Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Na hilo ndiyo jeshi ambalo naona hata kujiendeleza kielimu ni ishu maana kule unasoma ili ukawe nani sasa
Kuna ma afisa mifugo , afisa kilimo watu wa misitu watu wa afya nakadhalika

Na wote wana application ndani ya jeshi hilo hadi walimu maana wana shule zao


Acheni hizi dharau jamani hili jeshi limebadilishwa kiasi kikubwa

Linajitegemea ,lina miradi na viwanda mbalimbali

Na watu wanasoma vizuri sana
 
Usikubali mtu akupe maoni....

Nakumbuka wakati naingia jkt nilikuwa na mentality ya kudharau vyombo vingine, lakini nilikuja kubadirishwa na Captain moja hivi...!!

Aliongea akasema, "Vijana haya mambo ya kudharau vyombo vingine vya ulinzi yanepitwa na wakati na ni mambo ya zamani na ya kishamba, nyakati zenu ni nyakati ngumu sana kwenye swala la ajira, na hakuna zoazoa kama zamani..usije hata siku moja ujachagua uende wapi nenda kokote as lilong as ni maswala ya ulinzi na usalama kwa sababu, Rais wet Magufuli amejitahidi kufuta gepu lililokuwepo kati ya vyombo vingine na JW".

Vijana wenzangu, ajira ni ajira tuu unapokuwa kwenye haya maswala ya ulinzi na usalama, hayo maswala ya status tuwaachie wenye fikra finyu lakini ukibahatika freshi.. Mimi napenda kuyaangalia zaidi maisha yangu kwa sababu muhusika ni mimi. Kokote kule nitaenda.

Namshukuru Mungu sasa kwenye pdf ya kwanza nipo na nawashukuru wanajukwaaa kwa kuendelea kutiana moyo!! Tuko pamoja na tutaendelea kuwa pamoja.
Na mwenye masikio asikie na mwenye macho asome
 
Back
Top Bottom