Kuna wengine wamesoma mpaka elimu ya juu zaidi (shahada, uzamili na uzamivu) ili wakaitumikie nchi jeshini kwa taaluma zao. Sasa kama humpi nafasi kisa elimu yake si mapuuza hayo aroooh ?
Jeshi linahitaji watu wote, wasomi wa ngazi za juu wakafanye kazi zinazowahusu jeshini, na waliosoma elimu ya ngazi za kawaida wafanye kazi zinazowahusu (kupigana mstari wa mbele vitani na majukumu mengine).
Riziki ya mtu kama ipo ipo tuu, na kama haipo, haipo pia ! Roho mbaya ya afisa wa jeshi anayefanya usaili haiwezi kumzuia mtu asiwe mwanajeshi au kutokuwa mwanajeshi wa Tanzania kwa namna yoyote.
Mungu ndio anayejua maisha ya kila mtu. Ni kumtegemea yeye tuu na kupambana kwa kadri ya uwezo wako. Mengine unamwachia yeye mwenyewe. Ndio maana jeshi likihitaji wasomì wanafanyiwa usaili na maafisa wa jeshi wasomi mpaka wa makao makuu ya jeshi na wana wanaandikishwa kunako jeshi la wananchi kama kawaida.