Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Status
Not open for further replies.
Nimefurahi kuona sasa JWTZ inajenga mtandao wake wa mawasiliano, kufikia 2015 JWTZ litakuwa na saver yake maalumu ambapo litaacha kutumia civilian network' kazi ya ujenzi wa minara imeanza kwakasi.

Hongera sana JWTZ.

Sasa na TISS waige mfano huo.

You take me by surprise!! kumbe bado wanajenga minara hadi sasa.

Yericko nashauri kuwa si sahihi hata kama ni uhuru wa kujieleza, kuelezea strategic plans za majeshi na taasisi za usalama. Unatoa taarifa za bure kwa taasisi za kijasusi. kumbuka wanaohamasisha uhuru wa habari na wa kujieleza wana malengo yao mengine pia. kuchuja masuala ya kujadili is part of human nature. Just an advise. I am sure even guys from tiss hawawezi kukueleza wana mifumo gani ya mawasiliano kwa kuwa tgey are not for Show.
 
Mkuu angalia mifumo ya CIA, CIU,M16 na hata CFO vipo wazi na ndio propaganda intelijensia yavyo,

Kile wanachokifanya Korea kaskazini oeo ndicho dunia ya tatu yakiulinzi inavyotakiwa kufanya.
 
Mkuu ueledi wa TISS ulionekana pale;

(1) Tulipouziwa radar kwa bei ya kuruka.
(2) Wezi wa EPA kushindwa kukamatwa
(3) Twiga kubebwa wazima wazima pale KIA
(4) Shimbo kujichotea yale matrilion atakavyo
(5) Wauzaji wa madawa ya kulevya kuendelea kutembea vifua mbele hapa mjini etc....

Ila kazi ya kuwatoa wananchi meno, kucha na sasa macho inaonekana. Nawapongeza sana TISS, najua majukumu yenu...

Hakika haya unayoyasema yanaiweka wazi taswira ya hii taasisi. Angalia mambo yanavyoenda kwa ujumla utagundua efficiency yao ipo kubwa katika kulinda watu ambao mbele ya jamii wanaonekana ni maadui zao wakubwa na wale ambao wanagusa maslahi ya hao wachache wako wa tupu na hakuna wakuwatetea wakati wao wanatakiwa kutoa ulinzi kwa pende zote ili wenye kupewa jukumu la kuadhibu wapate nguvu kuanzia raia hadi wenye dhamana ya kisheria kama majudge na mahakimu. Kuna nyakati unatamani kama ungekuwa na jinsi ya kuwavurugia huo ulinzi wa hao maadui bila kuwadhuru bali kuwaonyesha kuwa bila kufuata sheria nobody is safe lakini wapi inabakia kuwa wishful thinking itokanayo na kukosa uwezo wa kufanya hivyo...Tabia ya kulinda baadhi ya wahalifu ina concreatise ama reinforce hizo tabia mbaya za watu wenye nafasi nyeti kwakuamini kuwa they can do whatever they like bila kuguswa na chochote...Wakumbuke tu kuwa wanatujengea sisi raia tension isiyo na sababu pia kutu provoke hadi kujikuta tukiongozwa hisia zaidi kuliko uhalisia. Hizo associated emossions siku ziki changanyika na hofu itapelekea watu kusababisha mass destruction...

Mfano mimi naweza kuwa provoked na out of emossions nikajikuta na vunja shria inayoweza niharibia maisha..kwakua najua haki yangu kupatikana na pengine nikihisi sasa zamu yangu kung'olewa kucha kabla ya hicho kutokea naamua kujiangamiza pamoja na wale ninaodhani ndiyo kisababishi cha frustration yangu....Ndivyo inavyokuwa kwa wanaojilipua..

TISS historia ya nchi hii itawasuta nanyi wenye maisha marefu mtatamani kujichimbia chini kama hamta rekebisha haya mambo kabla hayajaenda kombo!
 
Hii Taasisi ni muhimu sana lakini inabidi ijitathimini upya, kama bado inafauata misingi ya utendaji kazi kama ule wa enzi ya Mwalimu Julius K . Nyerere.

Maana enzi ile kumjua nani ni TISS ilikuwa vigumu sana, hii ilifanya hata kazai yao iwe na ufanisi. Tofauti na siku hizi vijana walioajiriwa miaka hii TISS hawaoni shida kujitangaza hata kwenye Bar ili tu wajikweze mbele ya watu.

Hali hii inamfanya adui yako akufahamu kabla ya wewe kumfahamu matokeo yake ndiyo haya, usalama wa raia upo mashakani, kucha na meno zinang'olewa kila kukicha, watu kuuawa na kutupwa mitaroni sasa ni kawaida tu. TISS wetu wapo lakini wamebakia kupokea mishahara minono na kuishi maisha mazuri pale Makumbusho.

Japo umewasifia sana lakini wabadilike.
 
