Sihitaji kutoa kashfa kwa wanasheria nawaheshimu nawatambua, ndo maana kuna umoja wa wanasheria. Tanganyika Law Society, na Lisu alishakuwa Rais wao. Kama Lisu angejua kuwa anaongoza wanasheria walio hivyo kama ulivyotaja. nadhani kusingehitajika kuwepo Chama cha wanasheria. Lisu angetosha Tanzania nzima yeye kama yeye kutokana na maneno yako.
Nacho fahamu Lisu anawaheshimu wanasheria wenzake na ndiyo maana kuna kesi kadhaa wamemwakirisha mahakamani. Na zingine kashirikiana nao. Sijawahi ona Lisu akidharau wanasheria wenzie kwa maneno kama yako.