Vita ni kubwa baadhi ya Wilaya wanachelewesha majina Sababu ikiwa ni mvutano ya kuchomeka watu. Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi, meya, afisa elimu n.k kila mmoja ana wadau wake anahitaji wawemo kwenye mkeka. Ngumu zaidi watu hao waliomba usimamizi wa maudhui kwa kuamini kuwa wanakoneksheni za maana hawatokosa, lakini hali imekuwa tofauti nafasi hizo n chache mnoo zimebanwa na walimu wakuu kutokana na maelekezo ya Sensa.
Kinachofanyika ni kupindua meza tu, kuwahamisha hao wenye koneksheni hizo kutoka maudhui kwenda karani na hapo ndo kutokuelewana kunakuwepo maana kwenye ukarani wapo walioomba wa kutosha kabisa, hapahitajiki kuongeza watu mlowashusha daraja.
NB: Tuishi na watu vizuri, Sensa haikuwa na intavyuuuu....[emoji3][emoji3][emoji23]