Mkuu angalia mifumo ya CIA, CIU,M16 na hata CFO vipo wazi na ndio propaganda intelijensia yavyo,

Kile wanachokifanya Korea kaskazini oeo ndicho dunia ya tatu yakiulinzi inavyotakiwa kufanya.

Its more of Economic Espionage than anything else nowadays!!!
 
Wa ndugu mm naomba kujuzwa hivi idara ya usalama wa taifa ipo chini ya wizara gani maana kuna wanaosema ipo mambo ya ndani kuna wanaosema ipo wizara ya ulinzi na wengine wanasema ofisi ya waziri utawala bora kwa anaejua tafadhari
 
Ofisi hizi ni baadhi tu ya nyingi zilizo chini
ya Rais :-

1. TISS
2. PCCB
3. TUME YA MAADILI YA VIONGOZI
4.TASAF
5.BEREAU DELIVERY UNITY
6.MKURABITA
7.

ZIPO NYINGI SANA ila namba 1&2 ndiyo
Rais kazikumbatia sana kuliko nyingine.
 
Wa ndugu mm naomba kujuzwa hivi idara ya usalama wa taifa ipo chini ya wizara gani maana kuna wanaosema ipo mambo ya ndani kuna wanaosema ipo wizara ya ulinzi na wengine wanasema ofisi ya waziri utawala bora kwa anaejua tafadhari
Ipo chini ya Ofisi ya Rais-Utawala bora. Nakupa assignment nyingine zaidi;
Ikiwa Idara ya usalama wa Taifa iko chini ya ofisi ya Rais-Utawala bora na kuna waziri katika ofisi ya Rais -Utawala bora, je Mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa anaripoti wapi moja kwa moja?? Kwa Rais au kwa Waziri wa Utawala bora?? Ikiwa anaripoti kwa Waziri, je waziri huyo ndiye ana mamlaka juu ya usalama wa nchi yetu?
Kama anaripoti moja kwa moja kwa Rais then kwanini kuna waziri chini ya Rais kuhusu usalama???
 
da mkuu hii asainimenti maksi ngapi??maana maswali yake magumu sana kujibu aisee
 
Ipo chini ya Ofisi ya Rais-Utawala bora. Nakupa assignment nyingine zaidi;
Ikiwa Idara ya usalama wa Taifa iko chini ya ofisi ya Rais-Utawala bora na kuna waziri katika ofisi ya Rais -Utawala bora, je Mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa anaripoti wapi moja kwa moja?? Kwa Rais au kwa Waziri wa Utawala bora?? Ikiwa anaripoti kwa Waziri, je waziri huyo ndiye ana mamlaka juu ya usalama wa nchi yetu?
Kama anaripoti moja kwa moja kwa Rais then kwanini kuna waziri chini ya Rais kuhusu usalama???
You are very brave hakuna wa kuweza kujibu swali lako, that is a story which will remain to be untold
 
du this is called think big.mkuu hapa kwanza mfumo wa utendaji wa tiss si wa kiuwizara ni katika kila kona na wizara zote hawa jamaa wapo lakini pia kwakuwa ni usalama wa taifa hili socially politically economically kuna mambo mengine ya kiutendaji ni raisi tu mwenye ruksa ya idhini haya ni baadhi tu lakini haimaanishi kwamba mkuchika hawajibiki kwa namna moja au nyingine.welcome for further thoughts
 
You are very brave hakuna wa kuweza kujibu swali lako, that is a story which will remain to be untold

Wewe ndo huwezi kujibu mkuu si kila mtu mweupe kichwani au kazaliwa juzi. Inabidi kwanza ujue Majukumu na dhumuni la kua na Wizara ya Rais Utawala Bora ndipo utajua kwann UWT ipo pale. Hii wizara ni km Custodian wa Idara na Taasisi flan flan ambazo zipo chini ya Usimamizi wa Rais Directly.

Tukichukua ile mihimili mitatu ya Serikali yaan Executive, Legislature & Judiciary UWT ipo ndani ya Executive. Na kwa sera za kiutendaji ndani ya Serikali Idara, Wizara au Taasisi zozote zilizopo ndan ya Executive lazima ziwe na Muongozo au policies ambazo zinakuwaga ni Guideline za Ilani za vyama. Hivyo mfano ilani ya CCM inatoa namna ya Utendaji wa Serikali yake katika mambo ya Miundombinu hapa Wizara Husika itakua ni Ujenzi sasa ikija Ilani ya UWT Wizara husika ndo itakua hii ya Rais Utawala Bora.

