Kwa mtazamo wangu ninavyo ona watu wote mnaosema kwamba kazi ya sensa wapewe watumishi wa serikari kwa kigezo eti itakuwa rahisi kuwapata sio sahihi kwa sababu zifutazo.
1.Kazi ya sensa safari hii inatumia vifaa vya kielectronic kwa hiyo sio walimu au watumishi wote wenye uwezo wa kutumia vifaa hivyo ipasavyo wapo vijana wengi walio maliza vyuo wanauwezo huo pia, kwanza nina ushahidi wa baadhi ya watumishi wa serikali walipo sikia maswala ya electrictonic, na interview waka kata tamaa hawakuomba.
2.Kwenye ile fomu iliyo kuwa ikijazwa kuna sehemu yalihitajika majina ya wadhamini wawili, namba zao za simu, Email na fingerprint. Pia muhuli na signature ya mtendaji wa kijiji ilihitajika, hawa watu wanatosha sana kama wakitaka kukutafuta, ingawa kwa taarifa za muhusika mkuu ni rahisi sana kukupata kama wakikuhitaji.
Kikubwa hapa tusubilie majina yatoke jamani, then tukanyooshane kwenye interview, maana kwa mujibu wa Msimamizi mkuu wa sensa mama Anna Makinda alisema watakao simamia ni wakufunzi(lecturers) kutoka vyuoni, tuombee yale mambo ya anwani ya makazi yasijirudie.
Sent from my SM-A225F using
JamiiForums mobile app