Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Pole sana ndugu yangu, katika maisha mambo kama hayo hutokea, katika kila jambo linalotokea kuna jambo la kujifunza, naamini kwa msaada wa Mungu utayashinda kama usipozimia moyo, neno la Mungu linasema
Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
1 Wakorintho 10:13 BHN
Tafakari neno hili moyoni mwako, litakupa matumaini na nguvu ya kushinda,
Mungu ndie aliyekuumba, mrudie yeye maana alikujua tangia ukiwa tumboni mwa mama yako, anayo makusudi yake katika maisha yako, mrudie yeye maana hatma yako iko mkononi mwake, yeye ndiye rafiki wa kweli, ameahidi hawezi kukuacha, na hakuna jambo lisilowezekana kwake, mimi nitazidi kukuombea, nina hakika Mungu amesikia kilio chako, ubarikiwe!
 
Mkuu ni ngumu sana trust me, kipindi tuko ma young Pineus mshua alipitia situation ya aina hio.

Alikuwa very educated and exposed young man akala u GM Cotton board, kijana mdogo hela za kumwaga akija home kila jioni briefcase imejaa mipunga yani kama movie, gari enzi hizo ni Niva TX maisha yetu yalianzia almost City center Palm beach ndio sehemu ya recreation jioni miaka ya 80's hio. Wote Mshua na bi.mkubwa ni ma Lifeist kinyama young and very generous patners. Nyumba haikauki wageni on weekends ni kuku kwa kwenda mbele.

93" meza zikapinduka mzee akapigwa kadi nyekundu. Ghafla tukahamia Tabata porini sana enzi hizo uzuri alishajenga 2 houses na viwanja kadhaa alikuwa navyo. Alipitia kipindi kigumu sana 4 young kids and wife, bi. mkubwa hakuwa mbinafsi akapambana sana hadi kuja kukaa sawa on early 2000's ndio mshua akaanza mishe mishe upya. Almost puzzled and really fucked up for 7 yrs ndio kuja kuikubali hali. Too bad on 2001 we lost Mom and one bro! Ilikuwa pigo sana.

Maisha ni fumbo kubwa sana hujui ya kesho cha msingi getting prepared tu for the odds. Hii situation ilinifunza kitu.
 
Aisee
 
Huu ndo ushauri wangu uliokuja nikiwa nasoma huu uzi.

Pale kampuni yake ilivyokuwa inasuasua 2017, angeacha kazi akakomaa na uber.

Sahivi angeshapiga hatua kubwa sana tu.

Tena alikuwa na gari 3, zote angezigeuza uber sahivi asingeteseka kwa kiwango hiki.

Kwenye maisha inabidi uwe flexible sana. Usisubiri ikawa "too late".
 
Hii ni one side story, sidhani kama huyo mwanamke ni mbaya kiasi hicho. Hapo nakataa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kabisa mzee, hasa uwe na mke chuchunge na mbinafsi..Unaweza tamani israel apite na roho yako chap uamkie kuzimu.😂
 
Aisee
 
Kweli kabisa yani, siku hela zimekata hutamuona Juma wala Uledi kmmmke zao. Na shughuli itakuwa ni kukuponda huko walipo na pedeshee mwengine.😂😂😂

Mke nae ndio wale wale anafungasha virago akiona hela hamna. Badala mkae mjadili mfunguane mawazo mtatoboaje, yeye hilo anaona halimuhusu.
 
mkuu pole sana, ndio ukubwa huo[emoji52]
 
Exactly
 
Maumivu unayopitia yasikutoe kwenye reli ndugu.Wengi wamejikwaa pindi wanapopitia magumu maishani mwao.Wengine hufikia hatua ya kuzikabidhi nafsi zao kwa yule mwovu na kuamua kujitenga kabisa na neema ya Mungu muumba wao.Jifunze kuwa positive kwenye kila hali maishani.Usiishie kuyasikiliza maumivu tu,ukaacha kutambua thamani kubwa iliyobebwa na maumivu hayo.Kipindi unachopitia kina faida kubwa maishani mwako kuliko unachoona kuwa ni hasara. Faida mojawapo iliyo wazi kabisa ni kwamba umeweza kuwajua watu wako wa karibu kwa uhalisia wao. Binadamu wengi ni waigizaji. Wengi huficha uhalisia wa nia zao ili wapate wayatakayo kwa ajili yao wenyewe. Imagine umekuwa ukiishi na umezaa na mke ambaye haoni shida kukufanyia hayo anayokufanyia sasa. Na si ajabu alikuwa anakutamkia maneno matamu matamu pindi ukiwa "mambo safi". Pili,umejifunza maana halisi ya Upendo na Thamani yake katika maisha.Kupitia hilo umejua kwamba miongoni mwa hitaji muhimu kabisa kwa binadamu ni kupendwa. Umeweza kuwatambua wakupendao kwa dhati na wale wakupendao kwa hati.Nakusihi sana kwamba hali hii ikuweke karibu zaidi na Mungu especially kama kabla ulikuwa unamchukulia poa(Hii ni faida kubwa kwako tena ya milele,itakufaa ukiwa hai na hata baada ya kufa.Mahusiano yako binafsi na Mungu ni muhimu zaidi kuliko chochote na wakati mwingine Mungu huruhusu haya yatokee ili kukurudisha mikononi mwake). Umeshindwa kutambua kwamba moto huu unaoupitia sasa si kwa ajili ya kukuangamiza bali kukung'arisha zaidi na kukuandaa kwa future iliyo bora zaidi ndio maana ukafikiria hata kujiua ingawa Mungu kaingilia kati ili kukupa fursa ujifunze kusudi lake jema maishani mwako. Unachopaswa kujifunza ni kwamba katika maisha wakati mwingine mbegu ya kale haina budi kufa ili kuipa nafasi mbegu mpya kumea. Jifunze kuishi kwa kumtumaini Kristo Yesu katika maisha yako ili uwe na uhakika na maisha yako ya sasa na yajayo pia. Mungu angeweza kuzuia haya yasikupate kabisa lakini jiulize kwa nini kayaruhusu?. Ukipata jibu sahihi na kamili la swali hili amini nakuambia huzuni yako itageuka furaha ambayo hata kabla hujapatwa na taabu hizo hujawahi kuipata.Inua macho juu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Hawa qnet sjui gnld wamewatia sana umaskini watu anyway watu wenyewe ni wagumu kuelewa

Ova
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…