So Waziri yupo pale sio km Head wa Mkuu wa Usalama wa Taifa ila yeye anasimamia utekelezaji wa policy za chama tu! Na majukumu yoyote ya kiutendaji professionaly yanabaki kua kati ya Rais na Mkuu wa UWT including other Senior Officers huu mfumo upo hata katika Wizara nyingne mfano Ulinzi ambapo Waziri Nahodha ndio Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT lakini Mkuu wa Majeshi haripoti kwake anaripoti kwa Rais Direct hii ni kwasababu Waziri yuko pale kama Mkuu wa Sera za Chama ndio maana hauhitaji kua na Waziri mwenye profession na Wizara husika ispokua tu unahitaji mwanasiasa mahiri mwenye kujenga hoja nzur juu ya utekelezaji wa sera za chama.. Hii rule might be exceptional to some Ministries mfano Afya na Fedha.

Kwenye Wizara kuna mtu anaitwa Katibu Mkuu huyu anateuliwa na Rais pia na yeye ndio mtendaji Mkuu wa shuguli za kiprofesheni ndani ya Wizara lakini sio Waziri.
 
Kwenye Wizara kuna mtu anaitwa Katibu Mkuu huyu anateuliwa na Rais pia na yeye ndio mtendaji Mkuu wa shuguli za kiprofesheni ndani ya Wizara lakini sio Waziri.

mkuu lakin lazima ujue mawaziri si watendaji ni wasimamizi tu wa sera za serikali kwaiyo hapa swala la msingi ni kwann mkurugenzi haripoti kwa waziri
 
Serikali ya Kenya inakusudia kuifumua Idara ya Usalama ya nchi hiyo baada ya kushindwa kugundua na kuzuia tukio la kigaidi la utekaji wa jumba la kibiashara la Westgate.

Akizungumza katika bunge la dharura nchini Kenya,makamu wa Raisi mh.Rutto ameeleza nia ya serikali kuivunja Idara hiyo kwa madai imeshindwa kutimiza wajibu wake licha ya kutumia mamilioni ya hela za walipa kodi wa nchi hiyo.Makamu huyo wa Raisi ameonyeshwa kushangzwa na kutokea kwa tukio hilo wakati usalama wa taifa upo.

Mimi nafikiri kama ni udhaifu basi Idara ya Usalama ya hapa nchini kwetu itakuwa imezidi na pengine hata hiyo ya Kenya inaweza kuwa bora mara kadhaa ukilinganisha na ya hapa kwetu(TISS).

Ukweli ni kwamba kama ni matukio ya kuhatarisha usalama wa nchi na raia yameshatokea mengi tu na kama tungekuwa na kiongozi makini idara hii ingeshafanyiwa mabadiliko.Mfano wa matukio hayo ni kama wanyamapori wetu(maliasili ya nchi) kusafirishwa nje ya nchi tena kupitia airport zetu, mabomu kulipuliwa katika mikutano ya kisiasa,watu kuhifadhi mabilioni nje ya nchi,watu kung'olewa kucha na meno,watu kumwagiwa tindikali,ufisadi kama wa EPA n.k.

Tofauti ya sisi na wenzetu wa Kenya ni kuwa mara baada ya tukio hilo serikali imetangaza kupitia bunge nia ya kuchukua hatua dhidi ya usalama wa taifa ambapo sisi hapa serikali yetu hainyeshi kushituka wala kuchukua hatua dhidi ya Idara hiyo nyeti licha ya mlolongo huo mrefu wa matukio ya aina hiyo.Cha ajabu hata kelele zinazopigwa na watanzania kutaka uwajibikaji wa Idara hiyo nazo zinapuuzwa!

Kama serikali inahusika na matukio haya na ndio maana inashindwa kuchukua hatua hilo ni jambo lingine ila kama ni matokeo ya uzembe wa Idara hii ya usalama wa taifa basi hata usalama wa Raisi na Ikulu yake na wenyewe uko mashakani.

Raisi chukua hatua sasa na usiju kumbuka shuka wakati kumekucha!
 
kwani Tanzania kuna matukio gani makubwa ya kigaidi ambayo yamelenga kuiathiri serikali ya Tanzania? mbona mnapenda kushabikia na kulinganisha mambo ya nchi jirani ya Tanzania yetu? shame on you Salary Slip
 
Marekani waliporipuliwa Pentagon na world trade centre, walivunja intelligence units zao au waliziongezea nguvu?
 
mkuu haya matukio yanaweza kutokea mahala popote kwani hata marekani na uingereza ambako kiusalama wamezidi sana uwezo lakini yanatokea nadhani ruto ujana na kujishoo kunamsumbua.
 
ngoja ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe atawauliza wazambia miaka ile walikurupuka kilichowakuta walikoma wakaanza upya tena.
 
Idara ya usalama ya Tanzania ipo imara sana kuliko watu wanavyofikiri,

Tatizo la hapa nchini ni sheria tu inayoinyima mamlaka kamili idara hii,

Hatua hiyo inapelekea watawala/wanasiasa kupuuza ushauri mwingi unaotolewa na idara hii kama sheria inavyotaka na kujiwekea matakwa yao wanasia hawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom