi kufanya meaningful discussion bila kuanza kuitana majina au kuwashusha wengine, ingekuwa vyema ukachagua watani wako spesheli maana si kila mtu yupo jf kwa ajili hiyo including me 🙏🏽🙏🏽
 
Nakwambia kitu ninachokifahamu siropoki tu nakwambia huku nilipo Bundi wapo na wanalia usiku na hakuna hicho mnachokisema nyinyi mmekaririshwa UONGO
Mm bundi kashalia sana juu ya paa ya nyumba yangu tena 3 days..huu ni mwezi wa 3 hakuna cha nini wala nini....na hakukua na mgonjwa..so ni mind set na vile tuu watu venye wanawaza...
 
Ni UONGO bundi hana hizo Mambo kinachomfanya bundi afuatilie nyumbani kwenu anawinda PANYA sio habari za mtu kufa sijui mzoga kufanya nini hizo ni porojo tu hakuna ukweli wowote
Unaweza kuwinda panya ukiwa unapiga kelele na ukawapata? Hata paka akitaka kuwinda panya huwa anaenda kimya kimya sasa huyo bundi atakua ni kichaa kama anaenda kuwinda halaf anawastua panya Kwa kupiga makelele
 
Wanasema ndege huyo huwa ana uwezo wa kuhisi kifo. Habari hizi nilizisikia kwa baadhi ya wazee miaka ya nyuma kidogo nilikuwa kijiji kimoja huko Dodoma ndani ndani.
Tumekaa home kwa baby bundi kula siku analia. Huu mwaka wa 10 wale bundi wapi na watu hawafi
 
Unaweza kuwinda panya ukiwa unapiga kelele na ukawapata? Hata paka akitaka kuwinda panya huwa anaenda kimya kimya sasa huyo bundi atakua ni kichaa kama anaenda kuwinda halaf anawastua panya Kwa kupiga makelele
Wewe ndio kwisha habari kabisa yaan ulichoandika hapo usifute ili watu wajue kiwango cha utoto ulionao kichwani,

Bundi hawindi kwa makelele ushaelewa Bundi anawinda kimya kimya zile nyimbo anazoimba usiku ni km Ndege wengine wanavyoimba Ila yeye haimbi km kunguru 'KWOOO KWOOO KWOOOO' au njiwa wenu hapo mabanda ya uwani 'NKRUUU KUA NKRUUU KUA' ushaelewa au bado hujaelewa nikupe mlio wa Bundi anaimbaje 'KRUUUKU KRUKUKU KRUUUKU KRUKUKU' hivyo ndivyo anavyoimba Bundi endelea kujifunza

Unataka nikuwekee video au utaenda mwenyewe YouTube ukajihakikishie?
 
Mm bundi kashalia sana juu ya paa ya nyumba yangu tena 3 days..huu ni mwezi wa 3 hakuna cha nini wala nini....na hakukua na mgonjwa..so ni mind set na vile tuu watu venye wanawaza...
Ndio watu kutishana tu na Imani zao za ajabu ajabu Ila sababu ni mafundisho ya Mila, Desturi na Tamaduni za maeneo tofauti, wengine hio Imani haiwatoki kichwani wakisikia Bundi kalia juu ya paa wanajua humu ndani kuna mtu atakufa kumbe sio kweli ni UONGO
 
Kuhusu Roho hii ni elimu kuwa sana hii kuliko upeo wako ndugu


Sema babu na baba zangu walinikaririsha habari za roho lakini sina uthibitisho nazo.

Unatetea kitu ambacho hukijui na huwezi kukitetea.

roho ni stori kama ya serer mythology kule senegali
 
Back
Top Bottom