Nadhani sasa mtaamini kwamba ule uliyoitwa mradi wa kimkakati, TUMEPIGWA

Nadhani sasa mtaamini kwamba ule uliyoitwa mradi wa kimkakati, TUMEPIGWA

Huyu ni ile familia ya wapigaji wa gas, ambao sasa hivi anafanya mbinu za kuchelewesha na mwishowe kuua kabisa mradi wa hydropower. ndio ubovu wa nchi zinazojiendesha kibinafsi zaidi kiasi kuwa kila kiongozi anapoingia anaanza mambo yake binafsi bila kuangalia masalahi ya taifa.
Jiulize aliyekuwepo alijali mwendelezo wa miradi na maslahi ya taifa au alibuni miradi yake
Vipi Samia nae akibuni ya kwake
 
Jiulize aliyekuwepo alijali mwendelezo wa miradi na maslahi ya taifa au alibuni miradi yake
Vipi Samia nae akibuni ya kwake
Aliendeleza Miradi yote aliyokuta, hata ile ilikuwa hoi bin taaban aliifufua na kuimalizia, kwa terminal 3 ilikuwa katika hali ngumu sana wakati anaingia, lakini aliimalizia. Kuna mradi mmoja tu ambao ulikuwa haujaanza, uliokuwa bado kwenye majadiliano ndio hakuendeleza akitaka majadiliano zaidi, yaani huo wa Bagamoyo ambao nadhani ndio unaolilia. Siyo serikali imeshaweka pesa kwenye mradi fulani halafu anakuja mtu anasema yeye hautaki mradi huo, na kuuacha ufe.
 
Matrilioni ya fedha tunayamwaga kujenga JNHPP lkn uhakika wa kuzalisha umeme hakuna.

Wenye dunia (wazungu) walionya kwamba ktk dunia ya leo inayokabiliwa na tatizo la "mabadiliko ya tabia nchi" umeme wa maji si wa kutegemewa tena. Tukawabishia. Kiko wapi Sasa?!

Kwa haya anayo yaongea PM kuna uzalishaji wa umeme utafanyika JNHPP?

View attachment 2012229
Labda ushirikiane nao kuloga. Mvua kuchelewa kujaza bwawa si hoja sana litajaa tu hata wazungu waloge nawe pamoja. Bwawa huwa halijazwi kwa msimu mmoja ni mingi ili uruhusu maji yaendelee kutiririka kuhakikisha shughuli za kilimo nk zinaendelea upande wa chini wa bwawa. Bwawa la 3 gorges la china walipiga kelele sana ambalo lilihusu hata kuhmisha binadamu lakini limekamilika na linaendelea kujazwa maji na kuanzakuzalisha umeme kwa vinu vichache. Ethiopia nako vivyo hivyo. Waethiopia wanagombana na watumiaji wa mto Nile wanaotegemea maji toka huko. Je unajua ktk mto CONGO kuna mradi wa kuzalisha umeme mwingi wa kutosheleza mataifa mengi yanayoizunguka? LAKINI MRADI UNAZUZUA KWA AJILI USIKAMILIKE NA KUSAIDI MATAIFA KUKUA KIUCHUMI.
 
Mkuu usifanye kama unaijua Rufiji pekee yako...ukweli gesi ndo suluhisho japo bei ila maji tumepoteza pesa nyingi sana kwa mradi wa miaka michache
Usilinganishe ruvu na Rufiji. Rufijini na issue nyingine.. Kama unabisha nenda pale Rufiji daraja la Mkapa halafu jizamishe uone kina cha maji yanayopita.
 
Mkuu usifanye kama unaijua Rufiji pekee yako...ukweli gesi ndo suluhisho japo bei ila maji tumepoteza pesa nyingi sana kwa mradi wa miaka michache
Nakumbuka mbunge mmoja huko mjengoni alisimama na kutoa dhana ya energy mix lakini alishambuliwa kama mpira wa kona na kwa kiwango cha kudhalilisha utu wake, usomi wake na hata uheshimiwa wake. Wakati kauli za kumdhalilisha zikitolewa yalipigwa makofi ya kutosha (kugonga meza) kuunga mkono kauli hiyo ya udhalilishaji. Clip hiyo inaweza kupatikana kwenye maktaba ya jukwaa hili kwa rejea. Sina uhakika kama mdhalilishaji alikuwa anaelewa somo. Hilo nimepita. Sasa na wewe unaleta hoja ya gesi asilia kuwa mwarobaini. Sasa tueleweje
 
Matrilioni ya fedha tunayamwaga kujenga JNHPP lkn uhakika wa kuzalisha umeme hakuna.

Wenye dunia (wazungu) walionya kwamba ktk dunia ya leo inayokabiliwa na tatizo la "mabadiliko ya tabia nchi" umeme wa maji si wa kutegemewa tena. Tukawabishia. Kiko wapi Sasa?!

Kwa haya anayo yaongea PM kuna uzalishaji wa umeme utafanyika JNHPP?

View attachment 2012229
Reactive approach.
 
Kama alijua alishindwa kuwa tambua kuwa uwanja was ndege Chato na mbuga za wanyama Burigi,no mradi was kijinga ....hili nalo linawezekana!
Ktk nchi maskini Kama Tanzania unaleta treni ya umeme.
Ndivyo itakavyo kuwa Bwawa la Umeme!
Hapa ndipo utajua namna binadamu tulivyo na tabia ya ubinafsi..wewe kwanza, kwemu kwanza wengine wasubiri.

Bado siamnini miradi hii ukiondoa huu wa reli ina manufaa kwa watanzania kwa kiwango cha kuwaondolea mzigo wa maisha.
 
