Nabii Josephat Mwingira anena Mazito kwenye Salamu za Heri ya Krismasi

Nabii Josephat Mwingira anena Mazito kwenye Salamu za Heri ya Krismasi

Mimi nitakufa siku yoyote and I don't care, nashukuru Mungu nitakufa na dhambi lakini siyo ya kuondoa uhai wa watu wala kuzurumu watu.
Kufa leo, huna faida kwa familia yako hadi taifa
 
Hivi je? Serikali hii:

1. haikukwiba kura?
2. haijabambikiza watu kesi?
3. haijapoteza watu?
4. haijadhulumu watu yakiwamo maisha yao?
5. haikuhusika na magenge ya wasiojulikana?
6. Nk. Msururu ni mrefu.

Kama majibu ni ndiyo basi kumbe aliyosema ni machache zaidi. Kama ndivyo basi lichumia tumbo ni wewe mjomba.
Mkuu The Sunk Cost Fallacy jibu hapa.
 
Yote tisa mia magufuri alikuwa na mapungufu ya kiongozi watu hawezi kuacha kusema. Ukiona watu wanaongea usidhani niwajinga wanaelewa. Kwenye issue ya vyeti fake mzee alikuwa na bias, rejea issue ya makonda. Issue za kukwepa Kodi mzee alikuwa na bias pia, rejea issue ya makontena barabarani. Kwenye issue za ufisadi alikuwa mnafiki tu, rejea report ya CAG, baadhi ya miradi kuzuia isikaguliwe. Acha ushabiki fungua akili yako Magu hakuwa Mungu alikosea mengi tu
Hayo mambo ya ukwepaji kodi namengine uliyo yaeleza yote tulielezwa bayana na nikweli watu walifanya nchi kama ya shangazi zao.

Sasa lete ushahidi wa ufisadi wa magu na nini kinafanyika kusawazisha hayo makosamengi, sio kujifanya ujuaji wakukosoakosoa mambo ya kipuuzitu bila akili.

Miradi yote mikubwa kabisa inaendelea kama kawaida mbona hatusikii kusitishwa kwa mradi hatammoja wenye tuhuma za ubadhilifu kwaajili ya uchunguzi, acheni kujifanya wajuaji.
 
Huyu mwizi wa wake za watu na sadaka! Ati nabii! Pumbaff
Ujumbe wake uko vipi lakini? Hili lichama lazima lipigwe spana za uhakika. Wizi wa kura wa 2020 hakuwa wa dunia hii. Hadi kina Mangula na Judge Werema wanaona kuna haja ya Tume huru ya uchaguzi (Katiba Mpya).

Watanzania wote tuseme Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
 
Kuna jambo uongozi wa juu serikalini unapaswa kufanya ili kuponya nafsi za wengi waliojeruhiwa.Kuudharau ukweli na kukaza shingo haitosaidia.
Hao wahuni wachache ni kama tone tu kwenye bahari!

Hao wahuni hakuna popote walijeruhiwa zaidi ya maslahi yao kuguswa tu basi
 
Salamu za Heri zinaendelea kumiminika. Hapa chini ni kutoka kwa nabii Mwingira:

View attachment 2058365

Salamu za kama hizi zinapoendelea kutufikia ni vyema kujitafakari. Ni wazi kuwa kama Taifa hatuko vizuri.

Walikuwapo kina Desmond Tutu, leo hatuko nao. Walifanya sehemu yao, wamekwenda. Angalia katika kuwaomboleza hakuna dongo hata moja.

"Tunayo ya kujifunza."

Kila mtu kwa nafasi yake anayo sehemu yake ya kufanya, atakayo kumbukwa nayo.

Ni wazi kuwa chuki tunazoziona kwetu ni matokeo ya kumea kwa mbegu zake tunazozipanda wenyewe.

Haki huinua taifa.

Barikiwa mtumishi wa bwana, nabii Mwingira.

=====

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/12/2021 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
SOMO: GIZA NA NURU.

Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”

Ninapoiona nchi ninaona muumbaji alifanya kitu, Mungu ndio mwenye mali lakini hapa tunaona giza liliruhusiwa kuwepo tangu mwanzo. Katika vyote vilivyokuwa vimeumbwa kuna kinachoshinda vyote ambavyo ni Roho ya Mungu ambayo hata giza liko chini ya mamlaka hiyo.

Mwanzo 1:3 “Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” Kwa nini alisema kuwe na nuru wakati mbingu na nchi ipo, giza pia lipo? Mwisho wa siku Mungu alitaka kitu kitokee kwa tangazo lakini vingine aliviumba tu na ikawa lakini kwa hili alitangaza. Nuru iko pale ili kufanikisha uzuri na ubora wa uumbaji wa Mungu;
• Nuru inafanya Mungu ajulikane kama Mungu na ubora wake.
• Nuru ipo ili uumbaji uoneshe ubora wake.

Haya mambo mawili giza haliwezi kufanya wala Roho ya Mungu lakini nuru inaweza.

Hapa tunaweza kuiona kazi ya nuru; Mithali 8:22-30 “………… Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi; Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake;” Hapa tunaona kuwa Nuru ni mtendaji na mboreshaji na Yeye ndiye mfanyaji wa mambo yaweze kuwa.

Wafilipi 4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Hapa anabainisha tofauti kati ya giza na Nuru, pasipo Nuru Mungu asingeitwa mwema, mzuri, Yeye ni wa rehema, asingeitwa ni wa fadhili wala asingeitwa ni wa upendo.

