Wakuu naomba anayefahamu taasisi zitoazo mafunzo ya matumizi ya silaha hasa binafsi kwa hapa Dar
Nenda duka la silaha, mzinga au tanganyikaarms. Chagua silaha unayoitaka, lipia.
Chukua risiti ya malipo ya silaha hiyo na nyaraka zingine za utambulisho wa silaha hiyo kutoka hilo duka la silaha.
Nenda polisi na nyaraka hizo ili upewe fomu ya maombi ya kibali cha kumiliki silaha. Fomu hiyo ni bure, pia unaweza kuipakua kutoka tovuti ya Jeshi la Polisi (ila angalia kuwa unapakua fomu mahsusi kwani kuna fomu za waombaji aina zaidi ya moja).
Jaza fomu hiyo kwa maelekezo utakayopata polisi au kama fomu inavyojielejeza na ambatisha nyaraka zote hitajika.
Nenda kwa wakili akusainie sehemu yake kisha nenda serikali ya mtaa unapoishi ili kamati ya ulinzi na usalama ikujadili na kuipitisha fomu yako kama utakidhi vigezo.
Ukipita mtaa, peleka fomu yako katani ili nao wakujadili. Wakikupitisha;
Rudisha fomu yako polisi wilaya ambapo itajadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya. Ukipita;
Utaitwa mkoani ambapo napo utajadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa. Ukipita, fomu yako itapelekwa kwa DCI ambae, akiridhika, atakubali upewe kibali cha kumiliki silaha.
Ukishapata kibali, peleka maombi polisi ya mafunzo ya kutumia silaha.
NB: HUWEZI KUPATA MAFUNZO YA SILAHA KAMA HAUNA KIBALI CHA KUMILIKI SILAHA.