Unaacha technologia current ya kauzalisha umeme ww unarudi miaka 100 nyuma kutumia hydroelectric power.
 
Pale maji hubaki kama mfereji tu kiangazi.

Huwezi tegemea umeme wa maji huku ukiharibu miti/mazingira.

Haya hiyo rufiji tutakuja kuambiwa kina kimepungua.
Sahihi kabisa pale Rufiji kiangazi maji yanapungua sana hata kwa miguu unatembea, sema tatizo mamba tuu. Kosa kubwa lililofanywa na awamu ya tano ni kutelekeza mradi wa gesi kuzalisha umeme. Mabwawa ya maji na huu ukame unaokuja tutapata tabu sana....watu wajiandae na kununua solar tuu.
 
Mto Ruvu hauna uhusiano wo wote na mto Rufiji. Mto Rufiji ndiyo mto mkubwa na mrefu kuliko mito yote nchini Tanzania na hata siku moja haujawahi kupungukiwa maji. Pale kwenye Stigler's gaudge ya mto huu ndipo tunajenga JNHPP. Great Ruaha ni moja ya tributaries zake kubwa. Mto huu haupitii DSM bali Mafia mkoani Pwani maili takribani 200 kusini ya DSM.
Nimekaa mikoa ya kusini for more than 5 years, nimevuka Rufiji tangia enzi za pantoni mpaka kwa mtumbwi pale pantoni inapozingua, na sasa daraja limeisha. Kipindi cha kiangazi maji hupungua sanaa, na sehemu nyingine unakatiza maji ya magotini. Pia miaka ya karibuni mafuriko ya mifugo ndiyo yamezidisha uharibifu kwenye huo mto. Hivyo hiki kiangazi kikikomaa mpaka mwakani na mvua za maana ikawa hakuna hali itakuwa tete sana.
 
Najaribu kupata muunganiko wa heading na mtiririko wa habari yenyewe nakosa.Labda sijaelewa kwa sababu ya ugumu wa bichwa mlio elewa msaada tutani!
Muunganiko uko. Heading imendaliwa na Makamba na mtirirko wa habari umeandikwa na kibaraka wake. Kwa kifupi kuna kampeni kubwa sana ya kutaka kuonyesha kuwa huo mradi haufai. Na mhusika mkuu ni hii awamu ya tano ya ''mshikizo'' ambayo inajiita awamu ya sita.
 
Effects of climate change are real and devastating indeed. Kujipa moyo kwamba ukame hautatokea ni sawa na kuchamba kwa kiganja bila maji huku ukiamini kwamba unajisafisha.
Wew nae na kingereza chako cha pre form one...hovyo kabisa.
 
Umepoteza muda bure kuandika gazeti hili. Kama lengo la serikali ni LNG, ili watu wapige, basi iwe hivyo. Hydropower itanyima watu upigaji.
Kwahiyo hapa ndipo ulipoishia uwezo wako wa kufikiri, sio?!

Eti Hydropower itawanyima watu upigaji... TOO LOW!!

Si nyie nyie ndo mlikuwa mnasema eti Mafisadi walikuwa wanaziba maji, lakini cha ajabu hata wakati wa JPM still umeme wa maji ulikuwa ONLY 36%!!

Na kama mliamini mafisadi walikuwa wanaziba maji, ina maana hayo ya Bwawa la Nyerere hayazibiki, au?!

In short, sio kwamba nimepoteza muda kuandika gazeti bali hilo gazeti limekuonesha ni namna gani ulivyo na mawazo finyu!!!
 
Muunganiko uko. Heading imendaliwa na Makamba na mtirirko wa habari umeandikwa na kibaraka wake. Kwa kifupi kuna kampeni kubwa sana ya kutaka kuonyesha kuwa huo mradi haufai. Na mhusika mkuu ni hii awamu ya tano ya ''mshikizo'' ambayo inajiita awamu ya sita.
Hivi ni wapi nyie watu paliposemwa Mradi wa Bwawa la Nyerere haufai?

Hivi ni wapi nyie watu ilipotangazwa kwamba Mradi wa Nyerere unasitishwa?

Yaani watu leo wasikague hata vyanzo vya maji eti kisa Mradi wa Bwawa la Nyerere?

Yaani leo hii kisifanyike kitu chochote nchi hii related na umeme... oh, wanaaka kuhujumu Bwawa la Nyerere!

Kuendelea kwa Mradi wa LNG, napo oh, "wanataka kuonesha mradi wa Bwawa la Nyerere haufai"

Mbona mna mawazo ya ovyo sana nyie watu?
 
Hivi ndugu yangu, ni kwamba hujui kuwa ni kuna bwawa la kuhifadhi maji linajengwa sambamba na na mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwenye hilo,

Au unamaanisha umeme utazalishwa mojamoja kutoka maji ya mto,

Nini maana ya bwawa.

Leo Leo tunategemea upungufu wa maji Dar kutokana na kutegemea maji ya mto yanayotiririka badala ya kuwa na bwawa la kuhufadhi maji kwanza,

Ujinga mtupu
Hivi ni nani mjinga kati yangu na wewe?

Kwani hilo Bwawa maji yake yatatoka wapi?!
 
Wewe ndio msukule!

Nani kasema mradi wa gesi usiendelee?

Hebu nioneshe!

Mleta mada na nae ni msukule vile vile kama ulivyo wewe, maana kichwa cha habari na kilichopo kwenye mada yake ni vitu viwili tofauti
Umewasome Misukule wenzako wanavyotoka povu baada ya kusikia majuzi kulikuwa na taarifa za mkataba wa Trillion 70?!

Au umekurupuka toka ulikokuwa unafugwa bila kujua mijadala inayoendelea?!
 
Back
Top Bottom