Hapa ndipo msingi wa kesho yako unapoanzia, unaanza wapi? Kwa wewe kufahamu ya kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi na kwamba hiyo nchi aliyoiumba ilikuwa ukiwa na utupu lakini pia kwenye hiyo nchi giza lilikuwepo lakini kwa kupitia uwepo wake (huyo giza) hakusababisha chochote kiwepo, kwa nini? Kwa maana yeye si halisi, hana kweli yoyote kwa maana yeye hana anachoweza kumiliki na ndio maana anaitwa mwizi.

Serikali yoyote isiyo na uwepo wa Mungu ni wezi na ndio maana wanaweza kuiba mpaka kura kwa maana ni wa ibilisi. Mungu akaona alete Nuru ili isababishe mambo kuwepo na utupu na ukiwa usiwepo.

Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”

Kazi ya giza ni uongo, wizi na uuaji, mwizi hazalishi chochote na ndio maana anaiba, mwongo hazalishi pia kwa maana hakuna kweli ndani yake.
Yaani huyu Nabii kanichosha kabisa. Hivi yeye alikuwa na ugomvi gani na serikali? Au kuna jambo anajihami kama ilivyokuwa kwa mh mbowe?? Ngoja tusubiri maana tangu enzi za JK
 
Hahahaaaa........ Chadema mnachekelea!
Dah! Ni furaha iliyoje kuona kumbe hata ma ccm yenyewe yanajua kuwa jambo jema, la haki, la upendo na kweli ni la chadema na ni furaha kubwa kwa wanachadema ila kinyume chake yaani jambo baya, la dhulumati, la chuki na la uongo ni la ccm hilo na ni furaha iliyoje kwa wana ccm!!!!
 
Wakwepa kodi wakubwa ni hao unaodhani ni wazalendo. Kama mtu analazimisha hawara yake apewe nyumba ya serikali. Kama mtu huyo huyo anatumia billions of shillings kutuletea Ferry isiyotembea, na baadaye kuihamishia jeshini ili isiongelewe . Eti ni kifaru cha kijeshi ! . Alikuwa na uzalendo gani huyo kuwazidi wpengine ?! Ukishaona mtu anampa mtoto wa dada kuwa paymaster general . Uzalendo happo ni zero

Vyeti feki na drs la saba hawakuingia kazini kwa kulazimisha. Ni mfumo uliowaingiza kazini. Badala ya kuwalaumu vyeti fake ungewalaumu waliowapa kazi.
Unamjua alie ruhusu nyumba za serikali wauziwe watumishi?, unamjua alie saini ununuzi wa hilo ferry?.
Swala la la pay master mtanzania yoyote mwenye sifa anaweza kufanya hiyo kazi.
Vyeti feki hakuna anaewalaumu wao ndio wanashinda humu kumlaani magu kwa kuwaondoa kazini maana waliingia kimagu mashi, sasa wanajiungu kuchafua kwa sababu ya chukiza maslahi.
 
Ujumbe wake uko vipi lakini? Hili lichama lazima lipigwe spana za uhakika. Wizi wa kura wa 2020 hakuwa wa dunia hii. Hadi kina Mangula na Judge Werema wanaona kuna haja ya Tume huru ya uchaguzi (Katiba Mpya).

Watanzania wote tuseme Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Na sisi wala hatusemi katiba mpya iwepo ili iiondoe ccm madarakani la hasha. Tunataka katiba mpya ili iweke mifumo wazi, ya haki na kweli ili vyama vyote vishindane kwa usawa kidemokrasi na kile kinachokubalika kwa wananchi hata kama ni hiyo hiyo ccm ndicho kishinde. CCM kinajinasibu kuwa ni chama kongwe chenye mtandao na wafasi nchi nzima lakin cha ajabu hakitaki uwanja sawa wa kupambana na hivi vyama vichanga visivyo hata na mtandao wala wanachama maeneo mengi ya nchi!!!!!
 
Kama mnaemuita mtesiwenu amesha kufa sasa mnataka maridhiano na nani wakati muhusika amesha kufa ama anawajia usingizini maana mnalopoka sana kama mmekatwa vichwa.

Subiri tukishtakiwa MIGA ndio nchi itapasuka upande mmoja tuuze tulipe fidia, vinginevyo utapasuka wewe.
Sasa wewe unajifanya unaweza kuwa na kauli za kijeuri na kifedhuli kuliko mwendasake?!!! Jifunze hata kwake, Mungu hadhihakiwi. Mwendasake alikuwa mbabe leo hii yupo wap? Achilia mbali kututolea maneno ya dhihaka na dharau kama haya kwako Sisi mpaka nyumba zetu katubomolea tumelala nje na watoto lakin bado tupo, yeye na maonevu na ubabe wake yupo wap??!!!!
 
Sasa wewe unajifanya unaweza kuwa na kauli za kijeuri na kifedhuli kuliko mwendasake?!!! Jifunze hata kwake, Mungu hadhihakiwi. Mwendasake alikuwa mbabe leo hii yupo wap? Achilia mbali kututolea maneno ya dhihaka na dharau kama haya kwako Sisi mpaka nyumba zetu katubomolea tumelala nje na watoto lakin bado tupo, yeye na maonevu na ubabe wake yupo wap??!!!!
Kwani kama amekufa ndio nini, ongea usiongee utakufatu kujadili kifo niujinga, duniani kifotu ndio kina guarantee kwahiyo hunahaja yakukiongelea chenyewe kipotu na hata huyo mwenda zake alishasema maranyingi tu kwamba atakufasikumoja acha uoga.

""Kama ulijenga kwenye hifadhi ya barabara nyumba ikabomolewa then hakuna haja ya kutoa malaana lukuki, lakini kama ulionewa tu kwa ubabe polesana ndugu namimi naumia pia kwahilo Mungu atakufanyia njia pasipo ""
 
Back
Top Bottom