Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Muongozo uliotoka NBS ni kwamba,,Wasimamizi wa Sensa ni Walimu Wakuu na Waratibu wa Elimu Kata tu kwa kila kila Kata,,kwahiyo kama wewe sio mwalimu mkuu na umeomba nafasi ya usimamizi hesabia umeliwa kichwa[emoji2163][emoji1],,

NBS watatoa majina ya waliopita katika usahili muda wowote kuanzia sasa,na usahili utafanyika rasmi tarehe 19 July 2022.Leo wamemaliza vikao vya mikoa kwa baadhi ya maeneo yamebaki mambo machache tu.Ila kila kitu kipo tayari.[emoji857]

Kila aliyeomba nafasi asikae mbali na simu yake au kompyuta yake asubiri kuvuna alichopanda maana wakati wa mavuno umewadia..Naomba kawasilisha[emoji120]
Nani anakupa hizi taarifa?
 
uku kwetu mzigo tayari kwenu bado sioo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG-20220715-WA0010.jpg
 
sioo utani masta hiyo ni kweli kabisaa

Ndo muwe mnasema ni wapi?
Utaratibu gani umetumika au unatumika huko ili na wengine wajipange.

Hii ya kusema kimenuka, oyaa mambo tayari, majina tayari nk..
Ndo inafanya jobless wengi kukosa fursa kwa kubaniana info ili tu aonekane ana info nyingi na watu kumzonga awaambie na wakati mwingine info zenyewe zinakua za uongo na anakufa na mafamba yake.

Haya tiririkeni hapa ..
 
Ni kweli majina yametoka kwa baadhi ya kata.

Majina yanabandikwa kwenye kata husika na sio kwenye website ya nbs.

usahili ni 19-21 kwenye kata.
 
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B anawatangazia wale wote waliomba nafasi za kazi ya muda kwa ajili ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 kwa nafasi za karani , msimamizi maudhui na Tehama kuangalia majina yao yaliobandikwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Magharibi B zilizopo Mwanakwerekwe karibu na kituo cha kuuzia umeme .

Wale wote wataoyaona majina yao wanatakiwa kufika katika usajili { Interview } utaofanyika Siku ya Jumanne tarehe 19/07/2022 katika Skuli ya Sekondari Aboud Jumbe Fuoni kuanzia saa moja na nusu asubuhi.

Aidha muombaji anatakiwa kuja na vyeti halisi vya kumalizia masomo na Kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi au Mtanzania.

Ahsante.

Imetolewa na :
Kitengo cha Habari na mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magh B
 
Back
Top Bottom