Nahitaji mtu mwenye wazo la Kibiashara ambalo litatusaidia kutengeneza pesa nyingi

Nahitaji mtu mwenye wazo la Kibiashara ambalo litatusaidia kutengeneza pesa nyingi

Je,unafahamu Tooth Pick Kwa Kiswahili inaitwa "Kimbaka",Kuna muda nawashangaa sana BAKITA na haya Majina Yao!


Any way


Wakuu nahitaji mtu yeyote mwenye wazo la Kibiashara ambalo liko tofauti na biashara ambazo zimezoeleka hapa Bongo!,Binafsi ninafanya biashara ya nafaka,pia Nina mashamba makubwa nalima,hivyo nikaona angalau tusaidiane na Vijana wenzangu ambao Wana mawazo na wameshindwa kuyafanyia kazi!

Nahitaji wazo hasa likiwa la kiteknolojia itakuwa poa sana!

Mtu aje na wazo na alitolee ufafanuzi namna wazo lake hilo litakavyoisaidia Tanzania au Afrika Mashariki kutatua changamoto,sitaki tuanze mbali Bali nataka tuanzie hapa hapa Tanzania Then tutafika Afrika Mashariki yote!

Binafsi nitatoa kiasi chote kitakachohitajika,pesa ipo ya kutosha na nimejipanga Kwa yeyote mwenye wazo zuri la biashara nzuri,maana kila nikaingalia naona wafanya biashara wengi ni kama wanaigana tu!

BIASHARA AMBAZO SIZITAKI

1.Biashara ya Nafaka (Hii naifanya na naijua nje ndani)

2.Biashara ya Usafiri
3.Biashara ya Viwanda vya Maji na Juisi
4.Biashara ya Mavazi
5.Biashara ya Nyumba au Real Estate (Hii naifanya na naifahamu nje ndani)
6.Biashara ya Wanyama (Ufugaji)

Akitokea mtu mwenye wazo la Biashara ya kiteknolojia nitafurahi zaidi!

Mtaji nilionao haupungui Tsh 500 milioni!

Kijana mwenye Idea hebu Lete wazo lako naamini tukaunganisha nguvu tutaweza!
Ninazo idea nyingi sana hata danguro litaingiza pesa zakutosha
 
Hakuna wazo jipya biashara nyingi ni zile zile isipokuwa inatakiwa upate mtu mwenye kujua siri za mifumo mipya wanayohitaji watu katika kufanya biashara hizo hizo zinazofanywa na wengi
Kumbuka watu walishafanya utafiti ikaja kugundulika pamoja na ukuaji mkubwa wa technology lakini binadamu ameweza kutumia asilimia 5 tu ya uwezo wake
Sasa ukiona mtu anafanikiwa biashara flani ujue katumia asilimia 5 ya mawazo tu 95% ya mawazo bado hayajatumika
Mim naonaga wanaongea, ila duh kuja na new idea ni issue nen
 
Brother,
Naitwa ✍️ Dr am 4 real PhD,
Nipo dar es salaam Tanzania 🇹🇿 Mimi ni mtendaji mkuu (management)

Nina data Nina files Nina MAARIFA utajiri kwa MAARIFA niliyo nayo ni ku copy na ku paste..

Mimi sito kutafuta ikikupendeza zama inbox nicheki wewe then Mimi nta present Kwako with viviv details.

Tunakosa information muhimu Sana za biashara Nina degree Zaid ya moja nime graduate practically kwa Sasa kwenye hii industry kwangu ni ku copy na ku paste utajiri.
Siamimini katika degree naamini katika akili, kama una copy na kupaste basi hujue hujakomaa akili.
 
Back
Top Bottom